Showing posts with label MICHEZO NA BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO NA BURUDANI. Show all posts

Monday, February 10, 2014

Baada ya Yanga kushinda 7-0 na Azam FC yaanza vyema CAF, yairarua Ferroviario 1-0

IKICHEZA mchezo wa kimataifa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza katika historia yake AzamFC jana imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi yaAwali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jana jioni.

Tuesday, January 28, 2014

MJASIRIAMALI WA SABUNI ZA MAJI ATIMKA NA MILIONI 30 ZA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusiana napromosheni hiyo ilivyobadilisha maisha ya wateja wao na watanzania kwa ujumla,mara baada ya kumtangaza mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya"promosheni ya Timka na Bodaboda" Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.

Tuesday, January 14, 2014

Ronaldo Mchezaji bora wa dunia 2013.

Christian Ronaldo
Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo jana usiku alinyakua tuzo ya mchezajii bora wa soka wa fifa wa mwaka 2013 na kuwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa Bayern Munich.
Ronaldo ambaye alinyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara kwanza mwaka 2008 alitangazwa kunyakua tuzo mwaka 2013 baada ya kupigiwa kura na makocha, manahodha na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa matokeo Ronaldo alipata kura 1365 akimshinda Messi aliyepata kura 1,205 na Ribery akiambulia kura 1,127.
Kwa upande wa wanawake golikipa wa Ujerumani Nadine Angerer alinyakuwa tuzo ya fifa ya mchezaji bora wa soka kwa upande wanawake huku aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes akinyakua tuzo ya kuwa kocha bora wa dunia.

Wednesday, October 30, 2013

NANI ATAKUWA MWANASOKA BORA NA KOCHA BORA WA FIFA 2013 KATI YA HAWA WAFUATAO?

Wachezaji 23 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA ni:-
Gareth Bale (Wales), Edinson Cavani (Uruguay), Radamel Falcao (Colombia), Eden Hazard (Belgium), Zlatan Ibrahimović (Sweden), Andrés Iniesta (Spain), Philipp Lahm (Germany), Robert Lewandowski (Poland), Lionel Messi (Argentina), Thomas Müller (Germany), Manuel Neuer (Germany), Neymar (Brazil), Mesut Özil (Germany), Andrea Pirlo (Italy), Franck Ribéry (France), Arjen Robben (Netherlands), Cristiano Ronaldo (Portugal), Bastian Schweinsteiger (Germany), Luis Suárez (Uruguay), Thiago Silva (Brazil), Yaya Touré (Côte d’Ivoire), Robin Van Persie (Netherlands), Xavi (Spain).

Makocha wanaowania taji la Kocha bora wa FIFA 2013 ni :- 
Carlo Ancelotti (Italy/Paris Saint-Germain FC/Real Madrid CF), Rafael Benítez (Spain/Chelsea FC/SSC Napoli), Antonio Conte (Italy/Juventus), Vicente Del Bosque (Spain/Spain national team), Sir Alex Ferguson (Scotland/Manchester United FC former coach), Jupp Heynckes (Germany/FC Bayern München former coach), Jürgen Klopp (Germany/Borussia Dortmund), José Mourinho (Portugal/Real Madrid CF/Chelsea FC), Luiz Felipe Scolari (Brazil/Brazil national team), Arsène Wenger (France/Arsenal FC).

Monday, October 28, 2013

JAMALI MALINZI BOSS TFF, AMBWAGA ATHUMAN NYAMLANI.MAKAMU WAKE WALACE KARIA.

Jamali Malinzi - Rais mpya wa TFF
JAMALI Malinzi amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa TFF baada ya kumpiku mpinzani wake Athuman Nyamlani katika uchaguzi mkuu uliofanyika usiku wa leo na kumalizika usiku huu. Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es Salaam.

Monday, October 21, 2013

SIMBA TIMU BORA KATIKA MECHI YAKE NA MTANI WA JADI YANGA.

Simba ikiwa chini ya kocha wake mkuu King Kibandeni imeonekana kuwa timu bora baada ya kuweza kusawazisha goli 3 alizokuwa ameshafungwa na mpinzani wake Yanga zilizofungwa katika kipindi cha kwanza.
Young Africans ilitoka sare ya mabao 3-3 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jana katika dimba la uwanja wa Taifa ambapo mchezo huo umeshuhudia mabao yote sita yakifungwa katika upande wa kusini mwa uwanja.
Baada ya kosa kosa ya Hamis Kiiza dakika ya tisa ya mchezo, Mrisho Ngassa aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 14 ya mchezo akimaliza pasi ya Kiiza aliyewatoka walinzi wa Simba SC na Ngassa kuukwamisha mpira wavuni.
Didier Kavumbagu alikosa bao la wazi kufuatia mpira aliopiga kutoka seintimeta chache langoni kabla ya tik tak ilyopigwa na Ngassa kupaa pia juu ya lango la Simba SC liliokuwa chini ya Abeid Dhaira
Hamsi Kiiza aliipatia Young Africans bao la pili dakika ya 35 ya mchezo, akimalizia pasi ya Mrisho Ngasa aliyemtoka mlinzi wa Simba SC Nassoro Maoud Chollo na mpira huo kumkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni.
Dakika ya 45 ya mchezo, Hamis Kiiza tena aliipatia Young Africans bao la tatu baada ya pira uliorushwa na Mbuyu Twite kuguswa na kichwa cha Didier Kavumbagu na kumkuta Kiiza ambaye alifanya kazi yake ya kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba SC 0 -3 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko, ambapo mabadiliko hayo yaliwaongezea uhai katika dakika ya 55 uzembe wa Nadir Haroub 'Cannavaro' ulimpelekea mshambuliaji wa Betram Mombeki kuipatia timu yake bao la kwanza.

Friday, October 18, 2013

VIWANGO VYA SOKA DUNIANI, TANZANIA YASHUKA NAFASI 2 NA KUWA YA 129.

 
TeamPts+/-   Pos
1 Spain15130Equal
2 Germany13111Up
3 Argentina1266-1Down
4 Colombia11781Up
5 Belgium11751Up
6 Uruguay11641Up
7 Switzerland11387Up
8 Netherlands11361Up
8 Italy1136-4Down
10 England10807Up
11 Brazil1078-3Down
12 Chile10514Up
13 USA10400Equal
14 Portugal1036-3Down
15 Greece983-3Down
16 Bosnia-Herzegovina9252Up
17 Côte d'Ivoire9172Up
18 Croatia901-8Down
19 Russia874-4Down
20 Ukraine8716Up
21 France8704Up
22 Ecuador862-2Down
23 Ghana8601Up
24 Mexico854-3Down
25 Sweden850-3Down
26 Denmark824-3Down
27 Czech Republic7835Up
28 Serbia77815Up
29 Romania7672Up
30 Slovenia752-1Down

Friday, October 11, 2013

Monday, September 30, 2013

YANGA - TAARIFA KUHUSU MRADI WA UWANJA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Francis Kifukwe (katikati) ambaye pia ni mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa uwanja eneo la jangwani akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, kushoto ni mzee Jabir Katundu (mwenyekiti wa baraza la wazee) na kulia Lawrence Mwalusako katibu mkuu wa Yanga SC
 
LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana

Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari. 

Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:
Kupata na kuwa na eneo la kutoshereza malengo ya mradi
Kupata ushauri mzuri, michoro mizuri na mkandarasi mzuri wa mradi
Kupata na kutenga fedha za kukamilisha usanifu na ujenzi wa mradi

Kwa upande wa BCEG wajibu wao ni kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha. BCEG wameandaa na kukabidhi michoro ya usanifu wa awali kukidhi matakwa ya YANGA. YANGA tunatakiwa kutoa maoni yetu na na kuingia RASMI mkataba wa ujenzi.

Kutokana na kukua kwa Jiji la Dar es Salaam, na katika hali ya kutaka klabu iwe na vitega uchumi klabu imeonelea ni vyema kama ingekuwa na uwanja wa mpira wa karne ya sasa na baadaye ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na mioundombinu ifuatayo:-

Friday, September 13, 2013

UNAIKUMBUKA ZE COMEDY YA MAPOUDA? HII HAPA Dawa ya Mapenzi

J.MARTINS KUWASHA MOTO USIKU WA LEO NDANI YA ELEMENTS LOUNGE.


J. MARTIN NA A.Y KUSHIRIKIANA NA VODACOM WALIPOTOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA DAR JANA.

Wanamuziki nguli Justice Martince (J.Martins) Kutoka nchini Nigeria na Ambwene Yessaya (AY) wakitoa misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Chamanzi Yatima Trust Fund kwa ushirikiano na kampuni ya Vodacom, wasanii hao walitoa wito kwa wasanii wengine kujitolea kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.

Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na watoto waishio katika mazingira magumu (Hawapo pichani) wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Chamanzi Yatima Trust Fund, walipo watembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao. Pamoja nao katika picha (waliokaa) ni wafanyakazi wa Vodacom, alie simama ni msanii Ambwene Yessaya. (AY).

Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom, (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule na Mlezi wa kituo hicho Bi. Winfrida Lubanza wakati wa utoaji wa misaada kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Chamanzi Yatima Trust Fund. Pamoja nao ni Meneja wa Chapa wa Vodacom Tanzania, Nicholous Machugu.


Msanii nguli wa muziki kutoka nchini Nigeria Justice Martins, (J.Martins) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utoaji wa misaada kwa watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Chamanzi Yatima Trust Fund.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...