Huduma za usafiri wa treni katikati ya jiji la
dar es salaam zinatarajiwa kuanza tena Jumatatu Aprili 22 kufuatia
kukamilika kwa Ukarabati wa reli katika eneo lililokuwa limeharibiwa na
mvua zilizonyesha hivi karibuni na kwamba hakuna badiliko la nauli.
Taarifa kamili tutawaletea baadae.
Sunday, April 21, 2013
NJIA YA YANGA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU YAZIDI KUTAKATA,YAILAZA JKT RUVU 3-0
Fuatana nami ujue nini kilikuwa kinatokea hatu kwa hatua kama ifuatavyo:-
Mpira unamalizika Yanga 3 - 0 JKT
Dk 90+4 Mgosi anachezewa faulo na Yondani nje kidogo ya eneo la hatari la Yanga. Faulo inapigwa na mpira unaokolewa na kuwa kona. Yanga 3-0 JKT
Dk 90+1 Nizar anapiga shuti kali linalopanguliwa na kipa wa JKT, Dihile.
Dk 89 Mwamuzi wa akiba Idd Soud anaonyesha bango kwa mpira umeongezwa dakika 5
Mara yangu ya mwisho kumuona Said Mohamed kwenye uwanja huu ni mwaka jana alipoingia kama sub kuchukua nafasi ya Yaw Berko kwenye mchezo ambao yanga walifungwa mabao 5:0 na Simba
Dk 86 Yanga inafanya mabadiliko ametoka Barthez ameingia Said Mohamed.
Dk 86 Inaonekana Barthez hawezi kuendelea na Said Mohamed anapasha misuli moto kujiandaa kuingia.
Dk 84 Kipa wa Yanga, Barthez anaanguka mwenyewe na mpira unaendelea kusimama ili Barthez atibiwe.
Dk 83 Mpira unasimama kwa muda baada ya Msuva kuchezewa rafu na Zahor Pazi. Yanga 3-0 JKT.
Dk 80 Jerry Tegete anaingia badala ya Hamis Kiiza
Dk 78 JKT wanafanya mabadiliko ametoka Ally Mkanga ameingia Charles Thadei.
Dk 76 JKT wamefanya mabadiliko ametoka Hassan Kikutwa ameingia Sosthenes Manyasi.
Dk 76 JKT wamefanya mabadiliko ametoka Hassan Kikutwa ameingia Sosthenes Manyasi.
Dk 75 Chuji wa Yanga anamchezea faulo Hussein Bunu wa JKT.
Dk 73 Msuva anachezewa faulo na Nashon Naftal nje kidogo ya eneo la hatari la JKT. Faulo inapigwa JKT wanaokoa. Yanga 3-0 JKT
Leo Yanga wametoa burudani kwa mashabiki walioingia uwanjani kwa soka safi
Shuti kali la Chuji linadakwa na kipa wa JKT
Goaaaaaaaaaaaal Nizar Khalfan anaipatia Yanga goli la 3
Dk 62 Mgosi anachezewa faulo na Kelvin Yondani.
JKT wanafanya mabadiliko anatoka Amos Mgisa anaingia Abdallah Bunu
Gooooooooal Free kick iliyopigwa na luhende imeunganishwa na Hamis Kiiza kwa kichwa
Dk 57 yanga wanapata faulo baaada ya Msuva kufanyiwa madhambi
Dk 55 Ally Nkanga analimwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Nizar
Dk 53 Kiiza wa Yanga anashindwa kuunga vizuri pasi ya Domayo kwa shuti lake kutoka nje ya eneo la hatari la JKT.
Dk 49 JKT wanapiga kona na Yanga wanaokoa.
Dk 49 JKT wanapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari. Faulo inapigwa lakini Cannavaro anautoa nje mpira na kuwa kona.
Dk 48 Mgosi anapiga shuti hafifu na Barthez anaudaka mpira.
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, JKT Ruvu 0 - 1 Young Africans
Dk 45 HALF TIME! Yanga 1-0 JKT
Simon Msuva anaipatia yanga bao hapa
Dk 41 Stanley Nkomola anapiga kona lakini kipa Barthez anaokoa.
Dk 39 Mgosi anamchezea faulo Cannavaro.
Dk 36 JKT wanapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Yanga. Faulo inapigwa na mabeki wa Yanga wanaokoa.
Dk35 Hamis kiiza anakosa bao la wazi
Dk 31 Yanga inapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari la JKT. David Luhende anamtengea Haruna Niyonzima lakini shuti lake linawababatiza mabeki wa JKT na mpira unaokolewa.
Dk 30 yanga wanapata kona nyingine Dihile anaokoa
Dk 26 Kwa mara ya tatu ndani ya dakika nne zilizopita mabeki wa Yanga wanamwekea Mgosi mtego wa kuotea naye anashindwa kung'amua hali hiyo na mara nyingi anajikuta akiwa ameotea.
Dk 26 Kwa mara ya tatu ndani ya dakika nne zilizopita mabeki wa Yanga wanamwekea Mgosi mtego wa kuotea naye anashindwa kung'amua hali hiyo na mara nyingi anajikuta akiwa ameotea.
Dk 24 Mussa Mgosi wa JKT anaipangua ngome ya Yanga lakini shuti lake linadakwa na kipa Ally Mustapha 'Barthez'.
Almanusura Nadir aipatie yanga bao kutokana na faulo ya Luhende
Dk 22 yanga wanapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari
Dk 19 Athuman Idd Chuji wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa JKT lakini mpira unatoka nje kidogo ya lango.
Dk 18 Zahor Pazi wa JKT anachezewa faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Yanga. Faulo inapigwa lakini mpira unatoka nje.
Dk 16 Yanga wanapata kona baada ya Damas Makwaya kuutoa nje mpira. Kona inapigwa na Dihile anaudaka mpira.
Dk 15 Kipa Dihile wa JKT anaudaka mpira wa krosi uliokuwa ukiwaniwa na Kiiza.
Dk 13 JKT wameanza kumiliki mpira na kuisumbua ngome ya Yanga. Yanga 0-0 JKT
Dk 12 Yanga inapata kona lakini kipa wa JKT, Shaaban Dihile anaudaka mpira.
Dk 10 Hamis Kiiza wa Yanga anamiliki mpira vizuri akipokea pasi ya Frank Domayo lakini mwamuzi Oden Mbaga anasema Kiiza ameoteaM
Yanga wanacheza vizuri sana hasa kwenye eneo la kiungo.
Dk 8 Mbuyu Twite wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa JKT lakini mpira unatoka juu kidogo ya mlingoti.
DIHILE AMENYANYUKA ANAPIGA FAULO
Shambulio hilo limesababisha golikipa wa JKT Dihile kuumia yupo chini anatibiwa
Dk ya tatu kona ya Luhende imesababisha kizaazaa kwenye lango la jkt ruvu
Yanga wanapata kona na inapigwa na David Luhende
Musa mgosi anamlazimisha Cannavari kuutoa nje mnamo dk 2
Mpira umeanza hapa taifa Yanga SC 0-0 JKT
Muda wowote kuanzia sasa soka litaanza na yanga ndo wanaanzisha kipute
Makame Rashid alifariki mwanzoni mwa juma hili,alikuwa mdau mkubwa wa soka
Wachezaji wanasimama kuomboleza kifo Makame rashid
JKT Ruvu line up: Shabani Dihile, Hassan Kikutwa, Stanley Mkomola, Madenge Ramadhan, Damas Makwaya, Nashon Naftar, Amos Mgisa, Ally Mkanga, Mussa Mgosi, Zahor Pazi na Haruna Adolph.
Kikosi cha Yanga
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.David Luhende
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6. Athunman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Hamis Kiiza
10.Nizar Khalfani
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Salum Telela
5.Nurdin Bakari
6.Said Bahanuzi
7.Jerson Tegete
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Salum Telela
5.Nurdin Bakari
6.Said Bahanuzi
7.Jerson Tegete
CHANZO,SHAFII DAUDA
AMUUA BABA YAKE KISA USHIRIKINA.
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka Richard Jecap (30) mkazi
wa kitongoji cha Matai A kwa tuhuma za kumuua baba yake kwa kumpiga
mpini kichwani akimtuhumu kuwa ni mshirikina.
Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua.
Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua.
Akizungumza mwenyekiti wa kijiji
hicho, Emmanuel Mwakibinga alisema kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji hayo
baada ya watoto wake kufariki ambapo mtoto wa kwanza mwenye umri wa
miaka minne alifariki Januari mwaka huu na alikuwa akidai baba yake huyo
ndiye aliyemloga.
Alisema kuwa Aprili 16 mtoto wake wa pili mwenye
umri wa miaka miwili alifariki na alidai kuwa baba yake ndiye aliyemloga
kwani amekuwa akiloga watoto wake hao na siku ya mazishi aliahidi
kumfanyia kitu kibaya baba yake huyo licha ya kuwa hakueleza ni kitu
gani.
Mwenyekiti huyo alisema siku ya tukio hilo alikuwa akipita karibu na nyumba hiyo akasikia kishindo kikubwa kutoka eneo la nyumba hiyo na kisha kufuatia vilio vya watu na aliposogea alikuta mtuhumiwa huyo amekwishampiga mpini kichwani baba yake huyo na kisha kuanguka na kupoteza fahamu.
Baada ya kuona hivyo, walisaidiana pamoja na
wanafamilia wengine kumwahisha hospitali na alitundikiwa maji sambamba
na kushonwa katika jeraha kubwa alilolipata kichwani na usoni na kisha
kulazwa ili kuendelea kupata matibabu.
Mwakibinga alisema kuwa wakati akiendelea kupatiwa
matibabu alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi na maumivu
makali aliyokuwa nayo katika jeraha alilolipata baada ya kupigwa na
mpini wa shoka kichwani.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
BARAZA LA WAFANYAKAZI MORUWASA LATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI.
Baraza la wafanyakazi MORUWASA lilifanya ziara katika hifadhi ya taifa ya Mikumi baada ya kumaliza kikao chake cha siku mbili katika Hoteli ya Chuo Cha VETA MIkumi.Hii ni rasili mali na hazina kwa Taifa letu,wote tushirikane kulinda na kuhifadhi.
Hapa ni bwawa kati ya mabwawa 3 yaliyochimbwa mbuni mikumi.Wanyama wanaopatikana ni Mamba,Kiboko na ndege maji |
Eneo la kuingilia mbugani Mikumi |
Pundamilia ambao kitu pekee kwao nikwamba wanasimama kila mmoja akiwa ameelekea upande wake kwa ajili ya usalama |
Hawa ni Tembo ambao wanapatikana kwa wingi mbugani Mikumi |
Hawa ni nyumbu ambao nao wanapatikana kwa wingi Mikumi. |
Hawa ni Twiga ambao kitu pekee kwao ni kuwa wakiwa wanatembea miguu ya upande mmoja inaenda pamoja tofauti na wanyama wengine ambao wanapishanisha miguu. |
Huyu ni kiboko aliyemo kwenye mabwawa yaliyochimbwa. |
Hawa ni nyati ambao wanasemekana kuwa wanya wakorofi hasa wakimuona mwanadamu. |
Mikumi kuna hata uwanja wa ndege,unaweza kutua moja kwa moja na ndege. |
Watu husema twiga huwa halali ukweli nikwamba analala kama anavyoonekana lakini hawezi kuinamisha kichwa,analala hivo hivo |
Hawa ni swala ambao wanapatikana kwa wingi Mikumi.Kitu cha pekee kwao ni kwamba dume moja unakuta linamiliki kundi kubwa la majike hata kuzidi idadi ya 100. |
BOSTON YATULIA BAADA YA MSAKO MKUBWA
Wananchi wa Bosto wakionesha furaha yao baada ya msako kukamilika |
Shughuli zilisimama katika jiji zima mnamo siku ya Ijumaa wakati polisi waliposambazwa kila pembe kumtafuta mshukiwa huyo Dzhokhar Tsarnaev, mwenye umri wa miaka19.
Alipatikana amejificha bustanini mwa nyumba moja katika kitongoji kimoja na alikamatwa baada ya mapambano ya risasi ambapo alijeruhiwa.
Kaka yake , Tamerlan, aliuwawa awali katika mapambano ya risasi na polisi. .
Watu watatu waliuwawa na zaidi ya 170 walijeruhiwa katika mashambulio ya mabomu ya siku ya Jumaatatu na afisa mmoja wa polisi aliuwawa wakati wa msako wa washukiwa..
Dzhokhar Tsarnaev anazuiliwa chini ya ulinzi mkali hospitali ambako pia wanatibiwa wengi wa waliojeruhiwa na mabomu siku ya Jumatatu.
Maafisa wa polisi wanasema wananuia kumhoji bila ya kumsomea haki zake kama mshukiwa --kama haki yake ya kumwita wakili na kutosema chochote kwa sababu za usalama kwa raia.
Uamuzi huo ulishutumiwa na Jumuiya inayotetea haki za raia nchini Marekani ilioyosema kwamba hatua kama hiyo inahusu tu kesi ambazo zinahusika na vitisho vya papo hapo kwa usalama na wala hakuna sababu ya kumnyima mshukiwa haki hizo.
Lakini baadhi ya wabunge wa chama cha Republican wamehoji kwamba Tsarnaev achukuliwe kama ni-mpiganaji adui ikimaanisha hastahili kupewa haki kama anazopewa mshukiwa wa jinai.
CHANZO:BBC
TETEMEKO KUBWA LAITIKISA CHINA,WATU 150 WAFA
Shirika la habari la taifa la Uchina linasema kuwa
watu 150 wamekufa katika tetemeko kubwa la ardhi ambalo limeporomosha
majengo na bara-bara katika jimbo la Sichuan, kusini-magharibi mwa nchi.
Wanajeshi kama 6000 wamepelekwa
kwenda kusaidia katika uokozi zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji
mkuu wa jimbo la Sichuan.
Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika.
Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo.
Tetemeko lilotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu 90,000.

CHADEMA: WABUNGE WALIOFUKUZWA NI MASHUJAA
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewasifu
wabunge wa chama hicho waliosimamishwa huku akimshambulia Spika wa
Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai kuwa wanaliendesha Bunge
kiharamia.
Akizungumza
jana katika uzinduzi wa M4C ya CCADEMA kwa Kanda ya Kati, Mbowe alisema Spika
Makinda amekuwa ni mwongo hata kuidanganya dunia kuwa uamuzi wao ni
sahihi jambo ambalo si kweli.
“Spika
Makinda ni mwongo, ameidanganya dunia na amekuwa akitumia maneno ya
uongo kuhalalisha uharamia uliofanywa na Naibu Spika wa Bunge kwa
kuwatoa ndani wabunge watano wa Chadema,”alisema na kuongeza:
“Uhuni kama
huu ndugu zangu haukubaliki, tutaendelea kufanya kazi usiku na mchana
kuhakikisha tunatetea masilahi ya nchi hii na watu wake. Na hapa
natangaza mbele yenu kuwa wabunge walioondolewa ndani ya Bunge ni
mashujaa,” alisisitiza Mbowe.
Mbowe ambaye
ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, aliwaambia wanachama na
mashabiki wa Chadema kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu ndani
ya Bunge na kwamba wanatakiwa kuwa majasiri wakiwa bungeni.
Alisema
kwamba wakati wote wamekuwa wakishutumiwa kuwa wanafanya fujo ndani ya
Bunge, jambo alilosema siyo kweli bali wao wanasimamia Kanuni za Bunge
ambazo zimekuwa zikivunjwa na Spika na Naibu wake kila wanapokuwa ndani
ya viti vyao.
Alisisitiza
kuwa hawako tayari na kamwe hawatakuwa tayari kutii mamlaka yoyote
wanayoamini kuwa inawakandamiza na kuwaondolea haki yao, zaidi ya
kupambana.
Kiongozi
huyo alinukuu baadhi ya vifungu vya Kanuni za Bunge alivyosema kuwa
vingetumika kwa kumaliza tatizo la Lissu, aliyemwelezea kuwa alikuwa
sahihi, hata angesimama mara mia moja kwa sababu alikuwa akipinga
upuuzi.
Kuhusu Katiba
Akizungumzia
masuala ya mchakato wa Katiba Mpya, Mbowe alisema kuwa uamuzi
uliotolewa ndani ya Bunge katika hotuba yake ndiyo msimamo wa Chadema,
akatahadharisha kuwa ikiwa Serikali haitakubali kufanya marekebisho
waliyopendekeza, chama hicho kitajitoa.
“Ule ulikuwa
ni msimamo wa Kamati Kuu ya chama chetu na bado tunasisitiza kuwa
wasipokuwa makini tutajitoa. Kama noma na iwe noma, hata kama uchaguzi,
tutashinda kwa nguvu ya Mungu,” alisema na kushangiliwa na umati wa
watu.
Hata hivyo,
alionya kuwa kama Serikali itapuuza ushauri wao, itaisoma namba kwa kuwa
wanajua kinachotaka kufanywa na tayari wameshajipanga kukabiliana
nacho.
Dk Slaa ammwagia sifa Lissu
Kwa upande
wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk Wilbrod Slaa alimwagia sifa Mbunge wa
Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Tundu Lissu, kuwa yeye na wenzake watano waliondolewa kishujaa
na wanatakiwa kusonga mbele zaidi.
CHANZO:Mtandao wa kijamii wa CHADEMA
WARAKA WA NDUGU GOLDEN CHARLES MARCUS KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
GOLDEN CHARLES MARCUS
WARAKA WANGU KWA SERIKALI, TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NA
WANANCHI KWA UJUMLA
(Kwenye Mitandao ya Kijamii:- Gmail, Yahoo, Facebook,
YouTube, Amazon, Twitter na AOL)
Mwanzo Kabisa, kabla hata ya kuanza Mchakato wa Kupata
Katiba Mpya, Tume ya Mabadiko ya Katiba ilitafuta na kupata na kutumia
Kaulimbiu isemayo TOA MAONI, TUPATE KATIBA MPYA, na Dira yake ilikuwa KUFANIKISHA
KUPATIKANA KWA KATIBA MPYA huku Dhamira yake ikiwa ni KURATIBU, KUKUSANYA NA
KUTHAMINI MAONI YA WANANCHI ILI KUPATA KATIBA MPYA.
Tume hiyo ya Katiba ikaanza Kazi mara moja kwa Ukusanyaji wa
Maoni ya makundi mbalimbali mnamo tarehe 7 – 25 January, 2013, baada ya hapo
ilichambua Maoni ya Wananchi mnamo 3 Februari – 4 Machi, 2013, Mnamo tarehe 4
Aprili ikaanza Uandishi wa Rasimu ya Katiba ambayoitashia 2 Mei, 2013.
Lakini licha ya Mipango hiyo mizuri ya Tume, kuna baadhi ya
vitu vinafanyika / vimefanyika bila mtazamo mkubwa na wakina na wandani zaidi kwa
sababu Wananchi ndiyo watoa Maoni na ndiyo wapendekezaji wakubwa katika hatua
hizo za Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Tume ilianzisha mchakato wa kuandaa
mabaraza bila kufikilia kwa mapana zaidi kuwa, kilichotakiwa kufanyika ni:-
Kutoa tangazo kwa Wananchi ili watume maombi – hili lilifanyika Vizuri
WDC (Baraza la Maendeleo la Kata la Wenyeviti wa Mitaa na
Madiwani husika) walitakiwa wachambue maoni na kupitisha watu wenye sifa husika
kwenda kuhakikiwa na Wananchi, kisha Wananchi ndiyo watoe maamuzi ya nani
atakayekuwa muwakilishi wao au Uteuzi wa moja kwa moja kutoka kwa Wananchi, sasa
mambo yakawa kinyumenyume ikaanza kwa Wananchi nao kwakuwa hawajui
kinachoendelea Wakateuwa na kuwaamini Watu watakao wawakilisha, baada ya
Wananchi kuchagua watu watakao wawakilisha, Baraza hilo la WDC likatengua
maamuzi ya Wananchi na kufanya Uchaguzi upya bila Wananchi kujua (Mchuujo),
huku Wananchi wakiamini wamemaliza kupeleka Wawakilishi wao!! kwa namna hii unafikili DIRA na DHAMIRA ya TUME YA KATIBA itafikia
malengo?
Mbali na hayo, kazi hii ya Uchaguzi au Muundo wa Mabaraza
ulikuwa ni wa KITAIFA badala yake umefanyika kwa UDINI, UCHAMA, RUSHWA na UDANGANYIFU
MKUBWA, kwa jinsi hiyo imepelekea Wananchi wengi kupoteza Imani na Tume, kwa
mfano Kata ninayotoka mimi GOLDEN CHARLES MARCUS Kata ya Kitaji Musoma Mjini
hayo yalijionesha wazi wazi na nilijaribu kuomba Muongozo wa Tume kama
yanayofanyika ni sahihi kwa kutuma sms kwenye Namba 0715 081508, 0767 081508,
0787 081508, 0774 081508 (namba hizi ni
za Tume) bila majibu yoyote.
Katika Kata yangu kuna Mitaa minne yaani Kitaji ‘A’, ‘B’,
‘C’ na ‘D’ pamoja na Madiwani watatu, wakuchaguliwa mmoja, viti maalum wawili, 02/04/2013
ulifanyika Uchaguzi wa Wawakilishi wa Mabaraza katika Ngazi ya Mtaa, kwenye
kundi langu nililoomba la kuwakilish Vijana nilichaguliwa na Wananchi kutoka Mtaa
wa Kitaji ‘C’ kwa Kura 120 huku aliyenifuatia alikuwa na kura 97, baada ya
Uchaguzi huo wa Tarehe 02/04/2013, tulikutana tena kwenye Mchuujo wa Ngazi ya
Kata (WDC) 08/04/2013 lakini kulikuwa na mama mmoja ambaye ni Mwl. Wa shule ya
Msingi Azimio na anaishi hapo hapo shule ina maana ni
Mtumishi wa Serikali
kadhalika Mme wake ni Trafki (Polisi wa Usalama Barabarani) na si Mkazi wa
kudumu wa Kata husika kama Tangazo la Maombi lilivyoahinisha, kwa jinsi
ninavyojua kuwa Mtumishi wa Serikali haruhusiwi kuwania nafasi kama hiyo nakama
angekuwa mkazi wa kawaida, kwa sehemu anayoishi ilimpasa mama huyu kugombea
Kitaji ‘C’ sababu shule anayoishi hiko Kitaji ‘C’, lakini alitumia pesa kwa
M/kiti wa Kitaji ‘C’ na Kitaji ‘B’ akafanyiwa mpango na kapita kwa mabavu na
ujanja ujanja mwingi na udanganyifu Mkubwa akawa ameshindia Kitaji ‘B’ ambayo
kitaratibu shule anayoishi haiku huko ina maana si Mkazi wa ‘B’.
Wakati tunasubiri Kikao hicho cha kutengua maamuzi ya Wananchi
cha 08/04/2013 mama huyo na Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata hii kilitangaza
Uchama sana na hata kufanya Vikao vya Usiku na Mchana kupanga safu yao
waliyoitaka, huku Wagombea kutoka Chama hicho wakifanya Kampeni chafu za Rushwa
na Uchama Usiku na Mchana mpaka nikajuta kugombea, nanikajiuliza kama hali
ilikuwa hivyo kwanini kazi hii wasingewapa watu wa CCM au Watu ambao wamewaanda
kuliko kutangazia UMMA halafu wao wanapanga Orodha ya Majina ya Watu ambao
wanawataka na kweli inakuwa hivyo huku Wananchi wakiwa wameduwaa kwa Matokeo ya
Mchuujo.
Kwa Upande wangu nilishangaa sana na kwa hatua hiyo Wananchi
walio wengi itakuwa ngumu kwao kuamini Kaulimbiu, Dira na Dhamira ya Tume,
Hivyo kwa Waraka huu Tume iangalie chakufanya mapema, kama kubatilisha Uchaguzi
huu, ama vinginevyo kwa kadri ya Maamuzi ya Wananchi wengi, waliopiga kura na
kubatilishwa na Wachache (WDC) kwa manufaa yao, itakuwa Ngumu kwa Wananchi, hii
imeonekana wazi kuwa, ni namna gani Uongozi mdogo wa Chini unavyochonganisha
Wananchi na Viongozi wa Juu wa Taifa kama Mchezo huu utakuwa hahukusukwa toka
juu, kwa Uchaguzi huu wa wawakilishi wa Mabaraza katika Kata yangu ya Kitaji –
Musoma, hauko mbali na Matokeo ya Kidato cha Nne, yaani waliofanya Mahojiano
yaani kujieleza mbele ya Baraza (WDC) hawakuchaguliwa
(wamefeli) lakini ambao hawakuwepo na walikuwa wameshatengeza Mazingira Mazuri
(Kampeni + Rushwa + Uchama) na hawakujieleza, wameshinda!!!!
hii nini au Hili ni
Taifa gani tunaloliandaa?.
MWISHO:
Wananchi ndiyo watumiaji wa Katiba na ndiyo wenye maamuzi
makubwa, Waheshimiwe na kusikilizwa katika maamuzi yao.
GOLDEN CHARLES
MARCUS
Mteule wa Wananchi – Kitaji ‘C’
0767 328202 / 0784 328202 / 0777 328202 / 0658 284625
(Kijana Mwenye Uchungu na TaifaCHANZO,Mtandao wa kijamii wa CHADEMA
Saturday, April 20, 2013
JOB VACANCIES - JoKUCo (UNIVERSITY)
JOSIAH KIBIRA UNIVERSITY COLLEGE OF TUMAINI
UNIVERSITY MAKUMIRA
P.O.BOX 1023 BUKOBA, TANZANIA
TEL.+255732983642;+255732983643; FAX +255732983644
Email: jokuco@jokuco.ac.tz; website:www.jokuco.ac.tz
18.03.2013
THE JOSIAH KIBIRA UNIVERSITY COLLEGE (JoKUCo) OF TUMAINI UNIVERSITY
MAKUMIRA (TUMA) INVITES APPLICATIONS FOR LECTURERS WHO CAN TEACH
HISTORY, GEOGRAPHY, ENGLISH, KISWAHILI, FRENCH, EDUCATION, INFORMATION
AND COMPUTER TECHNOLOGY, BUSINESS ADMINISTRATION, PHYSICS, CHEMISTRY,
BIOLOGY AND MATHEMATICS.
APPLICANTS SHOULD HAVE MASTERS DEGREE WITH A MINIMUM PASS OF B+ (GPA
OF 3.5) OR Ph.D. APPLICATIONS SHOULD BE SENT TO THE PROVOST, JOSIAH KIBIRA
UNIVERSITY COLLEGE, P.O.BOX 1023, BUKOBA AND THROUGH THE EMAIL ADDRESS:
jokuco@jokuco.ac.tz THE DEADLINE IS 31ST OF MAY, 2013.
By DEPUTY PROVOST FOR ACADMIC AFFAIRS
FOR PROVOST
AZAM YABANWA MBAVU NYUMBANI NA RABAT
AZAM
FC imelazimishwa sare ya bila kufungana jioni hii na AS FAR Rabat ya
Morocco katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, Kombe la Shirikisho
Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Azam iwe na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo Morocco, wakitakiwa lazima kushinda au kutoa sare ya mabao ili kufuzu.
Pamoja na sare hiyo, Azam watakumbuka sana mabao matatu ya wazi waliyokosa kupitia kwa washambuliaji wao wa pembeni, Kipre Herman Tchetche mawili na Khamis Mcha ‘Vialli’ moja,
Kipre aligongesha mwamba mashuti mawili katika dakika za 51 pembeni kushoto katikati na dakika ya 90+1 mwamba wa juu katikati baada ya jitihada za kuwatoka mabeki wa AS FAR Rabat.
Khamis Mcha naye alimtoka vizuri beki wa pembeni wa AS FAR Rabat dakika ya 52 lakini akapiga nje shuti lake.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Emile Fred wa Shelisheli, aliyesaidiwa na nduguze Steve Maire na Jean Ernesta pembeni, kipindi cha kwanza Azam walionekana kucheza kwa tahadhari zaidi na kufanya mashambulizi machache.
Lakini kipindi cha pili, walifunguka na kuanza kushambulia moja kwa moja jambo ambalo liliweka kwenye misukosuko lango la AS FAR Rabat kwa muda mrefu hadi wachezaji wa timu hiyo kuanza kufanya hila za kupoteza muda ili kupunguza kasi ya wenyeji.
John Raphael Bocco ‘Adebayor’ naye alilitia misukosuko mara kadhaa lango la wageni kila ilipoingizwa mipira ya juu kutokea pembeni hususan kona japokuwa alikuwa chini ya ulinzi mkali leo.
Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo/Luckson Kakolaki dk7, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno na Kahmis Mcha ‘Vialli’/Mwaikimba dk78.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Mustafa Mrani, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Yassine El Kordy, Abdelrahim Achchakir/Mostafa El yousfi dk74, Salaheddine Said, Mohamed El Bakkali, Salaheddine Aqqal/Souffiane Alloudi dk80, Mustafa Allaoui na Hicham El Fathi/Youssef Anouar dk69.

Subscribe to:
Posts (Atom)