Tuesday, January 28, 2014

MJASIRIAMALI WA SABUNI ZA MAJI ATIMKA NA MILIONI 30 ZA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusiana napromosheni hiyo ilivyobadilisha maisha ya wateja wao na watanzania kwa ujumla,mara baada ya kumtangaza mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya"promosheni ya Timka na Bodaboda" Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.

Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humudi Abdulhussein(kushoto)pamoja na Mkuu wa kitengo cha mtandao na huduma za ziada wa Vodacom Tanzania Bw.Charles Matondane(kulia)wakifurahia jambo wakati Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akiongea na mshindi wa droo kubwa ya mwezi ya promosheni ya Timka na Bodaboda Bi.Jovita Mosha(44)mkazi wa Ubungo external jijini Dar es Salaam aliyeibuka na kitita cha shilingi Milioni 30.Promosheni hiyo imebadilisha maisha ya watanzania zaidi ya 700.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...