Thursday, June 6, 2013
BREAKING NEWS: KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE.
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwimbaji wa Taarab wa kundi la TOT Khadija Kopa amefiwa na mumewe.Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea blogu hii.
Wednesday, June 5, 2013
KENYA YAFUNGWA 1-0 NA NIGERIA,KATIKA HARAKATI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014
Mchuano wa kufa na kupona umeshuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika
Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa
kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi-Kenya ambapo Nigeria wameshinda 1-0 dhiki ya Harambee Stars ya Kenya.
Goli la Nigeria limefungwa na Musa Ahmed kunako dakika ya 81 ya mchezo huo. Mashabiki wa .
Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda mlango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino, Brian Mandela, David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama, Jamal Mohammed, Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata
.Kikosi cha Eagles:Golikipa ni Enyeama, Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye
Goli la Nigeria limefungwa na Musa Ahmed kunako dakika ya 81 ya mchezo huo. Mashabiki wa .
Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda mlango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino, Brian Mandela, David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama, Jamal Mohammed, Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata
.Kikosi cha Eagles:Golikipa ni Enyeama, Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye
MAMA MANGWEA HALI TETE WAKATI MWILI WA MAREHEMU UKISUBIRIWA.
Mama mzazi wa
marehemu Albet Mangwea Bi.Denisia Mangwea akiwa kitandani nyumbani kwake
kihonda mazimbu road muda mfupi baada ya kutoka hospital ya mkoa wa Morogoro alikokuwa
amelazwa baada ya kuanguka ghafla baada ya kuelezwa kwamba mwili wa mwanae
ulishindwa kuwasili nchini juzi kama ilivyolipotiwa awali.
Leo blog hii ilifika tena nyumbani kwa mfiwa
huyo kwa lengo la kumjulia hali na kujua hali ya maandalizi ambapo alipohojiwa alidai kwamba bado afya yake
haijatengemaa.
Hata hivyo alisema vyovyote itajkavyo kuwa ni razima ashiriki kikamilifu
ibada na mazishi ya mwane kitinda mimba.
MASTERS SCHOLARSHIPS AT CARDIFF UNIVERSITY IN UK, 2013/14 .
The
School of History, Archaeology and Religion, Cardiff University offers
masters studentships in the field of archaeology, ancient history,
conservation, history, religious studies and theology. Minimum of 2:1 or
equivalent for overseas applicants) in a BA Degree in a relevant
subject. The masters studentships are awarded on the basis of academic
merit. Awards are open to students of any nationality. International
students will be offered an award equivalent to the value of the UK/EU
course fees and will be required to cover the remaining international
fees themselves. The application deadline is 1st July 2013.
Study Subject(s): Studentships are provided in the field of archaeology, ancient history, conservation, history, religious studies and theology.
Study Subject(s): Studentships are provided in the field of archaeology, ancient history, conservation, history, religious studies and theology.
TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAOMBI YA MIKOPO 2013/2014 KWA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU.
1.0 UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi
wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi
mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei,
2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza
kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).
2.0 WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA
Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa
mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za
kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na
Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za
mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na
kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe
kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni
kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu
kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza
kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi
anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.
Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya
kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa
mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango
cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha
ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu,
mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo
hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni
muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo,
kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa
wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014.
3.0 IDADI YA WANAFUNZI WALIOKWISHAOMBA MIKOPO KUFIKIA MEI 30, 2013
Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Na.
|
Waombaji wa mara ya kwanza waliokamilisha kujaza fomu
|
Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji
|
Wanafunzi wanaoendelea na masomo waliojaza fomu na kukamilisha
|
424
|
5320
|
60367
|
4.0 HITIMISHO
Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:
(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.
(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa
wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika
mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga
namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku
za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri
siku ya jumamosi.
(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
RAIS KIKWETE ATUA SINGAPORE KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kasulu mjini Mhe Moses Machali pamoja na wadau wengine wakati akiwasili Singapore. |
Tuesday, June 4, 2013
REMEDIAL PROGRAMME - SAINT AUGUSTIN UNIVERSITY OF TANZANIA.
TANGAZO
Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania kinawatangazia nafasi za kujiunga na Remedial Programme kwa mwaka wa masomo 2013/2014.Kozi hii ni kwaajili ya wale wote ambao alama zao hazifiki kiwango cha 4.5 katika kidato cha sita, ili kuwawezesha kupata elimu ya ziada iwasaidie kuendana na wanafunzi wenzao walio pata alama za 4.5 katika kidato cha sita.
Sifa za Muombaji:
1. Awe amemaliza kidato cha sita.
2. Awe na Principal Points kuanzia 2.5 hadi 4 kwenye masomo mawili ya kidato cha sita (mfano: EE, DE, CE, DD, EEE na masomo mengine kuwa na S).
3. Gharama ni Tshs. 390,000/= (Tuition Fee) kwa miezi 3, malazi (accommodation) ni Tshs. 70,000/=, chakula ni kujitegemea.
4. Wale wote wenye sifa hizo watakao chaguliwa na TCU kuja SAUT watatakiwa kufika chuoni miezi mitatu kabla ya tarehe ya kujiunga chuoni kwaajili ya kuanza masomo ya remedial.
5. Kozi hii itaanza tarehe 3/7/2013.
Fomu zinapatikana ofisi ya Admissions na kwenye tovuti (www.saut.ac.tz). Baada ya kumaliza kujaza fomu zirudishwe ofisi ya Admissions-SAUT. Wahitimu wataruhusiwa kujiunga na vyuo vyote vilivyo chini ya SAUT.
Wote mnakaribishwa.
Admissions Officer
Subscribe to:
Posts (Atom)