Monday, May 5, 2014

Watu wenye ulemavu wa ngozi waitaka serikali kuwachulia hatua kali watuhumiwa wa mauaji na ukataji viungo.


Watu wenye ulemavu wa ngozi wameitaka serikali kuhakikisha inawachulia hatua kali za kisheria watuhumiwa wanaobainika kuhusika na mauaji na ukataji viungo vya albino ili kukomesha vitendo hivyo huku wakitaka huduma za afya zitolewe bure kwao ili kupunguza idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na saratani ya ngozi.
Hayo yamo katika risala yao waliyoisoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya tisa ya siku ya albino duniani yaliyofanyika jijini dar es salaam ambapo wamesema mbali na tatizo la mauaji na ukatwaji wa viungo vya albino bado wanakabiliwa na changamoto ya saratani ya ngozi ambapo asilimia 80 ya albino hufia majumbani kwa kukosa huduma ya matibabu
Katika hotuba ya rais Jakaya Kikwete iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk Seif Rashid amesema serikali itaendelea kusimamia sera kikamilifu ambapo kwa sasa inafanya utaratibu wa kusambaza mafuta maalum kwa ajili ya albino katika vituo vya afya nchi nzima ambayo yatatolewa bure na kuongeza kuwa waraka wa kutoa huduma za afya bure kwa walemavu wa ngozi umeshasambazwa ngazi husika huku akieleza kuwa changamoto kubwa ni tatizo la imani za kishirikina ambalo linahitaji mapambano ya watu wote
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo mabalozi wanaoziwakisha nchi zao hapa nchini ambapo pia mmoja wa albino aliyenusurika kifo baada ya kukatwa mikono yake yote amepata fursa ya kutoa ushuhuda huku akiiomba serikali kuchukuwa hatua za makusudi juu ya watuhumiwa hao ambapo amedai kuwa aliyemfanyia kitendo hicho kwa sasa yuko huru wakati yeye anaishi kwenye kambi kama mkimbizi

Chanzo: ITV

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...