Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Thursday, August 15, 2013

KAULI YA ZITTO KABWE JUU YA VIONGOZI KUWEKA WAZI MALI NA MADENI YAO.

Mbunge wa Kigoma kaskazini mh.Zitto Kabwe katoa maoni yake juu ya uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kama ifuatavyo:-
" 'Uwazi wa mali na madeni ya viongozi ni moja ya hatua muhimu kupambana na ufisadi' nimemwambia leo Mama Salome Kaganda wa Sekretariat ya Maadili ya Umma.
Wanasiasa tunajaza fomu kutangaza mali na madeni yetu. Fomu hizo haziwekwi wazi kwa wananchi. Utajuaje kama Kiongozi kasema uwongo? Utawezaje kupambana na uzushi na uwongo dhidi ya viongozi waadilifu lakini wanachafuliwa na wapinzani wake kisiasa? Suluhisho moja tu. UWAZI. Daftari la mali na madeni ya viongozi liwe wazi kwa wananchi. Fomu za mali na madeni ya viongozi wa umma ziwe online. Kiongozi asiyetaka mali na madeni yake kujulikana, akauze vitumbua aache uongozi, hakuna atakayemgusa!
"
Source:Zitto Social media.

KAULI YA NAPE NAUYE WAKATI CCM TAIFA IKIWAREJESHA KAZINI MADIWANI 8 WALIOFUKUZWA BUKOBA.

Wednesday, August 14, 2013

CCM YAWASIMAMISHA UONGOZI NA KUWAFUKUZA MADIWANI WAKE WANANE BUKOBA.


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatolea uvivu kwa kuwavua uanachama na uongozi madiwani wake wanane katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Imeelezwa kwamba hatua hiyo imechukuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kagera kutokana na kudaiwa kupuuza maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na  Katibu wa CCM wa mkoa huo Avelin Mushi, imesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.

Mushi amewataja madiwani hao nane kuwa  Yusuph Ngaiza (Kata Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera, Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu Meya Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.

Mushi amesema kuwa  kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambapo Rais Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kutoendelea na mgogoro huo.

Pia, amesema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.
Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CHADEMA(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)

CHADEMA WAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KUJADILI NA KUTUMA MAONI YA RASIMU, MABARAZA YA CHADEMA KATIBA MPYA

CHADEMA jana kimeanza rasmi kuendesha mabaraza ya Katiba na taarifa hii ndiyo iliyotolewa:-
 
"Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na 
    timu mbili za viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. 
    Willibroad Slaa. 
    
    Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa umma, 
    kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).

2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba 
    Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.


4. Mitandao ya kijamii, mf; Jamii Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, 
    wanabidii n.k, utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni 
     pamoja na kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni 
     yao kwa njia hii.




Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press) Officer
0752 691569/ 0688 595831"
 
Source:CHADEMA Social Media.

Tuesday, August 13, 2013

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NA MKURUGENZI WA TAASISI YA NDI YA MAREKANI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwelewesha jambo Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, alipomkaribisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque, alipomkaribisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 12, 2013.  Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.

Monday, August 12, 2013

Dk. Slaa kuunguruma Tanga Alhamisi.

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, Alhamisi wiki hii anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kuzindua mabaraza ya Katiba ya chama hicho pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ilieleza alisema Dk. Slaa atawasili mkoani hapa Agosti 15 na kufanya mikutano ya hadhara na siku inayofuata atakuwa na kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bahweje alisema Dk. Slaa akitumia helikopta atafanya mikutano ya hadhara katika wilaya za Lushoto, Handeni, Korogwe, Muheza na Tanga Jiji.
“Katibu mkuu atawasili Lushoto na kufanya mkutano wa hadhara uwanja wa RRM saa mbili asubuhi, Handeni mjini saa 5.30 asubuhi, Korogwe Mazoezi saa 7.30 nchana, Muheza saa 9.30 uwanja wa CHADEMA Square na mkutano wa mwisho Tanga Jiji saa 11. 40 jioni,” alisema Bahweje.
Katibu huyo alitoa wito kwa wananchi kuhudhuria mikutano hiyo katika maeneo hayo na kumsikiliza ili kupata misingi halisi ya mikutano hiyo.
Sambamba na hayo, alieleza chama hicho ngazi ya mkoa kinaendelea na mikutano ya hadhara na ya ndani kwa kuanzia wilaya ya Korogwe kwa lengo la kuelezea mkakati wa CHADEMA.
Alisema mikutano hiyo inafanyika katika vijiji vya Masange, Mngwasa na Lutindi vya kata ya Lutindi na kuendelea katika kata ya Bungu, jimbo la Korogwe vijijini.
Source:CHADEMA Social Media.

Tuesday, July 30, 2013

CHADEMA YAVUNA WANACHAMA 300 TANGA.

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Tanga kimepata wanachama wapya zaidi ya 300.
Wanachama hao wamepatikana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika wilaya za Handeni, Muheza na Korogwe uliohutubiwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje.
Wanachama 220 wamejiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kwengoma, Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni na wanachama 71 ni kutoka Kibanda, wilayani Muheza.
Wanachama wengine 21 akiwamo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Turiani, Bakari Kimea walijivua uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kwashemshi, Wilaya ya Korogwe.
Wakizungumza katika mikutano hiyo baada ya kujiunga na CHADEMA, walisema wameamua kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa kimeshindwa kuondoa kero zinazowakabili kwa miaka mingi.
Miongoni mwa kero hizo kwa mujibu wa wananchi hao ni unyanyaswaji unaofanywa na viongozi wa serikali za vijiji, kunyang’anywa ardhi, kero ya maji na kuvunjiwa mikataba na muwekezaji.
Chanzo: CHADEMA Social media.

Friday, July 26, 2013

CHADEMA YAIKOROGA POLISI.

UAMUZI wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kuwasilisha ushahidi wa mauji ya mlipuko wa bomu uliotokea jijini Arusha, umeliweka njia panda Jeshi la Polisi na hivyo kushindwa kuchukua hatua.
Licha ya jeshi hilo kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na kumtaka awasilishe ushahidi huo, kiongozi huyo amekataa agizo hilo akisema kuwa wamekubaliana kuutoa ushahidi huo kwa tume huru ya majaji endapo Rais Jakaya Kikwete ataiunda kama walivyomuomba.
Chanzo chetu ndani ya jeshi hilo, kimedokeza kuwa msimamo huo wa CHADEMA umeliweka njia panda na hivyo kushindwa kuchukua hatua za kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafungulia mashtaka kutokana na mkanganyiko wa taarifa zinazotolewa.
Jeshi hilo linadaiwa kuwa awali lilitaka kujiegemeza kwenye kauli za kisiasa za baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ili kuonyesha kuwa CHADEMA ilisababisha mlipuko huo yenyewe kwa ajili ya kuwahadaa wafuasi na kujitafutia umaarufu.
Hata hivyo, mbinu hiyo ya kutaka kuwasakama baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA inadaiwa kufifishwa na tamko la Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba chama kina ushahidi unaoonyesha kuwa tukio hilo lilifanywa na polisi.
“Hapa kuna mkanganyiko hasa baada ya Mbowe kudai wanao ushahidi wa video ya tukio hilo. Wakubwa wetu wamegawanyika na kujikuta wakitoa kauli za kukinzana maana wanahofia wakiwafungulia kesi watu wengine mashtaka halafu CHADEMA ikaonyesha ushahidi tofauti itakuwa ni aibu,” kilisema chanzo chetu.

Monday, July 22, 2013

MNYIKA AKOSWA NA BOMU, LILIRUSHWA NA POLISI ALIPOSIMAMA.

VITUKO na matukio ya hatari kwenye mikutano ya CHADEMA vimeendelea kushika kasi.
Jana Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alinusurika kupigwa na bomu la machozi lililorushwa na polisi waliokuwa wakizuia kufanyika mkutano ulioitishwa na chama hicho.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Mabibo kwenye viwanja vya Sahara ambapo bomu hilo lilimpata mtu aliyekuwa karibu na Mnyika anayeitwa Thomas Jerome, aliyejeruhiwa sehemu ya paja.
Baada ya kurushwa kwa bomu hilo, polisi walitaka kumchukua majeruhi huyo ili wamweke kwenye gari lao apelekwe hospitalini, lakini Mnyika aliwaelekeza wafuasi wa CHADEMA kumchukua kwa madai kitendo kilichofanywa na askari hao kililenga kuficha ushahidi wa jambo hilo.
Polisi waliokuwemo eneo la tukio waliamua kukubaliana na matakwa ya wafuasi wa CHADEMA waliomchukua Jerome na kumpeleka hospitali ambako hali yake inadaiwa inaendelea vizuri.
Akielezea hali ilivyokuwa akiwa katika mkutano mwingine uliofanyika Ubungo, Mnyika alisema polisi walifika katika viwanja vya Sahara wakiwa na magari matatu kwa lengo la kutawanya wafuasi wa CHADEMA wasifanye mkutano wakidai haukuwa na baraka za jeshi hilo.
Mnyika alisema polisi hao walisema sababu ya kuuzuia mkutano huo ni uwepo wa ziara ya Makamu wa Rais katika Wilaya ya Kinondoni, hivyo walikuwa wameelekeza nguvu zao katika ziara hiyo, kwamba hawakuwa na uwezo wa kuulinda mkutano wa CHADEMA.
“Nikiwa nimejiandaa kupanda jukwaani ndiyo polisi walikuja kusema tuache tusifanye mkutano, nilisogea karibu na gari kumlalamikia ofisa wa polisi kwani kitendo cha kuahirisha mkutano kwa barua waliyoileta saa sita mchana siku ya mkutano wakati sisi tuliwapa taarifa siku nne zilizopita ilikuwa sio haki.
“Nilimwambia ofisa huyo wa polisi kuwa nilikuwa najadiliana kwa simu na viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema kumlaumu kutumika vibaya kwa Jeshi la Polisi.
“Nilipokuwa bado najibizana naye bila fujo zozote, bomu lilirushwa kutoka ndani ya gari ya polisi na kupita karibu na mimi likamjeruhi mtu aliyekuwa karibu yangu, ki ukweli nimeshangazwa sana na matumizi mabaya ya silaha za moto,” alisema.
Aliongeza kuwa katika purukushani zilizotokea baada ya bomu kupigwa, alipoteza nyaraka mbalimbali alizokuwa amebeba kama ushahidi kuwaonyesha wafuasi wa chama hicho hasa jinsi serikali ya CCM na wabunge wake walivyopitisha kodi ya huduma za simu, na kodi ya laini za simu.
Slaa anena
Aidha katika mkutano huo ambao awali ulitangazwa kuwa ungehutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, haukuweza kuhutubiwa naye kwa kile alichosema kuwa watu wake wa usalama walimwambia mapema hali si salama kwenye mkutano huo.
“Nilipata taarifa kutoka vyanzo vyangu kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuleta fujo, hivyo nikaona kwa kuwa wanatuwinda nisingeenda kuhutubia, pengine bomu lililomkosa Mnyika lilikusudiwa kwangu au kwa mwingine,” alisema Dk. Slaa alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu baada ya kutoonekana mkutanoni.

Friday, July 19, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KAULI YA CCM JUU YA KODI YA KUMILIKI KADI YA SIMU YA MKONONI/KIGANJANI.

Taarifa iliyotolewa na CCM na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari tarehe 18 Julai 2013 ya kuitaka Serikali inayoongozwa na CCM kuangalia njia nyingine mbadala ya kukusanya kodi na kuachana na hatua yake ya kukusanya kodi ya umiliki wa kadi ya sh. 1000 kila mwezi imethibitisha maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba ‘chama lege lege huzaa serikali legelege’.

Aidha, taarifa hiyo ni mkakati legelege wa kujinasua katika malalamiko, kukusanywa kwa saini, kuandaliwa kwa miswada ya sheria, migomo ya kuzima simu kwa muda maalum na maandamano dhidi ya Serikali ya CCM kutokana na chama hicho kushindwa kuwa na sera sahihi na mikakati makini. 

Taarifa hiyo haiwezi kurudisha nyuma hatua ya wananchi kukikataa chama hicho na kuunga mkono mabadiliko ya kweli kupitia CHADEMA kwa kuzingatia kuwa CCM imeshindwa kuhakikisha kwamba Ilani zake za uchaguzi ya mwaka 2005 na 2010 zinatekelezwa. Ikumbukwe kwamba kupitia ilani hizo CCM iliahidi maisha bora kwa kila mtanzania na badala yake maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu kutokana na ongezeko la bei na gharama za maisha.

TAMKO LA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB) KUHUSU UDHAIFU WA SERIKALI KATIKA KUKOMESHA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI.

 
Ndugu wanahabari, kwanza kabisa napenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wangu, ili niweze kuzungumza na watanzania kupitia kwenu kuhusu hatari kubwa inayolikumba taifa ya madawa ya kulevya.

Biashara haramu ya dawa za kulevya imekua kwa kasi sana hapa nchini miaka ya hivi karibuni licha ya kuwa na vyombo lukuki vya ulinzi na usalama na licha ya kuwa na Tume maalumu ya kudhibiti madawa ya kulevya chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera Uratibu na Bunge Mhe. Wiliam Lukuvi tarehe 26 Juni, 2013 siku ya maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya huko Dodoma ni kwamba katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012 watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini. Aidha, watanzania wapatao 240 walikamatwa na madawa ya kulevya katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika ya kusini na hivyo kutia doa taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa. Kutokana na kukithiri kwa biashara hii haramu, Serikali kupitia maadhimisho hayo ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani ilitangaza kuwa biashara ya dawa za kulevya kuwa ni janga la taifa. 

Wednesday, July 17, 2013

KAULI YA ZITTO KABWE ASUBUHI YA LEO.

CHADEMA na NCCR-M tuna jumla ya madiwani 13 katika halmashauri ya Wilaya Uvinza. Ni mamlaka mpya inaanza tarehe 20 Julai, 2013. CCM ina madiwani 8 tu, hivyo a clear majority kwa upinzani. CHADEMA ina madiwani 7, NCCR-M 5 + Mbunge 1.
Leo sekretariat za vyama vyetu zinakaa kuamua chama gani kati ya CHADEMA na NCCR-M kitoe Mwenyekiti, makamu na wenyeviti wa Kamati. Nimewaambia madiwani wetu kwamba Ni lazima kuhakikisha Halmashauri hii inaongozwa na Upinzani. Tukiendekeza tamaa zetu za kisiasa CCM watapita katikati yetu. CCM wakichukua Halmashauri ya Uvinza yenye madiwani wengi wa upinzani itakuwa Ni usaliti mkubwa Kwa wananchi. Nimewasihi viongozi wa vyama vyote 2 kuwa na hekima na kuzingatia matakwa ya wananchi waliotoa ridhaa mwaka 2010 na hivyo CHADEMA na NCCR-M kuongoza Halmashauri ya Wilaya Uvinza. Ni jaribio la demokrasia, Hekima na Maamuzi.
Source: Zitto Kabwe Social media.

Monday, July 15, 2013

TAARIFA NA MATOKEO KAMILI UCHAGUZI WA ARUSHA HII HAPA.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), `kimefunika' katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini uliofanyika jana.
Matokeo katika vituo mbalimbali vya kata hizo nne ambayo kwa mujibu wa   Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), yalionyesha Chadema ikiongoza kwa idadi kubwa ya kura zilizopigwa kwenye vituo 136 vya kupigia kura huku kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Matokeo kamili katika vituo hivyo yalikuwa kama ifuatavyo:-

KATA YA KALOLENI:

Matokeo ya jumla Chadema 1,470, CCM 530, CUF 275 na Demokrasia Makini 2,  Kwa matokeo hayo Emmanuel Kessy wa Chadema alitangazwa mshindi.
Kituo kidogo A, Chadema kilikuwa kimenyakua kura 51, CCM 25 na CUF 11.
Kituo B1, Chadema 68, CCM 19 na CUF 17 huku katika kituo A4, Chadema kilipata kura 67, CCM 20 na CUF 9, Kituo A3 Chadema kura 57, CCM 25 na CUF 7.
Katika kituo cha B4, Chadema kura 54, CCM 30 na CUF 9, B3 Chadema 54, CCM 15 na CUF 9, wakati B2 Chadema kilipata kura 73, CCM 9 na CUF 4 na kituo A2, Chadema 69, CCM 21 na CUF 8.
Kituo cha A1, Chadema kura 60, CCM 15 na CUF 11 na B6 Chadema kura 41, CCM 21 na CUF kura 9.

Katika kituo cha B5, Chadema kilipata kura 50, CCM 22 na CUF 10.
Katika kituo cha AICC Nursery School, kituo kidogo cha A2 Chadema kura 58, CCM 18 na CUF 17, A4 Chadema kura 62, CCM 22 na CUF 6, A3 Chadema 44, CCM 22 na CUF 5, E2 Chadema 58, CCM 22 na CUF 4, E3 Chadema 53, CCM 20 na CUF 5.

Aidha, katika kituo cha E4 Chadema 40, CCM 20 na CUF 5, B1 Chadema 57, CCM 18 na CUF 9, A1 Chadema 60, CCM 24 na CUF 5.

Kituo cha Shule ya Sekondari Kaloleli, A1,Chadema 52, CCM 17, CUF 15 huku katika kituo cha A2, Chadema kura 97, CCM  23,  CUF 19 na kituo A3, Chadema 46, CCM 20 na CUF 20.

Kituo cha A4 Chadema 46, CCM, 16, CUF 16, kituo B1 Chadema 56, CCM 10, CUF 16 na kituo B2 Chadema 42, CCM 23 na CUF 15.
Kituo B3, Chadema 53, CCM 17  na CUF 11, kituo B4 Chadema 38 CCM 16 na CUF 13

KATA YA ELERAI

Katika Kituo cha Shule ya  Sekondari Kata ya Elerai, Ofisi ya Katibu Tarafa, pia Chadema kimeendelea kuongoza katika matokeo ya awali.
Matokeo ya jumla Chadema kura 2,047, CCM 1,471, CUF 302, CCK 3, na TLP 1. Mshindi ni Mhandisi Jeremiah Mpinga wa Chadema.

Kituo A1, Chadema kura 37, CCM 17, CUF 3, TLP na CCK 0. Kituo A2, Chadema kilipata kura 28, CCM 13, CUF 2, CCK na TLP 0.

Kituo A3, Chadema kura 31, CCM 19, CUF 2, CCK na TLP 0 huku katika kituo A4 , Chadema 21, CCM 12, CUF 6 , TLP na CCK 0.

Vituo vingine katika kata hiyo ni pamoja na B1 ambacho Chadema waliongoza kwa kura 42, CCM 15, CCK na TLP 0 huku katika kituo C1, Chadema 42, CCM 15, CCK na TLP 0.
Kwa upande wa kituo cha C2, CCK 0, CCM 12, Chadema 35, CUF 3 na TLP 0, Kituo kingine cha Katibu Tarafa Ofisi, CCM kilipata kura 26, Chadema 25 na CUF huku cha B1 Chadema wakijipatia kura 43, CCM 23, CUF 5.

 Kituo B2, Chadema 34, CCM 24, CUF na TLP 0, kituo B3  CCM kura 26, Chadema 32, CUF 3, kituo cha Shule ya Msingi Burka B2, CCM ilinyakua kura 31, Chadema 30, CUF 2 na kituo B3, CCM ikipata kura 41, Chadema 43, CUF 5 wakati CCK na TLP wakiambulia patupu.

Aidha katika kituo hicho cha Shule ya Msingi Burka,B4 CCM ilipata 32, Chadema 28, CUF 3, TLP na CCK 0, vituo vya C1, CCM kura 26, Chadema 43, CUF 5 na kile cha C2, CCK 0, CCM 31, Chadema 43, CUF 7 na TLP 0.

KATA YA KIMANDOLU

Katika Kata ya Kimandolu kwenye kituo Shule ya Msingi Suye, CCM na Chadema ndivyo pekee vilisimamisha wagombea.

Katika kituo cha A1, CCM ilipata kura 15, Chadema 47, A2  CCM 24, Chadema 39, kituo A3 CCM 14, Chadema 35,  kituo B1 CCM 25, Chadema 56,  kituo B2 CCM 25, Chadema 48, kituo C2 CCM 30, Chadema 39 na kituo C1 CCM 11, Chadema 48.

Kituo cha ofisi ya Kata ya  Kimandolu, kituo A1 Chadema ilipata kura 97, CCM 22,  kituo A2  Chadema 88, CCM 29, kituo A3 Chadema 81, CCM 31, kituo A5 Chadema 90, CCM 41, kituo A6 Chadema 87, CCM 28, kituo A7 Chadema 70, CCM 35,  kituo B1 Chadema 84, CCM 27 na kituo B2 Chadema 82, CCM 27.

Kituo B3 Chadema 78, CCM 37, kituo B4 Chadema 87, CCM 36, kituo cha B5 Chadema 69, CCM 23, kituo C1 Chadema 97, CCM 28, kituo C2 Chadema 103,CCM 21, kituo C3 Chadema 79, CCM 32, kituo C4 Chadema 84 CCM 42 na kituo C5 Chadema 87 CCM 41.

Kituo cha Shule ya Msingi Kimandolu kwenye kituo A1 CCM ilipata kura 34, Chadema 64, kituo B2 CCM 26, Chadema 66, kituo B4 CCM 37, Chadema 74, kituo A5 CCM 48, Chadema 58, kituo A3 CCM 48, Chadema 53, kituo B5 CCM 24, Chadema 65, kituo C1 CCM 27, Chadema 74, kituo C3 CCM 36, Chadema 64, kituo C5 CCM 31, Chadema 78, kituo A2 CCM 27, Chadema 87, kituo A4 CCM 33, Chadema 57, kituo B2 CCM 30, Chadema 77 na kituo C2 CCM 30,Chadema 65.

KATA YA THEMI
Katika kata hiyo iliyokuwa na vituo 12, Chadema ilinyakua jumla ya kura 674, CCM 326 na CUF 307. Waliojiandikisha walikuwa 6,387, waliopiga kura 1,319, kura halali 1,307 ambapo zilizoharibika 12, kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo, Eveka Mboya ambaye pia alimtangaza mshindi kuwa ni Kinabo Edmund wa Chadema.

Matokeo kwa baadhi ya vituo yalionyesha kuwa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa  Kata ya Themi, CCM  9, Chadema 36, CUF 0, kituo A2 CCM kura 13, CUF 3 na Chadema 23, kituo cha A3 , Chadema 33, CCM 16, CUF 2 na katika kituo A1, CCM ikijipatia kura  44, CUF 1, Chadema 53.
Katika kituo A2, CCM 29, Chadema 57 na CUF 4 huku kile cha A3 CCM ikijipatia kura 23, Chadema 44 na CUF kikiambulia 0.

Kata ya Themi ilikuwa na vituo 12 ambapo hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya vituo sita yalikuwa yamepatikana huku matokeo ya vituo vingine yakiendelea kuhesabiwa.


CHADEMA YASHINDA VITI VYOTE 4 ARUSHA.

LICHA ya hujuma ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ufanisi mdogo wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata nne za jijini Arusha.
Katika Kata ya Elerai, mgombea wa CHADEMA Injinia Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 1,715, dhidi ya 1,239.
Kata hiyo ilikuwa na wapiga kura 23,797 waliojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi hawakujitokeza.

Wednesday, July 10, 2013

CHADEMA YAJIPANGA, YAANDAA VIJANA KUJILINDA NCHI NZIMA.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetishia kuuanika hadharani ushahidi unaothibitisha polisi kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani mwezi uliopita na kuua watu wanne mkoani Arusha, huku kikiamua kuanzisha kambi za mafunzo kwa vijana nchi nzima kwa ajili ya kuwalinda viongozi wao.
CHADEMA imesema itauanika hadharani ushahidi huo iwapo Rais Jakaya Kikwete atakataa kuunda tume ya kimahakama itakayokuwa na jukumu la kusikiliza shauri hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kikao cha dharura cha Kamati Kuu, kilichoketi kwa siku mbili jijini humo kimejadili masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwemo siasa, rasimu ya katiba mpya na uanzishaji wa kambi za mafunzo ya vijana.
Alisema CHADEMA hawapo tayari kuwasilisha ushahidi wao kwa polisi ambao ndio watuhumiwa wakuu, bali wanataka Rais Kikwete aunde tume huru ya kimahakama.
Alisema isipoundwa tume hiyo ya kimahakama, watauweka wazi ushahidi huo kwa wananchi wakati ukifika.
Mbowe alisema watausambaza ushahidi huo kwa vyama, mashirika ya kiraia ya haki za binadamu ndani na nje ya nchi pamoja na ofisi za kibalozi za mataifa rafiki na Tanzania pamoja na jumuiya ya kimataifa.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwataka waishinikize serikali kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo na mengine yanayofanana na hayo juu ya mauaji ya kisiasa.
Aliongeza kuwa serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Sera (Uratibu na Bunge) William Lukuvi imetoa kauli isiyostahili ndani ya Bunge kuwa CHADEMA wamejilipua kwa ajili ya kutafuta umaarufu.
“Tunalaani kauli ya serikali kupitia kwa Lukuvi, ni ya kitoto, kijinga na ya kiuendawazimu. Sisi hatuwezi kutafuta umaarufu kupitia damu za Watanzania.
“Kama umaarufu unatufikia kwa kazi tuzifanyazo kwa ajili ya wananchi, serikali inatafuta pa kushikia baada ya polisi kuhusishwa,” alisema Mbowe.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona Lukuvi akiwakilisha serikali na kujinadi kuwa CHADEMA wanahusika na mlipuko pasipo kuuweka hadharani kwa lengo la kukomesha hatua hiyo.



Thursday, June 27, 2013

HII NDO KAULI YA KAMANDA WILFRED LWAKATARE

Na Wilfred Lwakatare,
Sina budi kumshukuru sana mwenyenzi Mungu kwa kunitendea mema na zaidi ya yote kunipa uhai na afya hadi sasa. Wanasema “shukuruni katika yote” na mimi nalazimika kushukuru kwa yale yote niliyofunuliwa na kuwa sehemu ya ushuhuda wangu katika maisha niliyobakiza hapa duniani.

Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.

Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;

“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”

Ni kweli kabisa na wala si hadithi kuwa ‘jela ni MBAYA, jela ni MATESO!’ Lakini zaidi ya hilo, kwangu mimi nimeyaona pia maisha ya gerezani ni mahala pa mafunzo ya kuijua jamii, kuyajua maisha, kuyaelewa mambo, kuifahamu nchi n.k.

Nimekubaliana mia kwa mia na maneno ya mwenyekiti wetu wa CHADEMA-Taifa Freeman Mbowe(MB) aliponitembelea gerezani Segerea na kuniambia; “hupaswi kulia na kujuta sana;now you are going to be a PRISON GRADUATE, uhitimu ambao kila mwanasiasa na mpigania haki mahiri duniani ameupitia.” Kipindi cha siku 92 nilichokaa ndani nikianzia polisi kituo cha kati, gereza la Keko na kisha kumalizia Segerea kimenipa uzoefu na ufahamu usio wa kawaida.

Ipo tofauti kubwa baina ya idara za polisi na magereza,jambo ambalo lilikuwa nje ya ufahamu wangu kabla.Nina uhakika magereza wakipewa kazi ya kuwasaka walipua mabomu ,watesaji,wapiga risasi mapadri watawakamata. Nilipata bahati ya kuitwa na kufanya mazungumzo na wakuu wa magereza ya Keko na Segerea .

Lakini pia, nilitembelewa na viongozi wakuu wengi wa jeshi la magereza nchini akiwemo kamishena mkuu Minja.Wakuu hawa wana weledi mkubwa wa kumpa mtu somo la ‘ushauri nasaha’(counselling). Wanakufutia fikra zote za uraiani (nyumbani,mitaani na ofisini) na kukurejesha mahala pa maisha yako mapya ya gerezani na kukujuza taratibu na kanuni unazopaswa kuzifuata na kuzitii.
Madaktari na manesi waliweza kuangalia kwa karibu sana afya yangu kiasi cha kulidhibiti kwa kiasi kikubwa tatizo langu la sukari ambalo limekuwa likinisumbua kwa miaka 14 sasa.



2: KESI YA UGAIDI.

HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012-2013.

Wednesday, June 26, 2013

MAELEZO YA WAKILI WA SUGU, TUNDU LISSU KUHUSU KUITWA POLISI DODOMA MTEJA WAKE.



Kuhusu Joseph Mbilinyi 'Sugu', Mbunge wa Mbeya Mjini. Ni kweli alikuwa polisi Dodoma, alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo: 

1. Wakili wake, Tundu Lissu, amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini, maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bunge, wakati bunge likiendelea, kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu zinazotakiwa.

2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa hivyo. 

3. Wakili wake (Tundu Lissu)kawauliza, nani mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda mwenyewe? Majibu yalikuwa ya kigugumizi" 

Waliondoka polisi kwa makubaliano ya kurudi leo asubuhi.


BY: Tumaini Makene

Tuesday, June 25, 2013

UCHAGUZI ARUSHA WAAHIRISHWA HADI JULAI 14.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesogeza mbele chaguzi za madiwani katika kata 4 zilizoathiriwa na bomu Arusha hadi Julai 14 kwa sababu sa kiusalam.

Monday, June 24, 2013

MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI MFUMO WA SERIKALI TATU.


MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.



LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...