Sunday, August 18, 2013

VIDEO YA YAHAYA - LADY JAY DEE HII HAPA.

WAHAMIAJI HARAMU 8,666 WAREJEA MAKWAO MKOANI KAGERA, CHELSEA 2 - HULL 0.

Kutoka Kagera.
Serikali Mkoani Kagera imesema mpaka sasa wahamiaji haramu wapatao 8,666 wameshaondoka na kurejea nchini kwao ambapo kati yao 500 ni Waganda na silaha zipatazo 43 zimesalimishwa.

Kutoka Uingereza
 Katika Ligi kuu ya Uingereza,Tottenham 1 - Crystal Palace 0
wakati katika mtanange kati ya Chelsea vs Hull City matokeo ni Chelsea 2 - Hull 0

ALICHOKISEMA ZITTO KABWE LEO.

Katika moja ya maazimio ya Kamati za Bunge za mahesabu ya Umma (Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Bajeti) iliamuriwa kuwa Serikali ianze utaratibu wa kukusanya maduhuli yake kwa kutoa risiti za kielektroniki. Azimio hilo linasema
“Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki. Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.”
Nimepitia Mpango wa Serikali wa Mapato (Volume I – Financial Statement and Revenue Estimates 2013/14) na kugundua kuwa mapato yasiyo ya kikodi yamekadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 741 kutoka Wizara, Idara na Mikoa na shi...lingi bilioni 383 kutoka kwenye Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa. Sikuweza kupata mapato ya Mashirika ya Umma maana hayaletwi kwenye Bajeti za Serikali.
Wizara 10 zinazoongoza kwa Mapato (mapato kwenye mabano ni Wizara ya Nishati na Madini ( 220 bn), Wizara ya Fedha (126bn), Wizara ya Ardhi (100 bn), Wizara ya Maliasili (84 bn), Wizara ya Mambo ya Ndani – Uhamiaji (92 bn), Wizara ya Mifugo (19 bn), Wizara ya Mambo ya Nje (16 bn) na Wizara ya Mambo ya Ndani – Polisi (17 bn), kati ya hizi shilingi 16 bilioni ni kutoka idara ya Trafiki (traffic notification fees).
Kutokana na mafanikio ya makusanyo ya VAT ambapo inaonyesha kuwa mapato ya Serikali yameongezeka kwa asilimia 60 (kutoka 500 bn mpaka 800 bn), na kutokana na rekodi mbalimbali za Serikali zinazoonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya makusanyo ya Serikali hayafiki Serikalini, ni dhahiri kuanzishwa kwa makusanyo kwa risiti za kielektroniki kutapandisha mapato ya Serikali zaidi ya mara mbili. Idara ya Usalama barabarani peke yake inasemekana kuwa makusanyo ya sasa ni theluthi tu ya makusanyo stahili kutokana na rekodi za ‘notifications’ barabarani.
Risiti za elektroniki kwa kukusanya maduhuli ya Serikali yanaweza kuongeza mapato ya Serikali maradufu na kuepuka mtindo wa Serikali wa kupandisha kodi kwenye bidhaa muhimu kwa wananchi. Uamuzi wa Kamati za Bunge za Mahesabu wa kuitaka Serikali kukusanya maduhuli yake kwa kutumia risiti za elektroniki unapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania.
 
Zitto Kabwe

Einstein Postdoctoral Fellowship Program for International Applicants in USA, 2014.

The National Aeronautics and Space Administration (NASA) are funding ten Einstein postdoctoral fellowship programs for pursuing research that is broadly related to the science goals of the NASA Physics of the Cosmos program. International applicants are eligible for this postdoctoral fellowship. The duration of funding is about three years which covers annual stipend, plus health insurance, relocation costs and provides funding for research related travel, computing needs and other research costs. The fellowship is awarded on the basis of the applicant’s research proposal as well as the curriculum vitae, list of publications, summary of previous and current research and three letters of reference. The online application should be submitted by November 7, 2013.
Study Subject(s): The fellowship provides an opportunity for highly qualified, recent postdoctoral scientists to conduct independent research that is broadly related to the science goals of the NASA Physics of the Cosmos program.
Course Level: This fellowship is awarded for pursuing a postdoctoral program at Host Institutions in USA.
Scholarship Provider: The National Aeronautics and Space Administration (NASA)
Scholarship can be taken at: USA
Eligibility:- Applicants must have received a Ph.D., Sc.D., or equivalent doctoral-level research degree in astronomy, physics, or a related discipline after January 1, 2011.
-Applicants who have not yet formally received their degree must present evidence of having completed the academic requirements before commencing the Fellowship.
-Einstein Fellowships are open to citizens of the United States and to English-speaking citizens of other countries.
-Non-US applicants should read the VISA requirements under the “Additional Information” section below before applying. [Note: The United States is defined as the 50 states and the District of Columbia.] Qualified applicants will receive consideration without regard to race, creed, color, age, sex, or national origin.
-Women and minorities are strongly encouraged to apply.

MBOWE AWAKARIBISHA CHADEMA MADIWANI WALIOTIMULIWA CCM MKOANI KAGERA, AWAPA MBINU

MADIWANI wanane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Kagera waliofukuzwa uanachama wiki iliyopita wamekaribishwa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ndiye aliyewakaribisha madiwani hao wanaosubiri kufukuzwa rasmi na vikao vya Kamati Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika wiki hii mkoani Dodoma.
Madiwani waliofukuzwa na kata zao kwenye mabano ni Richard Gaspar (Miembeni), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni naibu meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uhuru wa Bukoba Mjini, Mbowe alisema CCM imewachakachua madiwani hao wanane na hata wakibaki huko chama chao hakitawaona wa maana, kwa sababu chama hicho kinalea ufisadi.
Mbowe alisema CHADEMA wako tayari kuwapokea madiwani hao waliofukuzwa na kuwafundisha siasa za mageuzi.
“Tutasimama nao katika kujenga Bukoba mpya isiyo na ufisadi kama unaofanywa na Meya wa manispaa hiyo iwapo wataamua kuja kwetu, milango ipo wazi nawakaribisha,” alisema.
Mbowe alisema CHADEMA kinamuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (CCM), anayepinga ufisadi unaofanywa na meya kutoka chama chake, Anatory Amani.
Alisema CHADEMA itashirikiana na kiongozi yeyote kutoka CCM atakayekuwa tayari kupambana na ufisadi ulioshamiri kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
“CHADEMA katika mambo ya ufisadi ina msimamno unaoeleweka na kwamba katika kupinga ufisadi kipo tayari kumuunga mkono yeyote bila kujali itikadi,” alisema Mbowe na kusisitiza kwamba hata kama meya angekuwa mwanachama wa CHADEMA kingeunga mkono afukuzwe.
“Hatuna masilahi ya kisiasa na Kagasheki lakini katika suala hili tunamuunga mkono. Nawapongeza madiwani wetu wa CHADEMA walioungana na mbunge huyo kupinga ufisadi wa meya na kusimamia masilahi ya wananchi wa Bukoba Mjini,” alisema Mbowe.
Mbowe aliikejeli CCM kuwa haiwezi kuwafukuza madiwani hao kwa sababu itakuwa imejimaliza na hawana uhakika wa kuzirejesha kata hizo ukiitishwa uchaguzi.
Alisema kutokana na hofu hiyo Makao Makuu ya CCM yaliamua kuwarejesha madiwani hao wanane waliofukuzwa na CCM Mkoa wa Kagera.

Thursday, August 15, 2013

KAULI YA ZITTO KABWE JUU YA VIONGOZI KUWEKA WAZI MALI NA MADENI YAO.

Mbunge wa Kigoma kaskazini mh.Zitto Kabwe katoa maoni yake juu ya uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kama ifuatavyo:-
" 'Uwazi wa mali na madeni ya viongozi ni moja ya hatua muhimu kupambana na ufisadi' nimemwambia leo Mama Salome Kaganda wa Sekretariat ya Maadili ya Umma.
Wanasiasa tunajaza fomu kutangaza mali na madeni yetu. Fomu hizo haziwekwi wazi kwa wananchi. Utajuaje kama Kiongozi kasema uwongo? Utawezaje kupambana na uzushi na uwongo dhidi ya viongozi waadilifu lakini wanachafuliwa na wapinzani wake kisiasa? Suluhisho moja tu. UWAZI. Daftari la mali na madeni ya viongozi liwe wazi kwa wananchi. Fomu za mali na madeni ya viongozi wa umma ziwe online. Kiongozi asiyetaka mali na madeni yake kujulikana, akauze vitumbua aache uongozi, hakuna atakayemgusa!
"
Source:Zitto Social media.

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES SUA.

 Employment Opportunities

The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites qualified Tanzanians to apply for positions for Tutorial Assistants (TA’s) (<35 yrs of age) and Assistant Lecturers (<45 years).
Applicants are advised to note that the minimum GPA of 3.8 or an average of B for unclassified degrees such as that of Veterinary and Medical graduates at undergraduate level applies for TA’s and 3.5 at BSc/BA level or equivalent (i.e. an average of B for Veterinary and Medical graduates) and a good Masters degree is applicable for those with postgraduate qualifications. Only registered Veterinarians will be considered for interviews.


During application the applicant should state the Department, Position and Discipline one is vying for. Applicants are advised to note that salary packages and fringe benefits shall be as per Treasury Registrar’s Salaries Circular No. 3 of 2013.
The deadline for submission of application letters indicating names and addresses of two referees, together with certified copies of certificates and transcripts, curriculum vitae shall be two weeks after the first advertisement. Only short listed applicants will be contacted for interview. Those who had applied for similar posts in the past are encouraged to apply.
Application letters to be sent to the undersigned.
A: ACADEMIC POSTS
1. DEPARTMENT OF AGRICULTURAL ENGINEERING AND LAND PLANNING
Lecturer (1 Post) in the discipline of Farm Machinery and Mechanization for applicants in possession of a PhD in the area related to Farm Machinery and Mechanization. At undergraduate level the applicant should have a BSc in the areas related to Electro – Mechanical Engineering/ Mechanical Engineering/ Agricultural Engineering and at MSc in the area related to Agricultural Machinery and Mechanization. Those working in the industry are encouraged to apply.
Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Irrigation and Water Resources Engineering for applicants in possession of a Masters degree in Irrigation/ Water Resources Engineering and a BSc in Agricultural Engineering/ Civil Engineering – Water Resources or related fields. Those working in the field and industry are encouraged to apply.
Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Commodity Processing and Post Harvest Technologies for applicants in possession of a BSc in Processing Engineering/ Chemical and Process Engineering or related field.
2. DEPARTMENT OF SOIL SCIENCE
Tutorial Assistant (1 Post) in the discipline of Soil Microbiology for applicants in possession of a BSc in General Microbiology or BSc. Soil Science/Agronomy/ Horticulture with relevant courses in Soil Microbiology/ Biochemistry/ Soil Biology/ Soil Science.
Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Structural Geology for applicants in possession of a BSc in Geology and an MSc in Structural Geology/ MSc Geology.
Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Soil Physics/Soil and Water Management for applicants in possession of a BSc in Soil Science/Agronomy/ Agriculture General/ Horticulture with relevant Soil Science courses in Soil Physics/Soil and Water Management/Land Management, and an MSc in Soil Physics/ Soil and Water Management/ Soil Science and Land Management with a bias/major in Soil Physics and or Soil – Water Management.
3. DEPARTMENT OF AGRICULTURAL ECONOMICS AND AGRIBUSINESS
Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Accounting and Finance for applicants in possession of a Bachelors degree in Accounts and Finance and a Masters degree majoring in Finance/Accounts. Possession of a CPA (T) will be an added advantage.
Assistant Lecturer (2 Posts) in the discipline of Agricultural Economics for applicants in possession of a honors degree in Economics/Agricultural Economics and a Masters degree in Economics/ Agricultural Economics majoring in Environmental and Natural Resource Management/ Farm Management/ Agricultural Marketing/Agricultural Policy and Trade.
Lecturer (1 Post) in the discipline of Business Management for applicants in possession of a honors degree in Business Administration/ Economics/Agricultural Economics and a Masters degree majoring in Human Resource Management/ Business Law with a PhD majoring in Human Resource Management/ Finance/ Marketing/ Agribusiness and Entrepreneurship Development.
Lecturer (1 Post) in the discipline of Agricultural Economics for applicants in possession of a honors degree in Economics/Agricultural Economics and Master in Economics/ Agricultural Economics majoring in Price Analysis/ Quantitative Methods and a PhD majoring in Agricultural Policy and Trade/ Agriculture and Rural Development/ Agribusiness Management/ Production Economics.
DEPARTMENT OF AGRICULTURAL EDUCATION AND EXTENSION
Assistant Lecturer (1 Post) in the discipline of Community Development for applicants in possession of a BSc. Agricultural Education and Extension/ BSc Community Development/ BSc. Agricultural Extension and an MSc in these areas.
Lecturer (1 Post) in the discipline of Community Development for applicants in possession of BSc in Community Development, MSc in Agricultural Education and Extension/ Community Development and a PhD in Agricultural Education and Extension/ Community Development.

TANGAZO LA UCHAGUZI TFF

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
14/08/2013

1.                   Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF utafanyika tarehe 20/10/2013 jijini Dar es salaam. Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za uongozi wa TFF wanataarifiwa  kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe  20 Agosti 2013 katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya  Fedha), kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti 2013.

2.                   Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni:

(i)                   Rais wa TFF.
(ii)                 Makamu wa Rais wa TFF.
(iii)                Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, nafasi kumi na tatu (13).

3.                   Mtu yeyote  anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti yafuatayo:

(i)                   Awe Raia wa Tanzania.
(ii)                 Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari.
(iii)                Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)               Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)                 Awe na umri wa angalau miaka 25.
(vi)               Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza.
(vii)              Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi.
(viii)            Mtu anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa TFF lazima awe na kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

4.                   Ada za Fomu za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo:

(i)                   Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano (Tshs. 500,000/=).
(ii)                 Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi Laki Tatu (Tshs. 300,000/=).
(iii)                Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
5.                   Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

KAULI YA NAPE NAUYE WAKATI CCM TAIFA IKIWAREJESHA KAZINI MADIWANI 8 WALIOFUKUZWA BUKOBA.

TANGAZO LA USAILI WA ANA KWA ANA UTUMISHI

Tangazo la Usaili wa ana kwa ana kwa  kada ambazo Usaili wake utafanyika  katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni tarehe 15 na 16 Agosti, 2013.
Mnajulishwa kwamba wasailiwa wa kada zifuatazo usaili wake utafanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam kuanzia saa moja kamili asubuhi kama ratiba ya Usaili Inavyoonyesha.

15 Agosti, 2013

1.    Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta
2.    Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba
3.    Msaidizi wa Mthamini Jiolojia
4.    Nahodha na
5.    Afisa Vipimo

16 Agosti, 2013.
1.    Fundi Sanifu Haidro jiolojia
2.    Mthamini
3.    Mjiolojia
4.    Mkadiriaji Ujenzi na
5.    Afisa Sheria

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Ofisi ya Raisi Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  14/08/2013.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...