Showing posts with label JAMII YETU. Show all posts
Showing posts with label JAMII YETU. Show all posts

Tuesday, June 9, 2015

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA YAENDESHA WARSHA KATIKA HOTEL YA GOLD CREST JIJINI MWANZA KWA AJILI KUHAMASISHA NA KUJENGA UWEZO WA KUJUMUISHA MASUALA YA VIJANA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA NA WILAYA

Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
Na: Thomas Nyindo
       Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.

Wednesday, May 27, 2015

Ukweli juu ya Umri wa Sitti Mtemvu bado mzigo mzito kwake.

Mtangazaji wa kipindi cha NIRVANA akiwa na mrembo Sitti Mtemvu.

Miss Tanzania ambaye alilivua taji mwaka jana 2014, Sitti Abas Mtemvu amekiri wazi kuwa maisha yake hayakuwa na amani tena toka skendo yake ya kudanganya umri katika mashindano ya Miss Tanzania, ambapo yeye aliweza kuibuka mshindi na kuvishwa taji hilo, Jana kupitia katika kipindi cha Fashion cha NIRVANA cha EATV,

Thursday, May 21, 2015

KINYEREZI I KUKAMILIKA MWAKA HUU.

Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima  (kulia)  akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani ni  Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert  Masatu na  Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano.

Na Oyuke Phostine Filemon 
Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.   

“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.

Monday, May 18, 2015

TAA yashauriwa kuimarisha kiushindani Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNIA.

Mshauri Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri (Kulia) maendeleo mradi huo.
Habari na Oyuke Phostine Filemon 

Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).

Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu za abiria kupandia na kushuka kwenye ndege, ofisi za uhamiaji na huduma zingine muhimu.

Thursday, May 14, 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Pichani meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.  

Thursday, March 5, 2015

TANAPA PARK FEES.

PRESS RELEASE: TANAPA PARK FEES TO REMAIN UNCHANGED FOR THE PERIOD 2015/2016

Tanzania National Parks would like to inform the general public that our Park Fees will remain unchanged for the period from July 2015 to June 2016.
This notice comes from the fact that our current fees structure available in the website and other printed materials shows that the current fees are applicable for the period from July 2013 to June 2015.

Issued by
Corporate Communications Manager
Tanzania National Parks
4th April, 2015
P.O.Box 3134
ARUSHA

Thursday, January 8, 2015

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE, HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA (PAC) YAKAGUA UKARABATI WA RELI YA KATI


Kamati ya Kudumu ya Bunge, Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) ilifanya ukaguzi wa ukarabati wa Reli ya Kati katika Wilaya ya Kilosa kwa kutumia Kiberenge 07/01/2015. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Zitto Zuberi Kabwe (MB) amesema "Zinahitajika tshs 500 bilioni kila mwaka kwa miaka 3 mfululizo kuweza kukarabati miundombuni ya Reli Tanzania ( Reli ya ratili 80 ). Ili kujenga Reli mpya kabisa ya ' standard gauge' zinahitajika $6.5bn .Kwa Nchi kama yetu, bila mtandao wa Reli madhubuti, Uchumi utakua kwa mwendo huu huu wa jongoo badala ya ukuaji wa kasi"

Friday, December 19, 2014

TUME YA MIPANGO WATEMBELEA BANDARI YA BUKOBA.


Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Bandari ya Bukoba, walipofika kujionea bandari hiyo kongwe iliyopo kwenye fukwe za Ziwa Victoria, mkoani Kagera. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wengine ni baadhi ya wajumbe wa msafara huo kutoka kushoto ni Bw. Omary Abdallah, Bibi Zena Hussein (Wapili kushoto) na Bw. Julius Edward (Kulia).

Wednesday, December 17, 2014

KAGERA KUJIVUNIA UWANJA WA NDEGE WA KISASA

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.
“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.

Friday, December 12, 2014

SUALA LA ESCROW, TANZANIA YABANWA ZAIDI.

MCC Statement on Board of Directors’ Discussion of Tanzania at the December 2014 Meeting
Washington, D.C.—The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) issued the following statement after its Board of Directors (Board) held its annual country selection meeting on December 10, 2014:
“MCC takes seriously all of its country partners’ commitments to combat corruption. At today’s meeting, MCC’s Board expressed continued concern over corruption in Tanzania, including the implications of the recent case involving Independent Power Tanzania Limited (IPTL). The Board noted that Tanzania has experienced a significant decline over the past seven years on the key indicator measuring efforts to control corruption. While the Board voted to allow Tanzania to continue working to develop a compact proposal—given its passage on MCC’s policy scorecards and its strong previous performance as an MCC partner—the Board stated its expectation that the Government of Tanzania must take firm, concrete steps to combat corruption before a compact is approved. Further, the Board voted to continue MCC’s engagement with Tanzania with the understanding that, in accordance with the Tanzanian State House December 9 statement, the Tanzanian government would act promptly and decisively on the late November parliamentary resolutions regarding IPTL. The Board also reaffirmed more broadly that Tanzania must undertake a series of previously agreed upon structural reforms to improve the efficiency, effectiveness and transparency of the energy sector, and more generally to deal with wider corruption.”
Source: http://www.mcc.gov

KATIBU MKUU KIONGOZI AMUAGA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI, BW. LUDOVICK UTOUH, NA KUMKARIBISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU MPYA WA HESABU ZA SERIKALI PROFESA MUSSA JUMA ASSAD, ALHAMIS, 11 DESEMBA 2014

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia), akimkabidhi zawadi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 11 Desemba 2014, amemuaga rasmi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovick Utouh, katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya Watendaji Wakuu na Waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuwa mahsusi pia kumkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.
Katika hotuba yake ya kumpongeza Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alielezea historia ya Utumishi uliotukuka ya Bw. Utouh ambayo imeleta sifa kubwa Ofisi hiyo ndani na nje ya nchi na katika medani za kimataifa. Kwa ujumla, hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi ilijikita kuelezea mchango binafsi wa Bwana Utouh kwa taifa ndani ya miaka zaidi ya arobaini (40) ya Utumishi wake Serikalini.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea mafanikio ya Serikali kwenye eneo la utawala bora, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za umma ambayo yamechangiwa na Bw. Utouh. Balozi Sefue aliwasihi watumishi wa umma kuiga weledi, uaminifu, msimamo, bidii na maarifa ambayo Bw. Utouh alivionyesha kwa vitendo katika utumishi wake.
Katibu Mkuu Kiongozi alitumia fursa hiyo pia, kumtakia kila la kheri, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Juma Assad, katika kufanikisha majukumu aliyopewa.
Bwana Utouh alistaafu rasmi nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, tarehe 19 Septemba, 2014 baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba na miezi kumi tangu alipoteuliwa na Rais, tarehe 19 Agosti, 2006

NB: Hotuba Kamili iko katika Tovuti ya Katibu Mkuu Kiongozi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kulia), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad(kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam,11 Desemba, 2014.

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YATEMBELEA MELI YA KIHISTORIA YA MV LIEMBA

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani.
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri zaidi ya miaka 100.
Mmoja wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.

MIKOA IHAMASISHE UWEKEZAJI WA VIWANDA.

Kaimu Meneja Utawala Bw. Atanas William  wa Kiwanda Cha Mafuta (Jielong Holdings) akitoa maelezo kwa timu ya ukaguzi jinsi mafuta yanavyofungashwa katika ndoo tayari kwa kwenda sokoni. Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha lita za mafuta milioni 2.4 kwa mwezi.

Na Oyuke Phostine - Shinyanga
Serikali imetoa wito kwa Ofisi za wakuu wa mikoa kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda kwenye mikoa yao ili kuweza kukuza uchumi wa mikoa husika na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa wakati akiongoza timu ya wataalam kutoka ofisi hiyo iliyokuwa  ikifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na sekta binafsi katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, na Mwanza.

Bw. Sangawe, alisema kuwa Wajibu wa Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza.  Alifafanua kuwa, moja ya vipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao utekelezaji wake unaishia 2015/16, ni miundombinu ili kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi.

Thursday, December 4, 2014

KIWANJA CHA NDEGE CHA KIGOMA KUTANULIWA

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakionesha eneo lililoainishwa na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya kazi ya utanuzi wa Kiwanja hicho.
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuanza kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
Azma imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa kiwanja hicho.
“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati ikiwamo Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.

Tuesday, December 2, 2014

KUKAMILIKA KWA UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE MPANDA, WAASWA KUTUNZA MIUNDOMBINU.

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelekezo ya uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kutoka kwa Meneja wa uwanja huo, Bw. Seneti Lyatuu (Kushoto).
Na Saidi Mkabakuli, Mpanda
Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi ya kuufanya uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya kuhakikisha miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.
“Kama munavyofahamu Serikali imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa miundombinu ya usafiri nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi za Serikali,” aliasa Bibi Mwanri.
Akitoa taarifa ya uendelezaji uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.
“Uwanja huu umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30,” alisema Bw. Lyatuu.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...