Wednesday, May 8, 2013

MAHAKAMA KUU IMEFUTA KESI YA UGAIDI KWA LWAKATARE.

Mwandishi wa blogu hii ameripoti kutoka mahakama kuu kuwa, leo Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
 
Kwa taarifa hiyo kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
 
Taarifa zaidi zinasema kuwa ilikuwa ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
 
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

MTOTO WA MIAKA 3 AKUTWA AMEKUFA MTO MOROGORO.


Mtoto mwenye umri wa miaka 3 aitwaye Issa Iddi amekutwa amekufa katika mtkondo wa mto Morogoro eneo la Mafisa karibu na Mabwawa ya majitaka yanayomilikwa na MORUWASA.Tukio hilo limetokea leo asubuhi ambapo wakulima wa mpunga wamekuta maiti ya mtoto huyo imenasa.
Maiti ya mtoto Issa Iddi aliyekutwa amekufa mto morogoro.
Bofya Read more kuendelea.

WATU 55 WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA BOKO HARAM

Watu waliokuwa na silaha nzito jana wamekishambulia kituo cha polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na kuwauwa watu 55, ikiwa ni pamoja na polisi na raia. Msemaji wa jeshi Musa Sagir amesema shambulizi hilo lilifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu katika kituo cha polisi cha mji wa Bama, jimbo la Borno, lilisababisha vifo vya polisi 22, maafisa 14 wa gereza, wanajeshi wawili na raia wanne. Musa amesema wafuasi 13 wa kundi hilo pia walikufa katika shambulizi hilo. Kiasi ya wafuasi 200 wa kundi la Boko Haram waliokuwa na silaha nzito wanaripotiwa kuwasili wakiwa na bunduki kabla ya kuushambulia mji huo. Wapiganaji hao waliokuwa na magari aina ya pick up, kwanza waliishambulia kambi ya jeshi na kituo cha polisi kabla ya kulivamia gereza. Hakuna kundi lililotangaza rasmi kuhusika na shambulizi hilo, ijapokuwa jimbo la Borno ni ngome ya kundi la Boko Haram, ambalo maafisa wanasema ndilo lililofanya shambulizi hilo.

Source: DW

HATIMA YA LWAKATARE NA ZOMBE KUJULIKANA LEO.

Wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikitarajiwa kutoa uamuzi wa maombi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare leo, pia itasikiliza rufaa ya kesi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe.
Lwakatare na mwenzake, Ludovick Rwezahula Joseph wanakabiliwa na kesi ya ugaidi, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 18 na kusomewa mashtaka manne yakiwamo ya ugaidi.
Taarifa zilizopatikana jana kutoka Mahakama Kuu na kuthibishwa na mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, zilisema uamuzi wa maombi hayo utatolewa na Jaji Lawrence Kaduri leo saa 3:00 asubuhi.
Kuhusu Zombe, Mahakama Kuu itaamua ama kutupiliwa mbali, au kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.
Zombe alikatiwa rufaa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese, Dar es Salaam.


Chanzo:CHADEMA social media.

Tuesday, May 7, 2013

MSc SCHOLARSHIP AT SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA)

                                 
                                              
                                                                 Announcement
                              MSc scholarship at Sokoine University of Agriculture (SUA)

Sokoine University of Agriculture (SUA) calls for application for a two year full-time MSc (Forestry) Scholarship attainable at SUA in 2013/14 academic year. The scholarship is fully funded by SUA and the successful candidate will specifically research on Cypress aphid (Cinara cupressivora) problems in Tanzania.

Eligible candidate
The applicants must hold BSc (For) degree (upper second or first class) from SUA or any other University recognized by SUA and MUST have an admission for MSc (For) at SUA for 2013/14 academic year. In addition, applicants with excellent grades (B+ or A) in Forest protection and Silviculture courses will have an added advantage.

Conditions and modalities
The scholarship covers tuition fee, accommodation, books, research and allowances as provided in the SUA Regulations and Guidelines for Higher Degrees.

When and how to apply
Applications to be submitted directly to the Dean, Faculty of Forestry and
Nature Conservation, Sokoine University of Agriculture, P.O. Box 3009, Morogoro, Tanzania.

Deadline for application: 30th August, 2013 and that late applications will not be considered.
The application must be submitted with the applicants CV and relevant copies of academic certificates. SUA will inform the successful applicant of the outcome of the award before mid- September 2013. Applicants must also fill application forms for higher degrees.
Details on how and when to apply could be obtained from SUA web address http://www.suanet.ac.tz

Source:SUA website.

UBUNGE CHADEMA 2015,NAFASI KUTANGAZWA GAZETINI NA WATU KUOMBA KAMA AJIRA.

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mfumo mpya wa kuwapata wagombea nafasi ya ubunge kuanzia uchaguzi wa 2015. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alisema kuwa kuanzia uchanguzi ujao wa 2015, nafasi za wagombea ubunge majimbo yote nchini zitatangazwa kwenye magazeti.
Dk. Slaa alisema baada ya waombaji kujitokeza watafanyiwa usaili kwa kufanya mtihani utakaokuwa umeandaliwa kwa kuzingatia nafasi hizo.

“Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe amekwisha kusema kwamba kuanzia sasa hatupokei makapi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hili naliweka wazi kwamba uchaguzi ujao utakuwa na mfumo mpya na wenye mabadiliko makubwa, tunaamini utaleta uzalendo na kuondoa upuuzi unaojitokeza.

“Kwa wale walio na mipango ya kujitokeza dakika za mwisho kugombea nafasi za ubunge kupitia CHADEMA au nje ya chama, naomba wasahau hilo tunataka mtu anayetetea wananchi, mwenye uzalendo, hoja, ujasiri na mwenye kuitoa Tanzania hapa ilipo na kuisogeza mbele,”alisema.

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya alisema CHADEMA haitakubali kuona inakuwa sehemu ya watu walioshiriki kutengeneza katiba isiyo ya Watanzania wote.

“Sasa kwa kuwa Serikali imetoa majibu yake bungeni kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda tunasubiria mwenyekiti wetu Mbowe awasilishe ripoti kwenye kamati kuu ndipo tutakapoamua.

“Pia suala la mwakilishi wetu katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu litazungumzwa kwenye kamati kuu, chama kikijitoa hata kama akibaki hayo yatakuwa ni mawazo yake,”alisema.

Hata hivyo alisema kuwa amani ya imevurugwa na viongozi wa Serikili na vyama vya siasa kutokana na kutanguliza ushabiki wa siasa badala ya uzalendo na misingi ya taifa.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iramba Magharibi, Ntundu Emmanuel amehamia CHADEMA akidai kuchoshwa na matusi ya Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
 
Source:CHADEMA social media.

RAPA WA KIKE LAURYN HILL AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 3 KWA KUTOLIPA KODI.



Rapa mkongwe wa kike Duniani Lauryn Hill ahukumiwa kifungo cha miezi 3 kwa kile kinachodaiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha $1.8 millioni.

Na hii hapa chini ni wasifu wa msanii huyu.


Background information
Birth name Lauryn Noelle Hill
Also known as Ms. Hill, L. Boogie
Born May 26, 1975 (age 37)
Origin South Orange, New Jersey, United States
Genres R&B, hip hop, soul, reggae fusion
Occupations Singer-songwriter, record producer, rapper, actress
Instruments Vocals, guitar, piano
Years active 1987–present
Labels Columbia, Ruffhouse
Associated acts Fugees, Nas, D'Angelo, Mary J. Blige, Santana
Website www.lauryn-hill.com    

NASHERA HOTEL-KIWANJA CHA KISASA MOROGORO.

Nashera Hotel is a 4-star hotel features an outdoor pool, and is located just over 3km from the centre of Morogoro. It has panoramic views of the Uluguru Moutain and includes free Wi-Fi throughout the property.
All of the rooms at Nashera Hotel are air-conditioned and offer a balcony and a satellite TV. Each has an en suite with a bath and a shower.
Breakfast is served daily, which can also be taken in the room. The restaurant, Udzungwa, serves dishes ranging from American specialties to classic Swahili fare. A number of restaurants serving a range of local and international cuisine can also be found within 5 minutes’ drive of the property.
Guests can relax in the garden with a drink from the bar, or the Nashera’s staff can arrange a tour in the local region. Morogoro Airport is located 5km away.
 

Click Read more to continue.

JESHI LA POLISI LATAKIWA LIVUNJWE,LADAIWA KUTUMIWA VIBAYA NA CCM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetaka Jeshi la Polisi nchini livunjwe na ligeuzwe kitengo ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Msimamo huo umetolewa jana bungeni na baadhi ya wabunge wa chama hicho walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyowasilishwa na Waziri Emmanuel Nchimbi.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde, alisema Jeshi la Polisi limeoza, kwa sababu limeshindwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu, ikiwamo kuwakamata wahalifu mbalimbali wanaoshiriki kwenye matukio ya kihalifu.
“Napendekeza Jeshi la Polisi livunjwe na liingizwe ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liwe sehemu ya kitengo katika jeshi hilo.
“Naamini kwa kufanya hivyo tutaboresha utendaji wake, silaha kubwa iliyobaki kulinusuru taifa hili kwa sasa ni kusema ukweli, kwani bila kufanya hivyo miaka sita ijayo hali itakuwa mbaya,” alisema.
Bofya read more kuendelea.

Monday, May 6, 2013

RAIA 4 WA SAUDIA WAKAMATWA KUHUSIKA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA.

Polisi Mkoani Arusha inawashikilia watu 8 kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa jana siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.
Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne (4) wa Saudi Arabia, na wengine wanne (4) ni raia wa Tanzania.
Wakati mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akuzungumza akiwa hospitalini mjini Arusha amesema idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia mlipuko huo ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali.
Polisi mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza ni kilipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo.
Lakini Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la tukio mbali na majeruhi hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia sakafu na kuta za kanisa hilo hazikuchimbika sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad Mubali anaongezea kuwa watu wawili sana wamethibitishwa kufariki dunia katika mlipuko huo uliotokea majira ya saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa papa na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia .
Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo unapotokea walikuwa tayari katika hatua ya kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa kanisa ulikuwa ukiongozwa na balozi wa Papa Fransis.
Shambulizi la Arusha
Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali watu kati yao wamefariki huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru mjini Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo zimesitishwa huku watalaalamu wa milipuko na polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa zozote kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo ama kundi lolote linalodaiwa kuhusika na utegaji wa bomu hilo.
Hili ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japo kuwa mwaka huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia kanisani.
 
Chanzo:BBC

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...