Polisi Mkoani Arusha inawashikilia watu 8 kwa
madai ya kuhusika na mlipuko wa jana siku ya jumapili katika kanisa Katoliki
la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne (4) wa Saudi Arabia, na wengine wanne (4) ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa
BBC Baruan Muhuza
akuzungumza akiwa hospitalini mjini Arusha amesema idadi ya watu
waliofariki dunia kufuatia mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama
ilivyoripotiwa hapo awali.
Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni kilipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la
tukio mbali na majeruhi hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia
sakafu na kuta za kanisa hilo hazikuchimbika sana.
Kutoka Dar es Salaam
Leornad Mubali
anaongezea kuwa watu wawili sana wamethibitishwa kufariki dunia katika
mlipuko huo uliotokea majira ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki
la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa
kujeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo
maalumu ya uzinduzi wa parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi
wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni
paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo
unapotokea walikuwa tayari katika hatua ya kubariki maji kwaajili ya
uzinduzi wa kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi wa Papa Fransis.
Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa
taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali
watu kati yao wamefariki huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali ya Mount Meru mjini Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo
zimesitishwa huku watalaalamu wa milipuko na polisi wakiendelea na
uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo
halisi cha bomu hilo ama kundi lolote linalodaiwa kuhusika na utegaji wa
bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini
Tanzania japo kuwa mwaka huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji ya Padre
wa kanisa hilo visiwani Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa
anajiandaa kuingia kanisani.