Tuesday, June 25, 2013
UBOMOAJI WA MAJENGO DAR KUANZA LEO.
Wakati zoezi la kubomoa majengo yote yaliyojengwa barabarani likitarajiwa kuanza hii leo,hayo hapo juu ndo mambo yanayotarajiwa kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
TANAPA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KUKABILIANA NA UJANGIRI.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Balozi Khamis Kagasheki ametangaza vita dhidi ya ujangiri. Mh.Kagasheki ameyasema hayo wakati akifungua semina iliyoandaliwa na Tanzania National parks (TANAPA) na Wahariri wa habari nchini iliyofanyika Iringa jana.
"Tunatakiwa kuchukua hatua sasa.Hali inatisha na haivumiliki" alisema wakati akijibu hoja juu ya ujangiri unaofanywa juu ya Tembo ndani ya nchi.
"Tunatakiwa kuchukua hatua sasa.Hali inatisha na haivumiliki" alisema wakati akijibu hoja juu ya ujangiri unaofanywa juu ya Tembo ndani ya nchi.
MKURUGENZI MKUU WA TANAPA ALLAN KIJAZI AKIONGEA KWENYE SEMINA. |
AJARI: BASI LA SUMRY LAUA WATU WAWILI MKOANI DODOMA.
Basi la kampuni ya mabasi ya Sumry limepata ajari na watu 2 wamekufa hapo hapo na wengine 2 kujeruhiwa.Ajari hiyo iliyotokea jana usiku ilihusisha basi la Sumry lililokuwa linatokea Bukoba kuelekea Dar baada ya kugongana na Lori mkoani Dodoma.
Monday, June 24, 2013
Walimu watangaza mgomo rasmi Nchini Kenya.
Chama cha kitaifa cha walimu nchini Kenya,
kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia leo baada ya serikali kukosa
kuwalipa marupurupu yao.Huu ni mgomo wa saba wa walimu tangu mwaka 2007.
Mwnyekiti wa kitaifa wa chama hicho,Wilson Sossion alituhumu serikali kwa kucheza siasa na maswala yanayowahusu walimu kwani wanafahamau masaibu ya walimu na mkataba wa mwaka 1997 uliotoa ahadi ya marupurupu hayo kwa walimu.
Kulingana na makubaliano hayo, serikali inapaswa kuwalipa walimu marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu , kuwlaipia nyumba , matibabu na pesa za usafiri.
"tumedurusu mienendo ya serikali na kugundua kuwa wantumia mtindo wa kugawanya watu. Hilo halitafanya halitafaulu,'' alisema bwana Sossion
"Tumetangza kuwa mgomo wa waalimu unaanza rasmi leo, '' aliongeza bwana Sossion
Sossion pia alisema kuwa tume ya kushughulikia maswala ya walimu, haina mamlaka ya kuwaamuru walimu kutogoma au vinginevyo kwani hilo ni jukumu la Knut.
Katibu mkuu Knut, bwana Nyamu aliseama kuwa chama cha walimu kimeweka bayana matakwa yao waliyokubana na serikali mwaka 1997.
"marupurupu haya yote sharti yalipwe.Tumekwenda kwa wizara ya limu ya kuelezea malalmiko yetu,'' alisema bwana Nyamu.
"tunawaambia walimu kuwa katibu mkuu atawapa maagizo kuhusu watakachofanya wakati wa mgomo huu. Walimu waanze kwa kukabidhi majukumu yao katika shule zao leo.
Nyamu pia aliwataka walimu kuwaondoa watoto wao shuleni kwani walimu hawatakuwepo kuwafundisha.
''Kwa sasa tunaiacha serikali ifanye uamuzi , tutaketi chini na kusubiri,'' alisema Nyamu
''Wanachokitaka walimu ni pesa, na wale wanaomshauri rais wamwambie kuwa lazima walimi wapewe pesa kwani hawatazungumzia kingine ila marupurupu yao,'' alisema Sossion
Source: BBC
Postgraduate Scholarships in UK 2013/2014.
Nottingham Trent University offers International Development Office postgraduate scholarships under International Scholarship, Vietnam Scholarship and Iraq Scholarship categories. To be eligible for a scholarship applicant must be have an offer of a place at NTU. Applicant should be a new international student starting on a new course. Sponsored students are not eligible to apply. The scholarships will be awarded on the basis of academic attainments and the quality of their personal statements. Final application should be submitted till 30th July 2013. All applications received before 30th July will be assessed in August.
Study Subject(s): Scholarships are provided for courses offered by the Nottingham Trent University, UK.
WAMILIKI WA MABASI ARUSHA & KILIMANJARO WASITISHA MGOMO.
Wamiliki wa mabasi Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wamesitisha mgomo wa kubeba abiria uliokuwa uanze leo kupinga magari ya Noah kuruhusiwa kubeba abiria.
Ikumbukwe kwamba kulikuwa na mvutano kati ya wamiliki wa mabasi na serikali juu ya kuruhusu Noah kutoa huduma ya kusafirisha abiria.
Ikumbukwe kwamba kulikuwa na mvutano kati ya wamiliki wa mabasi na serikali juu ya kuruhusu Noah kutoa huduma ya kusafirisha abiria.
WATU 10 WAMEUAWA HOTELINI- PAKISTAN.
Watu 10 wameuawa katika hoteli,kaskazini mwa Pakistan ikiwa pamoja na watalii tisa .
Watu waliokuwa na silaha waliivamia kambi moja ya sehemu hiyo ya Nanga Parbat na kuwaua watalii hao.
Kwa mujibu wa taarifa, waliouawa walikuwa raia wa Ukraine,Urusi na China.
Msaidizi wa watalii,mwenyeji wa sehemu hiyo pia aliuawa.
Marekani pia imethibitisha kwamba raia wake mmoja alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Washambuliaji 15 waliojifanya kuwa ni polisi waliivamia kambi hiyo katika jimbo la Gilgit-Baltistan
Kwa mujibu wa taarifa za mashirika ya habari, Taliban wamedai kuhusika na mashambulio hayo.
Msemaji wao ameeleza kuwa watu hao wameuliwa kulipiza kisasi kifo cha makamu kiongozi wa Taliban ,Wali ur Rehman alieuliwa katika shambulio la mwezi uliopita lililofanywa na ndege ya Marekani inayoruka bila ya rubani.
Source: DW
Subscribe to:
Posts (Atom)