Friday, September 27, 2013

KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI WA MWANANCHI VENANCE GEORGE.

Marehemu Venance George.
Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communication Limited Venance George, jana alipoteza maisha akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alipokuwa amelazwa.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu, Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaye kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.

Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na watoto wawili wa kike na wa kiume.
 
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.
ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya msingi.

-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.
AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi wa habari katika kampuni ya,
 -Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo katika chuo kikuu huria cha Tanzania ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka huu 2013.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...