Papa Jorge Mario Bergoglio akisalimiana na Papa aliyejiuzulu. |
Hatimaye ile kazi ya kumchagua papa mrithi wa Papa Benedict XVI aliyejiuzulu mwezi Februari imekamilika baada ya Kadinali Jorge Mario Bergoglio kuchaguliwa na anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa
Papa na mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka kwenye dohani
katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku
ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne
kwa siku.
Maelfu ya watu kutoka
sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa
Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali
Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea
ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa
No comments:
Post a Comment