Monday, August 19, 2013

SHEIKH PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGORO,WAKURUGENZI DECI HATIANI.

PONDA MAHAKAMANI MOROGORO:
Sheikh Issa Ponda amefikishwa Mahakamani Mkoani morogoro chini ya ulinzi mkali wa Polisi huku akiwa amesafirishwa kwa Helikopta ya polisi kutoka Jijini Dar.
Akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro amesomewa mashitaka 3 likiwemo la kutaka kuvuruga amani.Mashitaka yote ameyakana na amenyimwa dhamana na kurudishwa rumande.

WAKURUGENZI WA DECI:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani wakurugenzi 4 wa Kampuni ya DECI kwa tuhuma za kuendesha upatu bila leseni huku mmoja aachiwa huru.

Call For Papers UDSM - 50 Years of the Union between Tanganyika and Zanzibar.

EMPLOYMENT OPPORTUNITY EWURA - Director of Corporate Affairs.

MASTERS SCHOLARSHIPS FOR IRRIGATION.

TAMKO LA VODACOM KUHUSU KUKOSEKANA KWA HUDUMA ZA MAWASILANO NCHINI.

 
Wapendwa wateja wetu na jamii kwa ujumla;

Tunaomba radhi kwa dhati kabisa kwa kutoweza kuwapa huduma za mawasiliano za mtandao wa Vodacom kuanzia jioni ya siku ya Ijumaa Agosti 16 mpaka Jumamosi asubuhi Agosti 17, 2013....

Hali hii ilisababishwa na moto uliozuka katika jengo lenye kitovu cha kuendesha (switch) mitambo yetu lililopo Dar es Salaam . Moto huo ulipelekea kuzimika kwa mtambo wetu na kukata huduma zetu zote nchini na hivyo kuwaathiri wateja wetu wa ndani na nje ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla.

Tunatambua na kuelewa usumbufu uliosababishwa na kukosekana kwa huduma zetu, na tunapenda kuwashukuru kwa uvumilivu na uaminifu wenu kwa Vodacom katika kipindi hiki kigumu.

Tutawarejeshea gharama za vifurushi vya bidhaa zetu hususan, muda wa maongezi, SMS na huduma za intaneti , mlivyovinunua siku ya Ijumaa Agosti 16, na ambavyo hamukuweza kuvitumia kikamilifu kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano. Zoezi hili litakamilika Jumatatu Agosti 19, 2013.

Ninaomba niwahakikishie wateja wetu kwamba Vodacom ina dhamira ya dhati kabisa ya kuendelea kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu hapa nchini.

Aidha, ninaomba pia kuwashukuru wafanyakazi na washirika wetu wote waliofanya kazi bila kuchoka ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinarejea katika hali yake ya kawaida kufikia asubuhi ya Agosti 17, 2013. Kwa hakika jitihada zao, kujituma kwao na utendaji kazi wao kwa bidii, vilitoa mchango mkubwa sana katika zoezi hili.

Kwa mara nyingine ninaomba niwatake radhi kwa usumbufu na kuwashukuru kwa uvumilivu wenu.

Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji

Commonwealth Academic Fellowships for Mid-Career Academics in UK, 2014.

Each year, UK Department for International Development (DFID) funds academic fellowships for mid-career academics from developing Commonwealth countries. These fellowships enable fellows to spend three months to network and update knowledge and skills related to their academic subject and responsibilities at any approved UK university or higher education institution. The CSC also invites alumni who held Commonwealth Scholarships for PhD to apply directly to the CSC for a Commonwealth Academic Fellowship. All eligible alumni will be sent a letter with details of how to apply. All applications must be made through your nominating university/university body in applicants’ home country. The deadline for applications is 3 December 2013.
Study Subject(s): The purpose of the Academic Fellowships is to provide an opportunity for Fellows to network and update knowledge and skills related to their academic subject and responsibilities.
Course Level: The Fellowships are awarded for mid-career academics to spend three months at any approved UK university or higher education institution.
Scholarship Provider: UK Department for International Development (DFID)
Scholarship can be taken at: UK
Eligibility: To apply for a Commonwealth Academic Fellowship, candidates should:
-Be Commonwealth citizens, refugees, or British protected persons
-Be permanently resident in a developing Commonwealth country
-Be available to commence their Fellowship in the United Kingdom on 1 September 2014. Any other start date will only be permitted in exceptional circumstances
-Have been employed for at least five years as an academic staff member of a university in a developing Commonwealth country
-Be in the employment of the nominating university
-Hold a doctorate
-For awards to enhance clinical skills in the fields of medicine and dentistry, have qualified as a doctor or dentist before 1 October 2004.

MTAZAMO WA ZITTO KABWE JUU YA RASIMU YA KATIBA.

Rasimu ya Katiba ibara ya 215 inasema vyanzo vya mapato ya Muungano, kikubwa, ni ushuru wa bidhaa. Wajumbe wa Tume wanasema walifanya hesabu sawa sawa na fedha hizo zitatosha kuendesha Muungano. Lazima aliyewafanyia hayo mahesabu ama aliwapotosha au hajui.
Mwaka 2012/13 Ushuru wa bidhaa (ndani na nje) uliingiza mapato ya tshs 1.5 trilioni tu. Fedha hii inatosha kuendesha Wizara ya Ulinzi peke yake!
Haitoshi hata kuhudumia Deni la Taifa (ambalo mkopaji ni Jamhuri ya Muungano). Huu muungano utaendeshwaje?
Rasimu inapaswa kufanyiwa kazi sana. Nahisi Tume ilikuwa na haraka na haikutafakari kwa kina baadhi ya masuala.
Mambo ya Muungano inabidi yaangaliwe upya kabisa ili kuboresha mfumo wa Serikali 3 unaopendekezwa ikiwemo kuzuia Washirika wa Muungano kuunda vikosi vyao vya kijeshi, Ulinzi na usalama. Suala la biashara ya kimataifa na hata suala la usimamizi wa maliasili (regulatory function).
Source:Zitto Social media.

Sunday, August 18, 2013

Djotodia aapishwa kama rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kiongozi wa zamani wa waasi ambaye alifanya mapinduzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia ameapishwa kama rais.
Bwana Djotodia ameahidi kuandaa uchaguzi kufikia mwanzo wa mwaka ujao. Tangu achukue uongozi mwezi Machi kupitia kikundi cha waasi wa Seleka nchi hiyo imetajwa kutumbukia zaidi katika umaskini na utovu wa sheria.
Shirika la Umoja wa mataifa linakadiria kuwa zaidi ya thuluthi moja ya raia wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa dharura.
Baraza la uslama la Umoja wa mataifa limeonya kuwa kuongezeka kwa ukatili na uvunjifu wa sheria katika Jamhuri ya Afrika ya Kati inatishia usalama na uthabiti wa eneo lote.
Msemaji wa rais wa zamani Francois Bozize ambaye aling'olewa madarakani na bwana Djotodia amemtaja kiongozi huyo mpya kama 'kibaraka'.
Msemaji huyo Levi Yakete, amenukuliwa katika Redio Ufaransa kusema:
'Bwana Djotodia, ambaye ameingia madarakani kwa njia ambazo sote tunaelewa, ni kibaraka tu wa Chad na Sudan. Aliingia madarakani kupitia njia ambazo hazikubaliki na watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Alipindua utawala wa kisheria na katiba, ambao ulikuwa unaongozwa na Francois Bozize.'

Chanzo : BBC

VIDEO YA YAHAYA - LADY JAY DEE HII HAPA.

WAHAMIAJI HARAMU 8,666 WAREJEA MAKWAO MKOANI KAGERA, CHELSEA 2 - HULL 0.

Kutoka Kagera.
Serikali Mkoani Kagera imesema mpaka sasa wahamiaji haramu wapatao 8,666 wameshaondoka na kurejea nchini kwao ambapo kati yao 500 ni Waganda na silaha zipatazo 43 zimesalimishwa.

Kutoka Uingereza
 Katika Ligi kuu ya Uingereza,Tottenham 1 - Crystal Palace 0
wakati katika mtanange kati ya Chelsea vs Hull City matokeo ni Chelsea 2 - Hull 0

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...