Monday, March 4, 2013

NEEMA YA MAJI MOROGORO YAANZA KUONEKANA

Mafundi wakiwa kazini katika jitihada za kutengeneza bomba hilo.
 Ni kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu sasa tangu bomba kubwa lenye kipenyo cha 16" sawa na 400mm lilipopasuka eneo la Msamvu maarufu kama Stendi ya Dodoma kwenye ukuta wa Tanesco tarehe 19.12.2012.
 
Kupasuka kwa bomba hili kulipelekea maeneo karibia yote ya Kihonda kukosa maji jambo ambalo lilipelekea hadi wakazi wa eneo hilo kufikia hatua ya kufunga barabara na kuzuia magari yasipite wiki mbili zilizopita.
 
Katika hali ya kutia moyo na kufurahisha,sasa bomba hilo limeanza kushughurikiwa na kutengenezwa baada ya kupatikana mitambo maalum ya kutoboa barabara kuu ya Dodoma.
 
Kukamilika kwa bomba hilo kutapunguza upungufu wa maji uliokuwa unawakumba wakazi wa maeneo ya Kihonda.
Mafundi na wataalam mbali mbali wakiwa wanapeana mawazo nini cha kufanya.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...