Showing posts with label JAMII YETU. Show all posts
Showing posts with label JAMII YETU. Show all posts

Monday, November 3, 2014

Jaji Mstaafu Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba

Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.

Monday, October 27, 2014

TATIZO LA MAJIKWA MJI WA MPANDA LATATULIWA, NI CHANZO CHA MAJI IKORONGO.

Mhandisi Happiness Magalula, Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma (mwenye sweta la blue) akitaka ufafanuzi wa miundombinu ya kuwezesha maji kuwafikia wananchi kutoka katika chanzo hicho. Bomba la inchi kumi limetandazwa kutoka kwenye chanzo hicho mpaka mjini ambako kuna tanki kubwa la maji yanayosambazwa katika mji wa Mpanda na vitongoji vyake

Na Mwandishi wetu, Katavi
Chanzo cha maji cha chemichemi ya Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini, mkoani Katavi. Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa asili unaolinda maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Katavi Magdalena Mkeremi anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi.
Chanzo hiki kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.
Mradi wa maji wa Mji wa Mpanda ni wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote bali maji husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).
Bomba kubwa la maji la inchi kumi limelazwa kutoka kwenye chanzo na kupelekwa Kazima kwenye tanki kubwa la ujazo wa lita milioni moja ambalo limejengwa eneo la kilometa 13 kutoka kwenye chanzo cha maji.  Vile vile  maji kutoka kwenye tanki hilo na kwenda mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko hivyo, kurahisisha gharama zake.

Friday, October 24, 2014

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda wakamilika

Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Na Mwandishi wetu, Mpanda
Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.
Aliiambia timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.
Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.
Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.

Monday, October 20, 2014

UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.

Wednesday, September 10, 2014

Mkutano wa Maafisa Mipango kufanyika Oktoba, 2014.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.

Friday, August 1, 2014

MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) ATEMBELEA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kulia) akibadilishana uzoefu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kushoto) wakati alipotembelea na kukagua Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Na Saidi Mkabakuli
Katika kutekeleza mkakati wa kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vitengo vya mawasiliano serikalini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene leo ametembelea Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pia kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango.
Akiwa katika ziara hiyo, Bw. Mwambene ambaye ndiye Msimamizi Mkuu masuala ya Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Serikali amesema kuwa vitengo vya mawasiliano serikali vina jukumu kubwa ya kuuelimisha umma wa Watanzania juu ya masuala mbalimbali yanayojiri kwenye ofisi zao.

Thursday, July 17, 2014

KAULI YA ZITTO KABWE JUU YA MKATABA WA GESI WA STATOIL NA TANZANIA.

Swali kwa TPDC: Kwanini Makubaliano ni tofauti na Mkataba Elekezi (Model PSA)?
Baada ya kuvuja kwa Mkataba wa kutafuta na kuzalisha Gesi Asilia (PSA) kati ya Serikali kupitia TPDC na Kampuni ya Norway ya StatOil na baada ya baadhi ya wachambuzi kuhoji kuhusu mkataba huo, Shirika la TPDC limetoa maelezo yake. Sio mara moja, sasa ni mara ya tatu. Kimsingi TPDC wanasema wachambuzi waliochambua nyongeza hiyo ya Mkataba hawana uelewa wa mambo haya na wanaleta siasa. Nadhani ni muhimu TPDC wakajikita katika kueleza kwa lugha ambayo wananchi wa kawaida wataelewa badala ya kusingizia uelewa wa watu katika masuala haya. Wizara ya Nishati na Madini haina uelewa wa pekee wa masuala ya Mafuta na Gesi kama wanavyotaka umma uamini. Kuna watanzania wengi tu wenye kufuatilia mambo haya na wenye uwezo mpana hasa katika masuala ya kodi katika tasnia hii. Ni wajibu wa TPDC kutoa maelezo yasiyo changanya wananchi na bora zaidi waweke mikataba hii ya Gesi na Mafuta wazi. Maelezo yaliyotolewa na TPDC mpaka sasa hayaeleweki na yana lengo la kuwachanganya wananchi kama sio kuwaongopea.
Swali la Msingi

Tuesday, July 1, 2014

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA CHUMA LIGANGA MKOANI NJOMBE.

Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia), ambae ni Makamu Afisa Muendeshaji Mkuu wa Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili  ni eneo ambalo kiwanda cha chuma chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka kushoto, wengine ni Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama - NDC , Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi - Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu Meneja Utawala - TCIMRL, Bi. Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anaeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E. Mkucha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.

Wednesday, June 11, 2014

TAARIFA KWA UMMA - KUTOKA UTUMISHI.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa tahadhari kwa waombaji wote wa nafasi za kazi kupitia chombo hiki kuwa kumezuka kundi la watu wanaojifanya ni watumishi wa Sekretarieti ya Ajira ambao kwa makusudi wamekuwa wakiwapigia simu kwa lengo la kuwalaghai baadhi ya waombaji wa nafasi za kazi Serikali wakidai wapewe fedha  ili waweze kuwasaidia kupata kazi Serikalini kwa urahisi  mara baada ya kufanya usaili.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amefikia hatua ya kutoa tamko hili kutokana na baadhi ya waombaji wa nafasi za kazi Serikalini kukumbwa na kadhia hiyo na kutoa taarifa. Amesema Ofisi yake haina utaratibu wa kuwapigia simu waombaji wa fursa za ajira Serikalini na kuwadai fedha ili kuweza kuwapatia nafasi ya ajira. Hivyo, endapo kuna msailiwa yeyote atakayepigiwa simu ajue hao watu ni matapeli na ni vyema akawapuuza kw akutokuwapa ushirikiano na badala yake kuwaripoti katika vyombo vya dola ili waweze kuwachukulia hatua stahiki.

Monday, May 19, 2014

VODACOM WATOA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBEYA.

Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga(kulia)akipokea msaada wa vyandarua kupitia chama cha Msalaba Mwekundu”Redcross”kwa niaba ya wahanga wa mafuriko wa wilaya hiyo toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania nyanda za juu kusini Bw.Macfyden Minja,anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation,Yessaya Mwakifulefule. Jumla ya shilingi Milioni 10 zimetumika kwa misaada mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.

Monday, May 5, 2014

Watu wenye ulemavu wa ngozi waitaka serikali kuwachulia hatua kali watuhumiwa wa mauaji na ukataji viungo.


Watu wenye ulemavu wa ngozi wameitaka serikali kuhakikisha inawachulia hatua kali za kisheria watuhumiwa wanaobainika kuhusika na mauaji na ukataji viungo vya albino ili kukomesha vitendo hivyo huku wakitaka huduma za afya zitolewe bure kwao ili kupunguza idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na saratani ya ngozi.
Hayo yamo katika risala yao waliyoisoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya tisa ya siku ya albino duniani yaliyofanyika jijini dar es salaam ambapo wamesema mbali na tatizo la mauaji na ukatwaji wa viungo vya albino bado wanakabiliwa na changamoto ya saratani ya ngozi ambapo asilimia 80 ya albino hufia majumbani kwa kukosa huduma ya matibabu
Katika hotuba ya rais Jakaya Kikwete iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk Seif Rashid amesema serikali itaendelea kusimamia sera kikamilifu ambapo kwa sasa inafanya utaratibu wa kusambaza mafuta maalum kwa ajili ya albino katika vituo vya afya nchi nzima ambayo yatatolewa bure na kuongeza kuwa waraka wa kutoa huduma za afya bure kwa walemavu wa ngozi umeshasambazwa ngazi husika huku akieleza kuwa changamoto kubwa ni tatizo la imani za kishirikina ambalo linahitaji mapambano ya watu wote
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo mabalozi wanaoziwakisha nchi zao hapa nchini ambapo pia mmoja wa albino aliyenusurika kifo baada ya kukatwa mikono yake yote amepata fursa ya kutoa ushuhuda huku akiiomba serikali kuchukuwa hatua za makusudi juu ya watuhumiwa hao ambapo amedai kuwa aliyemfanyia kitendo hicho kwa sasa yuko huru wakati yeye anaishi kwenye kambi kama mkimbizi

Chanzo: ITV

Wednesday, April 16, 2014

WATU 25 WATHIBITISHWA KUFA KWA MAFURIKO DAR.


Watu 25 wamethibitika kufa mkoani Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia Ijumaa hadi Jumapili wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadik amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo akisema watu wengine 14 wanadaiwa kufa, lakini hawajathibitishwa na polisi.
Taarifa kutoka wilaya ya Temeke imesema watu saba wamethibitishwa kufa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha.Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam wenye wilaya tatu, amesema watu 11 wamekufa katika wilaya ya Ilala, huku wengine wawili hawajaonekana mpaka sasa.
Pia kuna taarifa za watu 21 kufariki dunia katika wilaya ya Kinondoni, japo hawajathibitishwa.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik amesema miundombinu ya barabara na madaraja imeanza kurejeshwa baada ya kuharibiwa na mafuriko na kusababisha mkoa wa Dar es Salaam kukosa mawasiliano ya ndani na pia kukosa mawasiliano na mikoa jirani.


Chanzo: BBC

Tuesday, April 15, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA HATI YA MUUNGANO.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni (picha na Freddy Maro)

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS 

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE, 
P.O. BOX 9120, 
DAR ES SALAAM.
Tanzania. 
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425 




TAMKO LA KATIBU MKUU KIONGOZI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HATI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR IKULU, DAR ES SALAAM, TAREHE 14 APRILI, 2014
______________________________ ____________________ 


Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu. 

Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union). 


Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...