|
Mtafiti mkuu wa mradi Profesa Jamidu Katima akisaini kitabu cha wageni wakati wa utambulisho wa mradi. |
Manispaa ya Morogoro imepata bahati ya kujengewa mradi wa uondoshaji wa majitaka na uhifadhi wa mazingira unaojengwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha Uhandisi (COET) unaofadhiliwa na COSTECH ambao ni mradi wenye thamani ya zaidi ya Milioni 200 unaojengwa Mafisa katika mabwawa ya majitaka ya MORUWASA.
|
Bwawa litakalo kuwa linatumika kutibu majitaka. |
Mradi huo ujulikanao kama Constructed wetlands and fish ponds.Katika mradi huo ambao malengo yake ni utafiti juu ya matumizi ya majitaka baada ya kutibiwa na kujenga mabwawa ambayo ni ya bei nafuu.
|
Bwawa la kufugia samaki katika mradi huu. |
Katika mradi huo utahusisha ujenzi wa mabwawa ya samaki na kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kuthibitisha kama majitaka hayo baada ya kutibiwa yanaweza kutumika kwa ufugaji wa samaki na umwagiliaji.
|
Utafiti juu ya kilimo gani kitafaa kulimia kutumia maji hayo,hapa ni Mpunga,nyanya na Chinese. |
Akiongelea juu ya baadhi ya faida za mradi huo ,mtafiti mkuu wa mradi huo profesa Jamidu Katima alisema kuwa ni gharama ndogo za ujenzi,hupunguza adha ya harufu mbaya,maji yake yanaweza kutumika katika kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment