Akizungumza
na waumini wa Kanisa hilo Jumapili asubuhi, Machi 17, 2013 kabla
ya kuendesha harambee hiyo, Waziri Mkuu aliusifu uongozi wa Kanisa
Katoliki la Magomeni kwa kuamua kufanya upanuzi wa kanisa hilo ili
liweze kuhudumia waumini wengi zaidi.
“Nia yao ni nzuri sana na wameona mbali mapema. Magomeni
hii ya leo si ya wakati ule, na wala haitakuwa hivi katika miaka
mingine 50 ijayo. Zamani usingeweza kuona hata ghorofa moja hapa
Magomeni lakini sasa hivi maghorofa hayahesabiki,” alisema.
Aliwasisitiza waumini hao kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana kwa sababu hakuna sadaka ambayo ni ndogo. “Hakuna
sadaka iliyo ndogo mbele ya Mungu, kikubwa ni dhamira tu. Kanisa ni
letu na litajengwa na sisi waumini ili mradi kila mmoja wetu aseme Kansa
hili nitalijenga,” alisisitiza.
Mapema
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini hao, Baba Paroko wa
kanisa hilo, Padri Sixfrious Rwechungura alisema wameanza kazi ya
ukarabati tangu Agosti 15, 2011 na kwamba hadi sasa wamekwishakusanya
sh. milioni 350 iliyotokana na nguvu za waumini wenyewe bila msaada wa
kutoka nje.
Alisema
wanahitaji kiasi cha sh. milioni 300 ili kukamilisha kazi hiyo ambayo
inapaswa kukamilika katika miaka miwili ijayo ili iendane na maadhimisho
ya miaka 50 ya kanisa hilo.
Katika
harambee hiyo, Waziri Mkuu na mkewe Mama Tunu Pinda waliahidi kuchangia
sh. Milioni 10 na kutoa sh. Milioni mbili za kianzio. Pia aliendesha
mnada wa mbuzi aliyenunuliwa kwa sh. 600,000/- na mkoba ulionunuliwa kwa
sh. 150,000/-.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment