Kampuni ya kutengeza madawa ya GlaxoSmithKline
inataka kuruhusiwa kisheria kuidhinisha chanjo ya kwanza ya Malalaria
ikisema kuwa imeweza kupunguza vifo vya Malaria miongoni mwa watoto
barani Afrika.
Wataalamu wanasema kuwa wana matumaini kuhusu
mafanikio ya chanjo hiyo ya kwanza ya Malaria duniani baada ya kufanyiwa
majaribio.
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na
Mbu na ambao huwaua maelfu ya watu duniani kila mwaka.
Wanasayansi wanasema kuwa chanjo inayofaa ndio
njia ya pekee kumaliza ugonjwa wa Malaria.
Chanjo hiyo inayojulikana kama RTS,S
iligunduliwa kuwa iliweza kupunguza idadi ya vifo vya Malaria miongoni
mwa watoto wadogo wakati wa majiribio na pia iliweza kupunguza vifo
miongoni mwa watoto wachanga kwa 25% .
Kampuni ya GlaxoSmithKline (GSK) inatengeza
chanjo hiyo kwa usaidizi wa wakfu wa Bill na Melinda Gates.
Majaribio ya chanjo yenyewe yalifanyiwa barani
Afrika ambako iliwahusisha watoto 15,500 kutoka nchi saba.
Matokeo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa
matibabu uliofanyika mjini Durban, Afrika Kusini.
Kampuni ya GlaxoSmithKline sasa inataka kisheria
iweze kuruhusiwa kuanza kuuza chanjo hiyo ambayo imekuwa ikitengezwa
kwa miongo mitatu.
Kwa mujibu wa kampuini hiyo, inataka shirika la
afya duniani kuweza kuidhinisha matumizi ya RTS,S angalau kuanzia mwaka
2015 ikiwa wadhibiti wa madawa EMA wanaweza kuwapa leseni ya kuanza
kuuza chanjo hiyo.
Kulingana na utafiti uliofanyiwa watoto
waliopewa chanjo hiyo, ulionyesha kuwa miezi 18 baada ya kupewa chanjo
watoto waliona miezi mitano hadi 17 waliweza kukingwa dhidi ya ugonjwa
huo kwa 46% .Lakini watoto waliokuwa kati ya wiki 12 wakati huo waliweza
kukingwa tu kwa asilimia 27.
Msemaji wa kampuni ya GSK, aliambia shirika la
habari la AFP kuwa kampuni itawasilisha ombi lake chini ya mkakati wa
kuziwezesha nchi maskini kuweza kupata dawa.
Chanzo: BBC