Wednesday, June 5, 2013

KENYA YAFUNGWA 1-0 NA NIGERIA,KATIKA HARAKATI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014

Mchuano wa kufa na kupona umeshuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi-Kenya ambapo Nigeria wameshinda 1-0 dhiki ya Harambee Stars ya Kenya.
Goli la Nigeria limefungwa na Musa Ahmed kunako dakika ya 81 ya mchezo huo. Mashabiki wa .

Kikosi cha Harambe Stars: Mlinda mlango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino, Brian Mandela, David Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama, Jamal Mohammed, Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis Kahata
 .Kikosi cha Eagles:Golikipa ni Enyeama, Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa, Ideye

MAMA MANGWEA HALI TETE WAKATI MWILI WA MAREHEMU UKISUBIRIWA.

Mama mzazi wa marehemu Albet Mangwea Bi.Denisia Mangwea akiwa kitandani nyumbani kwake kihonda mazimbu road muda mfupi baada ya kutoka hospital ya mkoa wa Morogoro alikokuwa amelazwa baada ya kuanguka ghafla baada ya kuelezwa kwamba mwili wa mwanae ulishindwa kuwasili nchini juzi kama ilivyolipotiwa awali.

Leo blog hii ilifika tena nyumbani kwa mfiwa huyo kwa lengo la kumjulia hali na kujua hali ya maandalizi ambapo alipohojiwa alidai kwamba bado afya yake haijatengemaa.

Hata hivyo alisema vyovyote itajkavyo kuwa ni razima ashiriki kikamilifu ibada na mazishi ya mwane kitinda mimba.

 Albaet aliyekufa ghafla nchini Afrika kusini jumanne ya wiki iliyopita.Mwili wa msanii huyo unatarajiwa kuzikwa jirani na kaburi la marehemu baba yake Mzee Keneth Mangwea kwenye makaburi ya Kihonda yaliyopo nje ya kanisa la Mtakatifu Monica kesho Alhamisi.

MASTERS SCHOLARSHIPS AT CARDIFF UNIVERSITY IN UK, 2013/14 .

The School of History, Archaeology and Religion, Cardiff  University offers masters studentships in the field of archaeology, ancient history, conservation, history, religious studies and theology. Minimum of 2:1 or equivalent for overseas applicants) in a BA Degree in a relevant subject. The masters studentships are awarded on the basis of academic merit. Awards are open to students of any nationality. International students will be offered an award equivalent to the value of the UK/EU course fees and will be required to cover the remaining international fees themselves. The application deadline is 1st July 2013.

Study Subject(s): Studentships are provided in the field of archaeology, ancient history, conservation, history, religious studies and theology.
 

TASWIRA YA ZOEZI ZIMA LA KUUAGA MWILI WA MANGWEA DAR LEO.




TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAOMBI YA MIKOPO 2013/2014 KWA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU.

  1.0            UTANGULIZI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013.  Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).

2.0   WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA

Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.
Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).  Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa.  Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014.

3.0       IDADI YA WANAFUNZI WALIOKWISHAOMBA MIKOPO KUFIKIA MEI 30, 2013

Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni   424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Na.
Waombaji wa mara ya kwanza waliokamilisha kujaza fomu
Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji
Wanafunzi wanaoendelea na masomo waliojaza fomu na kukamilisha

424
5320
60367

4.0            HITIMISHO

Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:
(i)                Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.
(ii)              Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi.  Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.
(iii)            Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.

IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

RAIS KIKWETE ATUA SINGAPORE KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Bw. Laurence Bay, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kushoto ni Balozi wa Tanzania India na Singapre Injinia John  Kijazi na mbele yao ni Naibu Mkurugenzi wa Itifaki wa Singapore Bi. Christine Tay.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kasulu mjini Mhe Moses Machali pamoja na wadau wengine wakati akiwasili Singapore.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jijini Singapore jana wakati alipokutana na wafanyabaishara za ujenzi wa nchi hiyo mara tu baada ya kutua kutoka Japan alikokuweko kwa ziara nyingine ya kikazi. Katika mkutano huu  Rais Kikwete aliwakaribisha wafanyabishara hao wa Singapore  Tanzania kuwekeza katika sekta ya nyumba wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Tuesday, June 4, 2013

REMEDIAL PROGRAMME - SAINT AUGUSTIN UNIVERSITY OF TANZANIA.

  
                                                        TANGAZO
Chuo cha Mtakatifu Agustino Tanzania kinawatangazia nafasi za kujiunga na Remedial Programme kwa mwaka wa masomo 2013/2014.Kozi hii ni kwaajili ya wale wote ambao alama zao hazifiki kiwango cha 4.5 katika kidato cha sita, ili kuwawezesha kupata elimu ya ziada iwasaidie kuendana na wanafunzi wenzao walio pata alama za 4.5 katika kidato cha sita.

Sifa za Muombaji:
1. Awe amemaliza kidato cha sita.

2. Awe na Principal Points kuanzia 2.5 hadi 4 kwenye masomo mawili ya kidato cha sita (mfano: EE, DE, CE, DD, EEE na masomo mengine kuwa na S).

3. Gharama ni Tshs. 390,000/= (Tuition Fee) kwa miezi 3, malazi (accommodation) ni Tshs. 70,000/=, chakula ni kujitegemea.

4. Wale wote wenye sifa hizo watakao chaguliwa na TCU kuja SAUT watatakiwa kufika chuoni miezi mitatu kabla ya tarehe ya kujiunga chuoni kwaajili ya kuanza masomo ya remedial.

5. Kozi hii itaanza tarehe 3/7/2013.

Fomu zinapatikana ofisi ya Admissions na kwenye tovuti (www.saut.ac.tz). Baada ya kumaliza kujaza fomu zirudishwe ofisi ya Admissions-SAUT. Wahitimu wataruhusiwa kujiunga na vyuo vyote vilivyo chini ya SAUT.

Wote mnakaribishwa.

Admissions Officer

TAMKO RASMI LA PUSH MOBILE KUHUSU MAUZO YA NYIMBO ZA MANGWEA


HAYA NDIO MAPOKEZI YA MWILI WA MANGEAR JIJINI DAR.











HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE, DAR ES SALAAM

Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,  
Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu, 
Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, 
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, 
Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria, 
Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, 
Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 
Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, 
Viongozi wa Vyama vya Siasa, 
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
Ndugu Wananchi, 
Wageni Waalikwa, 
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana,


UTANGULIZI 

Ndugu Wananchi,

Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.

Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.

Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao 1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya wananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano ya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume, Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.

Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika. Makundi zaidi ya 160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya viongozi wa juu wa Serikali walioko madarakani na waliostaafu. Kwa jumla viongozi 43walitoa maoni.

Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni tuliyopata yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, tulitambua umuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchi yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana. Aidha, baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji. Tulifanya uchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo tumeikamilisha na rasimu imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya kuizindua, ambapo Wananchi watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya Tume, napenda kutaja maeneo machache tu ambayo tunayapendekeza.

2.0. IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA

Ndugu Wananchi,

Katiba yetu ya sasa ina ibara 152. Tume ilifanya jitihada kubwa sana kuandaa rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu ya Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.

3.0. MISINGI MIKUU YA TAIFA

Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na inastahili kubaki kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza misingi mingine mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tume imependekeza Katiba iwe na Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki,

Udugu, Usawa, Umoja, Amani na Mshikamano.

4.0. TUNU ZA TAIFA

Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu,

Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...