Showing posts with label MAZINGIRA. Show all posts
Showing posts with label MAZINGIRA. Show all posts

Thursday, November 29, 2012

MATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI.

Katika harakati za kuhifadhi mazingira tunatakiwa kutumia kanuni ya 3R (Reduce,Reuse and Recycle).Hii imeonekana kutumika ipasavyo katika Manispaa ya Dodoma upande wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA).

Kuna gari ambalo lilinunuliwa mwaka 1954 lakini mpaka sasa linafanya kazi katika kituo cha kuzalisha maji cha Mzakwe ambacho ndo chanzo kikuu cha maji kwa mji wa Dodoma.
Nawapongeza sana Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Dododma kwa kuweza kulitunza gari hili na kulifanya kumbukumbu.
Mamlaka zingine nchini ziige mfano wa Mamlaka ya majisafi Dododma ili kuweza kutunza rasilimali tulizonazo.

Wednesday, November 28, 2012

UZURI WA MBEGA UMEMPONZA,ANAWINDWA KWA UDI NA UVUMBA

MBEGA (COLOBUS MONKEY).
 Mbega ni kima wa nusufamilia Colobinae katika familia Cercopithecidae. Wanatokea Afrika na Asia. Spishi nyingi huishi mitini lakini spishi nyingine huishi savana zenye miti na hata mijini. Vidole gumba vya spishi za Afrika vimekuwa vigutu pengine ili kurahisisha kwenda katika miti. Mbega hula majani, maua na matunda, pengine wadudu na wanyama wadogo.
Bega wanapatikana hata katika safu za milima ya uluguru, lakini wanauwawa sana na wakazi wanaoishi karibu na safu za milima hii.



Domeni:
Himaya:
Animalia (Wanyama)
Faila:
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli:
Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda:
Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Nusuoda:
Haplorrhini (Wanyama wanaofanana zaidi na kima)
Oda ya chini:
Simiiformes (Wanyama kama kima)
Oda ndogo:
Catarrhini (Kima wa Dunia ya Kale)
Familia ya juu:
Familia:
Cercopithecidae (Wanyama walio na mnasaba na kima)
Nusufamilia:
Colobinae (Mbega)
Jenasi:
Nasalis E. Geoffroy, 1812
Piliocolobus Rochebrune, 1877
Presbytis Eschscholtz, 1821
Procolobus Rochebrune, 1877
Pygathrix E. Geoffroy, 1812
Rhinopithecus Milne-Edwards, 1872
Semnopithecus Desmarest, 1822
Simias Miller, 1903
Trachypithecus Reichenbach, 1862








Kuna spishi nyingi za Mbega na hapa ni baadhi ya spishi hizo:-

Spishi za Afrika

Spishi za Asia

Tuesday, November 27, 2012

MAAJABU YA KIDUNIA YANAYOTEKETEZWA.

MAAJABU YA KIDUNIA YANAYOTEKETEZWA.

ULUGURU BUSH-SHRIKE – Ndege anayepatikana Milima ya Uluguru pekee Duniani
Ndege huyu ni ndege ajulikanaye kwa jina la kitaalamu kama Malaconotus alius mwenye ukubwa wa sm 22- 24 ambaye hupatikana katika safu za milima ya Uluguru Tanzania. Mwaka 1999-2000, sensa ilikadiria kuwepo jumla ya jozi 1,200 sawa na ndege 2,400 (Burgess et al. 2001); tafiti nyingine za mwaka 2006 and 2007 zote zilionesha kuwa idadi ya ndege hawa haikubadilika (J. John in litt. 2007).

Jambo la kusikitisha, ndege hawa wanauwawa na wanazidi kupungua idadi yake kutokana na uchafuzi wa mazingira unaoendelea katika safu za milima hii ya Uluguru kwa kuchoma moto ovyo.
Wananchi wote wanaoishi karibu na safu hizi za milima ya Uluguru washirikiane katika kuhifadhi mazingira na kuwalinda hawa ndege adimu duniani ili tuweze kukuza uchumi wetu na kupata fedha za kigeni kupitia utalii.

Monday, November 26, 2012

KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO



KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO 
Ni mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuangamiza kunguru weusi katika mikoa ya Pwani.
Hawa ndege ni wasumbufu sana hasa upande wa jikoni kiasi kwamba ukizubaa tu chakula unachopika mnakigawana.
 




 Nimefurahi kuona tangazo la serilaki la kuwaangamiza hawa kunguru weusi Mjini Morogoro,naona tutapumua wakazi wa Morogoro.
 


 Na tangazo la serikali ni hili hapa.

KUNGURU WEUSI KUANGAMIZWA MOROGORO


Wizara ya Maliasili na Utalii itaendesha zoezi la kuwaangamiza Kunguru Weusi katika Manispaa ya Morogoro kuanzia tarehe 16 Novemba hadi 15 Desemba 2012.
Kunguru weusi watauwawa kwa kutumia sumu tulivu aina ya DRC 1339 ambayo haina madhara makubwa kwa binadamu. Hata hivyo tahadhari inatolewa kuwa watoto wasichezee mizoga ya kunguru iliyoanguka barabarani na mitaani.
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kikosi kazi kinachoendesha zoezi hilo kwa kutoa taarifa kuhusu maeneo yenye idadi kubwa ya Kunguru weusi. Aidha, taarifa zitolewe endapo mizoga ya kunguru itaonekana katika makazi ya watu na barabarani.
Lengo la operesheni hii ni kupunguza idadi ya kunguru weusi ambao wanasababisha kero na adha kwa wananchi katika makazi yao. Pia kunguru hao wamekuwa wakiua viumbe wa asili wakiwemo ndege pamoja na kueneza vimelea vya magonjwa kama vile kuhara na mdondo kwa kuku.
Zoezi hili ambalo limeshafanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga litaendeshwa Morogoro kwa mara ya mwisho kabla ya kurudi tena Dar es Salaam kukamilisha zoezi katika sehemu ambazo zitakuwa na kunguru weusi waliosalia.
Kuanzia mwezi Julai 2010 hadi Oktoba 2012 Jumla ya kunguru weusi 856,831 wameshauawa kwa kutumia sumu hiyo ya DRC 1339 na mitego katika Jiji la Dar es salaam, Pwani na Tanga.
Katika Manispaa ya Morogoro taarifa kuhusu Kunguru Weusi zitolewe katika ofisi za Maliasili, pamoja na kupiga simu kwa: Meneja mradi – 0754498957 au 0716129120 na Mtaalamu wa sumu – 0757 – 585358.              
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
16 Novemba 2012
Simu: 0784 468047

Monday, November 19, 2012

UTUNZAJI WA MAZINGIRA MVOMERO.

Sehemu ya Mgeta inavyoonekana kwa mbali.

Kikundi cha ngoma aina ya mdundiko kikitumbuiza katika harusi ya Bw na Bibi Samsoni Mgeta.

Kituo cha afya kilicho makao makuu ya tarafa ya Mgeta- Mvomero

Kijana Mpeka akiwa anacheza Pool table eneo la Mgeta.

Pool table lililotengenezwa kwa vifaa rahisi.

Mama Kibena akiwa anatafakari kabla ya kwenda kutoa zawadi kwa maharusi Bw na Bibi Samsoni Visomolo Mgeta.

Mbuzi wakiwa wamefungwa makopo midomoni ili wasiharibu mifugo ya wakulima.

Mzee Mkude akiwa anafurahi siku ya harusi ya Bw.Samsoni eneo la Visomolo- Mgeta.
UTUNZAJI WA MAZINGIRA MVOMERO.
Ni tarafa ya Mgeta Wilaya ya Mvomero kijiji/sehemu inayojulikana kwa jina la Visomolo ambako mazingira yamehifadhiwa vizuri kiasi kwamba maji yanatiririka hata kipindi cha kiangazi.Katika kuhakikisha kuwa hata mifugo haiaribu mazao ya wakulima mbuzi na ng'ombe wamefungwa midomo yao kwa makopo mpaka watakapofika sehemu wanakochungiwa.
Hata hivyo,ili kupunguza ukataji wa miti ovyo,mchezo wa pool table unachezwa kwa kutengeneza meza hizo kwa vifaa rahisi tofauti na mbao.

Friday, November 16, 2012

HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.





HALI YA HEWA MANISPAA YA MOROGORO.
Tarehe 15.11.2012 mnamo saa 10 jioni hali ya hewa ya Manispaa ya Morogoro ilibadirika ambapo kulitokea upepo mkali uliotimua vumbi kiasi cha kuufunika mji mzima wa Morogoro na kuwa vumbi tupu.
Hali hii imekuwa ya kawaida hasa wakati wa jua kali kutokea upepo mkali kama huu.Ukali wa upepo huu ulisababisha watu kushindwa kutembea na magari yaliyokuwa barabarani yalitembea yakiwa yamewasha taa ili kuepuka ajali.
Hata hivyo,upepo huu kidogo ulikuja na neema kwani mvua kidogo iliweza kunyesha maeneo mengi ya mji wa Morogoro.

Thursday, November 8, 2012

3R ENVIRONMENTAL MANAGEMENT.

3R ENVIRONMENTAL MANAGEMENT.
katika kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanakuwa safi na salama na kupunguza milipuko ya magonjwa tunatakiwa tutumie" 3R principal" Maana yake ni Reduce,Reuse na Recycle.
Njia hii ikitumika tutajikuta mazingira yetu yanakuwa yakuvutia.Hii inazihirishwa na kama wakazi wa Manispaa ya Morogoro Msamvu walivyokutwa wamekusanya taka ngumu na kuzifungasha vizuri zikisubiri usafiri zisafirishwe kwenda kiwandani.

Tuesday, November 6, 2012

USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO.

USAFI WA MAZINGIRA MOROGORO.
Katika kuhakikisha kuwa mji wa Morogoro unakuwa safi Manispaa ya Morogoro inamiliki magari ya kunyonyea majitaka mawili na magari ya watu binafsi yako zaidi ya manne.
Magari haya hutumika kuwanyonyea wakazi wa Morogoro majitaka yakiwa yamejaa kwenye soak away pits.Majitaka hayo yakishanyonywa hutupwa katika mabwawa ya majitaka yaliyoko Mafisa yanayomilikiwa na MORUWASA ili kusiwepo na uchafuzi wa mazingira.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...