Alisema kitendo hicho kinaweza kukwamisha malengo
ya milenia na yale ya itifaki ya jinsia na maendeleo katika nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) ya kuwa na uwakilishi wa
asilimia 50 ya wanawake bungeni.
Naibu waziri huyo alisema kama nafasi hizo
zitatolewa, kuna ulazima wa katiba kutamka wazi namna ambavyo itahakisha
kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi katika ngazi zote za serikali.
Alitolea mfano katiba ya Kenya ambayo inaeleza bayana namna viongozi
wanawake wanavyopatikana katika nchi hiyo.
Alisema hayo katika kongamano la waandishi wa
habari na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayojihusisha na
masuala ya kijinsia, jijini Dar es Salaam jana.
Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kutathimi itifaki ya malengo 28 ya kijinsia ya Sadc ifikapo 2015.
Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kutathimi itifaki ya malengo 28 ya kijinsia ya Sadc ifikapo 2015.
Naibu waziri huyo aliwataka waandishi wa habari na
wanaharakati, kuhakikisha kuwa masuala ya ujinsia yanafafanuliwa kwa
kiasi kikubwa katika rasimu ya Katiba Mpya inayotarajiwa kuwasilishwa
juni mwaka huu na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba.
Pia aliwataka waandishi kutumia wanawake kama
vyanzo vya habari kwa sababu takwimu zinaonyesha ni asilimia 21 tu
wanawake ndio wanatoa sauti katika vyombo mbalimbali vya habari hapa
nchini.
Habari hii ni kwa hisani ya Mwananchi.
Habari hii ni kwa hisani ya Mwananchi.
No comments:
Post a Comment