Friday, December 12, 2014

KATIBU MKUU KIONGOZI AMUAGA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI, BW. LUDOVICK UTOUH, NA KUMKARIBISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU MPYA WA HESABU ZA SERIKALI PROFESA MUSSA JUMA ASSAD, ALHAMIS, 11 DESEMBA 2014

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia), akimkabidhi zawadi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 11 Desemba 2014, amemuaga rasmi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovick Utouh, katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya Watendaji Wakuu na Waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuwa mahsusi pia kumkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.
Katika hotuba yake ya kumpongeza Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alielezea historia ya Utumishi uliotukuka ya Bw. Utouh ambayo imeleta sifa kubwa Ofisi hiyo ndani na nje ya nchi na katika medani za kimataifa. Kwa ujumla, hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi ilijikita kuelezea mchango binafsi wa Bwana Utouh kwa taifa ndani ya miaka zaidi ya arobaini (40) ya Utumishi wake Serikalini.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea mafanikio ya Serikali kwenye eneo la utawala bora, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za umma ambayo yamechangiwa na Bw. Utouh. Balozi Sefue aliwasihi watumishi wa umma kuiga weledi, uaminifu, msimamo, bidii na maarifa ambayo Bw. Utouh alivionyesha kwa vitendo katika utumishi wake.
Katibu Mkuu Kiongozi alitumia fursa hiyo pia, kumtakia kila la kheri, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Juma Assad, katika kufanikisha majukumu aliyopewa.
Bwana Utouh alistaafu rasmi nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, tarehe 19 Septemba, 2014 baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba na miezi kumi tangu alipoteuliwa na Rais, tarehe 19 Agosti, 2006

NB: Hotuba Kamili iko katika Tovuti ya Katibu Mkuu Kiongozi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kulia), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad(kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam,11 Desemba, 2014.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (wa pili kulia), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad (kushoto) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi Fatma Mohamed Said (kulia), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ndg. George Yambesi, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Bw. Philemon Luhanjo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, Bw. Ludovick Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi Fatma Mohamed Said na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh

Pichani Kutoka kushoto waliokaa ni: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Mussa Juma Assad Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, Bw. Ludovick Utouh, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi Fatma Mohamed Said wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara na Watendaji mbali mbali wa Taasisi za umma, katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014

Pichani, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue akitoa hotuba fupi ya kumpongeza kwa utumishi uliotukuka na kumtakia kila la kheri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh, katika hafla ya maalum na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ndg. George Yambesi, akisoma wasifu wa kiutumishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh, katika hafla ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam jana 11 Desemba, 2014.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh, akitoa neno fupi la shukrani kwa wageni waalikwa katika hafla ya maalum ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, 11 Desemba, 2014.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa pili kulia) akimpongeza Bw. Utouh mara baada ya kutoa hotuba fupi ya shukrani, Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu na kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...