Tuesday, July 1, 2014

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA CHUMA LIGANGA MKOANI NJOMBE.

Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia), ambae ni Makamu Afisa Muendeshaji Mkuu wa Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili  ni eneo ambalo kiwanda cha chuma chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka kushoto, wengine ni Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama - NDC , Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi - Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu Meneja Utawala - TCIMRL, Bi. Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anaeshughulika na Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E. Mkucha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.

Kilima  chenye madini Ya chuma, ambapo  shughuli ya uchimbaji wa chuma unategemea kuanza kutekelezwa. Uzalishaji wa chuma unatarajiwa kuanza mwaka 2016.


Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika eneo ambalo uchimbaji wa chuma utatekelezwa. Pamoja nao ni Viongozi kutoka National Development Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources Ltd. Nyuma ni kilima ambacho kimejaa utajiri wa mawe yenye madini ya chuma ambapo jiwe linakadiriwa kuwa na chuma kwa 52%.

Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), National Development Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMR) wakiwa pamoja na viongozi wa kijiji cha Mundindi ambapo ni eneo ambalo Mradi wa Uchimbaji wa Chuma utatekelezwa. Viongozi hawa pamoja na wanakijiji wameonyesha ushirikiano mzuri na mwekezaji katika kufanikisha utekelezaji wa mradi.

Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd kuhusu Iron Ore Samples zilizopatikana wakati wa utafiti kuhusu wingi na ubora wa chuma kitakachopatikana katika eneo la Liganga.

Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Dkt. Philip I. Mpango (aliyesimama) akiongea na Viongozi wa Kijiji cha Mundindi pamoja na viongozi na wataalam wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resorces Ltd.


Picha na: Thomas Nyindo.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...