Tuesday, July 2, 2013

MATUKIO KAMILI YA SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA OBAMA TANZANIA.

Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba
na watoto zao,wakiwasili chana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku
mbili hapa nchini.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani
muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani
muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na
mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani
Mama Michelle Obama.

Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa
Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana
na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam jana.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali
za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali
za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani
wakifurahia na kufuata mapigo ya ngoma za utamaduni katika uwanja wa
Ndege wa Mwalimu jijini Dar es Salaam jana mchana wakati wa mapokezi ya
kiongozi huyo wa Marekani na ujumbe wake.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi
wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.Picha na Freddy
Maro,Ikulu.
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam mchana wa jana


Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake,Rais Barack Obama wa Marekani wakati walipokuwa wakielekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Waandishi wa habari Ikulu,Jijini Dar es salaam jana.






Obama akipanda mti Ikulu ya Tanzania jana.


Monday, July 1, 2013

JOB ADVERTISEMENT TFDA - JUNE 30,2013

Rais wa zamani wa Chad akamatwa Senegal.

Polisi nchini Senegal , wamemkamata rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre, aliyekuwa anatafutwa kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wake wa miaka 8.
Wakili wa Bwana Habre, El Hadji Diouf, alisema kuwa alikamatwa na polisi kutoka nyumbani kwake mjini Dakar na kupelekwa sehemu isiyojulikana.
Habre mwenye umri wa miaka 70, amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani, nchini Senegal tangu mwaka 2005 alikokimbilia baada ya kung'olewa mamlakani mwaka 1990.
Aanatuhumiwa kuwatesa maelfu ya watu, wanaominika kuwa wapinzani wake.
Mwaka jana mahakama ya kimataifa ya haki, iliamuru Seengal kumchukuliwa hatua za kisheria au kupeleka kwingineko ambako atakabiliwa na sheria kwa uhalifu aliotenda.
Kukamatwa kwake kunakuja siku kadhaa baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kumsifu rais Macky Sall kwa hatua zake za kuelekea katika kumfungulia mashtaka Habre mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamekuwa yakishinikiza Senegal kwa miaka mingi, kumfungulia mashtaka Habre.
Tuhuma anazokabiliwa nazo ni za tangu mwaka 1982, wakati alipoingia mamlakani hadi mwaka 1990 alipoondolewa uongozini kwa njia ya mageuzi .
Habre alishtakiwa kwa mara ya kwanza nchini Senegal mwaka 2000, lakini mahakama za nchi hiyo ikaamua kuwa wakati huo isingeweza kushtakiwa huko.
Waathiriwa wa utawala wake baadaye waliwasilisha malalamishi chini ya sheria ya kimataifa ya Ubelgiji ambayo inaruhusu majaji wake kusikiliza na kuhukumu washukiwa wa kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu kokote duniani.
Hata hivyo Senegal imekataa ombi la Ubelgiji kumhamisha nchini humo ili ahukumiwe.

Chanzo:BBC

KONGAMANO LA WAZI JULAI 03,2013 WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

BEI KIKOMO ZA PETROLI KUANZIA JULAI 01,2013.

WATANZANIA MILIONI 32 KUPATA MAJI IFIKAPO 2016.


Waziri wa Maji Prof.Jumanne Maghembe.
Serikali imesema hadi ifikapo mwaka 2016 zaidi ya Watanzania milioni 32 nchini sawa na asilimia 74 watapata huduma ya maji safi na salama.

Hayo yalisemwa  jana mjini Dodoma na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe kwenye hafla fupi ya kuwaaga wajumbe zamani wa Bodi ya 5 ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa) na kuikaribisha Bodi mpya ambayo ipo chini ya Mwenyekiti Balozi Job Lusinde.

Profesa Maghembe alisema kwa upande wa vijijini kwa sasa ni asilimia 57 ya watu ndiyo wanaopata  maji safi na salama.

Alisema miradi ambayo inatekelezwa hivi karibuni vijijini inaonekana miundombinu yake imechakaa na watu wanaopata huduma hiyo bila tatizo ni asilimia 40.

“Uwezo wa kufanya hivyo tunao…iwapo hatutafanya vitu kama tulivyokuwa tunafanya zamani…bomba linatoa maji hapo badala la kulifunga mara moja tunaliacha,” alisema Akizungumzia kwa Mji wa Dodoma, alisema watu wanaotakiwa kupata maji safi na salama ni asilimia 99.

Kwa upande wake Balozi Lusinde alisema jitihada za Wana-duwasa zimezaa matunda kutokana na kupungua kwa kiwango cha upotevu wa maji kutoka asilimia 34 na kufikia 32.

CHANZO: NIPASHE

MISRI HALI TETE,RAIS ATAKIWA KUJIUZULU HADI KUFIKiA KESHO.

Umoja wa vyama vya upinzani unaompinga Rais Mohammed Morsi wa Misri, umemtaka Rais huyo kujiuzulu hadi kufikia kesho au atarajie uasi zaidi,na hii ikiwa ni mwaka mmoja tangu aingie madarakani. Siku ya jana ilimalizika kwa kuwashuhudia watu wakimiminika mitaani kwenye mji mkuu, Cairo. Wapinzani wanalituhumu kundi la Udugu wa Kiislamu la Rais Morsi kwa kuyateka mapinduzi ya umma, kupitia ushindi kwenye uchaguzi, kujilimbikizia madaraka na kutaka kuweka Sharia ya Kiislamu. Waandamanaji wengine wanasema wamevunjwa moyo na mgogoro wa kiuchumi. Maafisa wa usalama wanasema ofisi tatu za chama cha Udugu wa Kiislamu zilichomwa moto na waandamanaji kwenye jimbo la Nile Delta. Zaidi ya wafuasi 20,000 wa Rais Morsi pia walikusanyika karibu na kasri ya Rais mjini Cairo kumuunga mkono kiongozi huyo.

BRAZIL MABINGWA WA KOMBE LA MABARA ,NEYMAR MCHEZAJI BORA.

Kombe la Mabara limeitimishwa rasmi usiku wa kuamkia leo baada ya Brazil kutwaa taji hilo kwa kuwachapa Hispania magoli 3-0. Magoli ya Brazil yalifungwa na Frederico Chaves Guedes (Fred) dakika ya 2 na 47 huku na Neymar da Silva Santos  akifunga dakika ya 44.
Kukamilika kwa mashindano hayo tuzo mbali mbali zilitolewa kama ifuatavyo:-
Mchezaji Bora - Neymar da Silva Santos
Kipa bora - Julio Cesar
Mfungaji bora - Fernando Torres
Timu yenye nidhamu - Hispania (Licha ya kadi nyekundu ya Pique)

Saturday, June 29, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUKANUSHA BAADHI YA MATANGAZO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.

Katibu wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi wakati akizungumza na wandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu maswala mbalimbali ya Ofisi yake. Kulia kwake ni Naibu Katibu Idara ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili.

 

Taarifa ya Kukanusha Baadhi ya Matangazo katika Mitandao ya Kijamii

Ndugu Wandishi wa Habari, kwanza niwashukuru kwa kuitikia wito, nimewaita hapa kwa mambo mawili.
Awali ya yote nianze kwa kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuelimisha umma  juu ya masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii licha ya changamoto mbalimbali mnazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yenu.

Baada ya kusema hayo, nianze kueleza nilichowaitia hapa nikitambua umuhimu  wa nafasi yenu katika jamii hususan katika kuelimisha umma kupitia vyombo vyenu.   Moja ya kazi za msingi za taasisi yetu kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kutangaza nafasi wazi za Ajira kwa mujibu wa mahitaji.

Napenda kutoa rai kupitia  kwenu na kwa wadau wetu wote watambue kuwa ni kosa kwa mtu au taasisi yoyote kuchukua matangazo ya Sekretarieti ya Ajira bila idhini na kuyafanyia marekebisho.  Vile vile ni kosa kwa mujibu wa sheria kuandaa  matangazo mbalimbali yanayohusiana na Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupotosha umma ilhali wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazozichapisha au kuziandika katika baadhi ya mitandao ya kijamii siyo halali na hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira.

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UTUMISHI, JULAI 2013.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...