Saturday, May 18, 2013
MABOMU YAUA 77 NA KUJERUHI KADHAA - IRAQ
Wimbi la mashambulio ya mabomu limewaua kiasi ya watu 77 na kuwajeruhi wengine wengi nchini Iraq hapo jana huku ghasia za kimadhehebu zikiongezeka nchini humo.
Kituo cha televisheni cha Alsumaria kimeripoti kuwa takriban watu 20 wameuawa na wengine 32 wamejeruhiwa wakati mabomu ya kutegwa kando ya barabara yaliporipuka moja baada ya jingine katika eneo la kibiashara katika mji wa Amariya magharibi mwa mji mkuu Baghdad.
Katika mji wa Baquba bomu lililotegwa katika gari liliripuka nje ya msikiti wa Wasunni na kuwaua watu 38 na wengine 55 wamejeruhiwa. Mripuko huo ulitokea wakati waumini walipokuwa wakitoka kusali sala ya mchana.Picha katika vituo vya televisheni nchini humo zimeonyesha miili ikiwa imetapakaa karibu na msikiti huo maarufu wa Saria.watu saba wameuwawa na wengine 10 wamejeruhiwa wakati bomu liliporipuka katika mazishi ya kaka yake mbunge wa kisunni katika eneo la Bayia magharibi mwa Baghdad.
Watu wengine 10 wameuawa na wengine 32 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu katika mazishiya kishia katika mji wa Maadan kusini mwa Baghdad.
SOURCE: DW
DR.SLAA ANAANZA ZIARA YA UJENZI WA CHADEMA MKOA WA MANYARA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KATIBU Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza
ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za
Mkoa wa Manyara, siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013
Katika ziara hiyo
Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja
na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara.
Akiwa katika ziara
hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo
atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili
kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na
wanachama na viongozi wa maeneo husika.
Ratiba ya ziara hiyo
itakuwa kama ifuatavyo;
Atawasili Babati
Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu
kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9
mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini.
Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang).
Tarehe 20/5/2013,
Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Haydom
(Mbulu).
Siku ya tarehe
21/5/2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh
na Mbulu Mjini.
Tarehe 22/5/2013 akiwa
njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji
vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara
Galapo, Babati Vijijini, kuanzia saa 8 mchana.
Siku ya tarehe
23/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda
na Bashnet, Babati Vijijini.
Tarehe 24/5/2013,
Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika
maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.
Siku inayofuata,
tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo
ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa
Mererani, kuanzia saa 10 jioni.
Imetolewa leo, Mei
17,2013 na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa
Habari CHADEMA
Friday, May 17, 2013
KUITWA KAZINI KWA WALIOFANYA USAILI TAREHE 06-13 APRILI,2013.
KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwaarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 06 hadi 13 Aprili, 2013 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=143

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WALIOOMBA KAZI - MZUMBE UNIVERSITY.
Kwa tangazo, tarehe na majina fungua link ifuatayo:
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=145
http://ajira.go.tz/index.php?option=com_docman&task=doc_details&Itemid=0&gid=145
MAJINA YA WAGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA - KANDA YA KASKAZINI.
TAARIFA KWA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI -
KANDA YA KASKAZINI
Tarehe 15
Mei 2013, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania
nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya
Kaskazini.
Wagombea
hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa
sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya
kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika
kuwatumikia.
Wagombea
waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
JINA LA MGOMBEA
|
KATA
|
JIMBO
|
MKOA
|
BI. YOSEPHA
KOMBA
|
GENGE
|
MUHEZA
|
TANGA
|
BW. OMARI
HATIBU SALIMU
|
TINGENI
|
MUHEZA
|
TANGA
|
BW. LAWRENCE
SURUMBU TARA
|
BASHNET
|
BABATI
VIJIJINI
|
MANYARA
|
BW. ERNEST
JOROJIK
|
DONGOBESH
|
MBULU
|
MANYARA
|
ENG.
JEREMIAH MPINGA
|
ELERAI
|
ARUSHA
MJINI
|
ARUSHA
|
BW. RAYSON
NGOWI
|
KIMANDOLU
|
ARUSHA
MJINI
|
ARUSHA
|
BW. MALANCE
KINABO
|
THEMI
|
ARUSHA
MJINI
|
ARUSHA
|
BW. EMMANUEL
KESSY
|
KALOLENI
|
ARUSHA
MJINI
|
ARUSHA
|
BW. JAPHET
SIRONGA LAIRUMBE
|
MAKUYUNI
|
MONDULI
|
ARUSHA
|
CHAMA
kimejipanga kushiriki uchaguzi huu kikamilifu sana na katika maeneo yote kanda
imeteua MAMENEJA WA KAMPENI ili kuhakikisha uratibu na utekelezaji wa kampeni
kwa mfumo tuliouweka.
Imetolewa leo tarehe 16 Mei 2013.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
Thursday, May 16, 2013
CALL FOR APPLICATIONS FOR TRAINING WORKSHOP ON M&E - UDSM.
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, DEPARTMENT OF GEOGRAPHY
CALL FOR APPLICATIONS FOR TRAINING WORKSHOP ON MONITORING AND EVALUATION OF DEVELOPMENT PROJECTS
The department of Geography of the University of Dares Salaam is announcing a five days workshop training on MONITORING AND EVALUATION FOR DEVELOPMENT PROFESSIONALS to be conducted at the University of Dar es Salaam Main Campus from 27th to 31st May, 2013.

CALL FOR APPLICATIONS FOR ADMISSION (EVENING CLASSES)- SAUT.
ST. AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA P.O. BOX 307, MWANZA, TANZANIA
St. Augustine University of Tanzania invites applications from qualified candidates for admission into parallel programmes (Evening Classes) into CERTIFICATE, DIPLOMA and DEGREE PROGRAMMES at Mwanza Campus.

CALL FOR APPLICATION FOR DEGREE & DIPLOMA PROGRAMMES- JoKUCo
JOSIAH KIBIRA UNIVERSITY COLLEGE OF TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA
P.O. BOX 1023, BUKOBA, TANZANIA
Tel: +255 732 983 642; +255 732 983 643; Fax: +255 732 983 644
E-mail: admission@jokuco.ac.tz; or jokuco@jokuco.ac.tz; Website: www.jokuco.ac.tz
CALL FOR APPLICATION FOR DEGREE AND DIPLOMA PROGRAMMES FOR 2013/2014 ACADEMIC YEAR
Josiah Kibira University College (JoKUCo) of Tumaini University Makumira (TUMA) invites applications for qualified candidates to apply for Degree and Diploma Programmes for Academic Year 2013/2014.
Degree Programmes:
BAADA YA SERIKALI KUKASILISHWA NA KATIKA KATIKA YA UMEME,KUIFUMUA TANESCO.
Serikali ilitangaza kuwa inakamilisha zoezi la kuifumua TANESCO na kuiunda upya kwa kuigawa katika makundi ili iweze kuwa na ufanisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)