Wednesday, May 27, 2015

Ukweli juu ya Umri wa Sitti Mtemvu bado mzigo mzito kwake.

Mtangazaji wa kipindi cha NIRVANA akiwa na mrembo Sitti Mtemvu.

Miss Tanzania ambaye alilivua taji mwaka jana 2014, Sitti Abas Mtemvu amekiri wazi kuwa maisha yake hayakuwa na amani tena toka skendo yake ya kudanganya umri katika mashindano ya Miss Tanzania, ambapo yeye aliweza kuibuka mshindi na kuvishwa taji hilo, Jana kupitia katika kipindi cha Fashion cha NIRVANA cha EATV,
Malkia huyo alionyesha wazi kuwa suala la umri wake bado ni mzigo mzito kwake kwani hakuwa tayari kuweka ukweli kwa jamii juu ya umri wake.
Mtangazaji wa Kipindi cha NIRVANA alitaka Sitti Mtemvu awaambie ukweli wa Tanzania juu ya umri wake ili kuondoa dhana ya kuwa yeye ni muongo na alidanganya umri lakini mrembo huyo bado alionyesha kutokuwa tayari kusema ukweli, kutokana na kigugumizi ambacho alikuwa nacho katika kujibu suala hilo.
"Naomba watanzania tuachane na suala la umri wangu maana si jambo la msingi sana ila tunaweza kuaangalia mambo mengine ya msingi ya kimaendeleo, maana kwa sasa hilo suala mimi nishalifunga na naangalia mbele mambo mengine ya msingi"
Kuanzia mwanzo wa kipindi mpaka wanamaliza kipindi Sitti Mtemvu alisimamia msimamo wake wa kutosema umri wake ingawa alikubali na kuvitambua baadhi ya vyeti na stakabadhi ambazo zilionyeshwa katika mkutano wa waandishi wa habari ambavyo vilikuwa vikionyeshwa na waandishi hao.
Lakini pia Mrembo huyo alikana kuwa na mtoto na kusema mtoto huyo ambaye watu walikuwa wakimzushia kuwa ni mtoto wake si wake bali ni mdogo wake, pia alidai maneno hayo ya watu yalikuwa yakiathiri sana familia yake na yeye mwenyewe na ndiyo maana alikuwa kimya kwa kipindi cha miezi sita, mbali na hilo Sitti alishukuru kutokea kwa jambo hilo maana alidai ndiyo limemfanya kuja na kitabu chake cha Chozi la Sitti pamoja na kuweza kuanzisha asasi yake (NGO).
Licha ya kukataa kusema umri wake kwa jamii Sitti alikana pia tetesi zilizokuwa zikisema kuwa alitoa hongo ya penzi kwa muuandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania Hashim Lundenga na kusema suala hilo halina ukweli wowote bali ni uzushi wa watu, hapo hapo mrembo huyo alidai ya kuwa aliporudisha taji la Miss Tanzania hakuweza kurudisha zawadi aliyopewa ya pesa ambazo anadai zilikuwa ni Milioni 8 sababu hakuambiwa azirudishe ndio maana hakuweza kurudisha.
Chanzo: EATV.TV

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...