Monday, October 20, 2014

UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.



Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya  Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.  Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC)

Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma  –Sumbawanga.  


No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...