Tuesday, June 9, 2015

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA IDADI YA WATU (UNFPA) TANZANIA YAENDESHA WARSHA KATIKA HOTEL YA GOLD CREST JIJINI MWANZA KWA AJILI KUHAMASISHA NA KUJENGA UWEZO WA KUJUMUISHA MASUALA YA VIJANA KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA MKOA NA WILAYA

Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
Na: Thomas Nyindo
       Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
Washiriki wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.

Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno la ufunguzi kwa ajili ya warsha hiyo kuanza rasmi.

Afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na vijana Bi. Tausi Hassan, akiwashukuru washiriki kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu warsha hiyo.

Bw. Ramadhani Hangwa afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na Program ya Idadi ya Watu na Maendeleo, akitoa neno kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue semina hiyo.

Mwezeshaji  Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.

Washiriki wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...