Thursday, May 30, 2013

URUSI YAIKABIDHI SYRIA 'ZANA ZA KIVITA'

Syria imepokea ngao za kwanza kutoka kwa Urusi, za kuikinga nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya makombora ya angani. Hii ni kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.
Urusi imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuhami Syria, mara tu baada ya uamuzi wa muungano wa Ulaya wa kuondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha.
Bwana Assad pia anaripotiwa kuambia televisheini yenye uhusiano na kundi la Hezbollah, kuwa sasa kumekucha kwani vita ndio vinaanza kushika kasi.
Awali, kiongozi mmoja wa waasi aliambia BBC kuwa Hezbollah imekuwa ikishambalia Syria.
Generali Selim Idriss, kwenye mahojiano na BBC alisema kuwa zaidi ya wapiganaji 7,000 wa kishia kutoka Lebanon, wanashiriki vita dhidi ya utawala wa Syria mjini Qusair, mji ambao unadhibitiwa na waasi.
Mfumo wa S-300 ni wa hali ya juu ambao unaweza kukinga makombora ya angani na ya sakafuni.
Hatua ya Urusi kuikaibidhi Syria zana kama hizo, inazua wasiwasi zaidi hasa baada ya Syria kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel, msimamo ambao pia umechukuliwa na Urusi.
Wadadisi wanasema kuwa huenda pande zinaojihusisha na mzozo wa Syria zikaanza kutumia makombora kwenye vita hivi.
Pia inahofiwa kuwa mashambulizi ya makombora yanaweza kutishia juhudi za kuandaa mkutano wa amani kuhusu Syria mjini Geneva mwezi Juni.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo sasa yamerejea katika hali nzuri ya kupambana na waasi.

TAARIFA KWA UMMA: TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA.

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA UMMA.
TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha “Novel Coronavirus”.Taarifa hiyo inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013 idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 viliripotiwa
Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huu kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza. Katika bara la Afrika, ugonjwa huu umetokea Tunisia.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho “novel coronavirus (nCoV).”. Dalili kuu za ugonjwa huu ni kushindwa kupumua kwa ghafla, homa kali, kukohoa, na kubanwa na mbavu na hatimaye kupata Nimonia. Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na kuharisha.Vile vile ugonjwa huu unaweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi na hata kusababisha kifo. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu
ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukizi. Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Njia za maambukizo bado hazijajulikana ingawa uwezekano mkubwa wa maambukizo ni kwa kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga chafya) au kwa kugusa majimaji/makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:
Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara. Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani. Aidha watalaamu hawa pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.
Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi vya ugonjwa huu vimetumwa katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana
Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya
Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini. Wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA.
Pia wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
30/05/2013

TAARIFA KWA UMMA: TAHADHARI YA TISHIO LA MLIPUKO WA UGONJWA WA KUPOOZA (POLIO)

TAARIFA KWA UMMA

TAHADHARI LA TISHIO LA MLIPUKO WA UGONJWA WA KUPOOZA (POLIO)
 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepokea taarifa mnamo tarehe 22 Mei 2013 kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni, (WHO) ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (Polio) katika Wilaya ya Fafi nchini Kenya. Mpaka sasa kuna mgonjwa mmoja bila kifo.
 
Ugonjwa wa Polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kama “Polio Virus”. Ugonjwa huu unaathiri misuli na mfumo wa fahamu hivyo kusabisha kupooza kwa viungo hasa miguu na hata kifo. Ulemavu huu ukishajitokeza huwa ni wa kudumu. Waathirika wakuu wa ugonjwa huu ni watoto hasa walio na umri chini ya miaka mitano. Hata hivyo ugonjwa huu unazuilika kwa chanjo ya Polio ambayo ni salama na inatolewa bure na Serikali katika vituo vyote vya huduma ya afya. Mtoto aliyepata chanjo ya Polio anakuwa amekingwa na ugonjwa wa Polio kwa maisha yake yote.
 
Kutokana na taarifa hiyo ya kutoka nchini jirani ya Kenya, baadhi ya mikoa ina uwezekano mkubwa wa kupata maambukizo ya ugonjwa huo kufuatia ushauri wa kitaalam. Aidha, mikoa hii mingine inapakana na nchi jirani ya Kenya na mingine ina mapungufu yaliyopo katika hali ya chanjo ya Polio. Mikoa hii ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mara na Mwanza.
 
 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:
 
·        Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya.
    
·        Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipaka
 
·        Kufuatilia kwa karibu hali ya chanjo mikoani na wilayani hususan ya Polio hususani iliyo katika hatari ya maambukizi
 
·        Kuhamasisha watoto ambao hawajakamlisha ratiba yao ya chanjo hususani ya Polio au ambao hawajapata ya chanjo hii waweze kwenda vituo vya karibu vya afya vya kutolea chanjo
 
Wizara inapenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa Viongozi na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kila mtoto mlengwa anapata chanjo ya Polio. Aidha Wizara inatoa rai kwa wadau wetu, taasisi za dini, taasisi zinazofanya kazi katika jamii na vyombo mbalimbali  kuhamasisha watu wapeleke watoto wao kwenye vituo vya huduma wakapewe chanjo hii muhimu. Chanjo hii ni salama na inatolewa bila malipo.
 
 
Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu mara wanapoona au kupata taarifa ya mtoto yoyote anayepata ulemavu wa ghafla pasipo sababu yoyote. Mtoto huyo apelekwe katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na hatua za haraka.
 
 
 
 
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaaja
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
30/05/2013

Scholarships for High Achieving International Students at RMIT University in Australia, 2013

RMIT university, Australia offers Seventy four international scholarships. These scholarships are awarded to pursue various program at undergraduate and postgraduate level at university in Semester 2 2013 (July intake). Each scholarship worth of  A$3000 will be awarded towards tuition fees. Before applying these scholarships, applicants must apply for admission into one of RMIT program. Applications should be submitted till June 7, 2013.


KINANA NA NAPE WAENDA "BEACH" ZIWA NYASA.

Katibu mkuu wa CCM Kinana na Nape Nnauye wakiwa ziarani mkoani njombe wamekagua ufukwe wa ziwa Nyasa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, Wilayani Ludewa, na kuwambia wananchi wasihofu na maneno Malawi kuhusu ziwa hilo, Serikali ipo imara kuwalinda usiku na mchana.





HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MH. JOSEPH O. MBILINYI (MB)

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA KWA MWAKA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa spika, mwaka jana nilianza hotuba yangu kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki  wa wale wote waliofariki dunia kwa ajali ya mv skagit, mwaka huu naomba nianze hotuba yangu kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa wale waliofariki kwa ajali nyingine ya kizembe ya kuanguka kwa ghorofa la Dar Es Salaam. Aidha, mwaka jana nilianza kwa kutoa pole kwa Mh. Joseph selasini kwa kufiwa na baba yake na mwaka huu nianze pia kwa kutoa pole kwa Mh. mchungaji Israel Natse kwa kufiwa na baba yake mzee Yohana Natse. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake , mahali pema peponi.
Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi wala ushindani kuwa Serikali yoyote makini duniani huweka sera na mifumo thabiti ya kuhakikisha kuwa ajira za kutosha zinatengenezwa, mazingira ya kazi yanaboreshwa na wafanyakazi wanalipwa ujira na mishahara yenye staha, si tu kwaajili ya kuwawezesha kumudu gharama za maisha, bali pia kuwapa morali wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya taifa.
Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza kuwa  Taifa lolote duniani ambalo haliwezi kutengeneza ajira na hivyo kuwafanya vijana wake wengi wenye uwezo wa kuajiriwa kuzurura mitaani, na wale walio vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu ya Serikali kushindwa au kupuuza kugharamia masomo yao; sote tunatambua kuwa Taifa hili  limejaliwa rasilimali nyingi za utalii na madini ya thamani, lenye vyanzo vingi vya kodi na mapato, lakini limegubikwa na migogoro mingi, ya mara kwa mara na isiyokwisha, ya wafanyakazi wanaodai haki na mafao yao halali, huku wakiishia kunyamazishwa kwa kauli laini zenye matumaini hewa; Kwa namna yoyote ile taifa hilo, ni kielelezo cha nchi inayoongozwa na Serikali isiyo na vipaumbele, yenye viongozi wasiojali na wanaotekeleza sera wasizozijua au zilizoshindwa.
2.0 MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
Mheshimiwa Spika, katika Maoni yetu ya mwaka jana, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilituhumu kwamba Serikali hii ya CCM haiijatekeleza ahadi zake kwa Watanzania kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii kama zilivyotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2010 – 2015. Katika Maoni hayo tulidai kwamba ahadi ya “… kurekebisha viwango vya mafao ili visipishane mno haijatekelezwa hadi sasa kwani viwango vya mafao vinavyotolewa na Mifuko mbali mbali ya Hifadhi ya Jamii ni vile vile vya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.” Aidha, tulifafanua jinsi ambavyo ahadi ya “… ya kupanua wigo wa kinga ya hifadhi ya jamii ili Watanzania wengi zaidi wafaidike na huduma hiyo nayo haijatekelezwa.” Vile vile, tulionyesha jinsi ambavyo ahadi ya “kuelimisha jamii … juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa maendeleo ya wafanyakazi na ya nchi kwa ujumla”, nayo haikutekelezwa kwa sababu Serikali yenyewe imekiri kwamba ‘“… bado kuna uelewa mdogo wa masuala ya hifadhi ya jamii kwa watunga sera, waajiri, waajiriwa, wanachama na wananchi kwa ujumla.”’
Mheshimiwa Spika, katika Maoni yetu hayo tulionyesha kwamba ahadi pekee ambayo Serikali hii ya CCM imeitekeleza ni “… kuendelea kutumia fedha za wafanyakazi zilizomo katika Mifuko mbali mbali ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza katika miradi ambayo haina manufaa yoyote kwa wafanyakazi wenyewe.” Tulifanya rejea pana ya Taarifa Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Hesabu za Mashirika ya Umma na Taasisi Zingine kwa Mwaka 2010/2011, iliyoonyesha kwamba “… kuna udhaifu mkubwa katika vitega uchumi vinavyosimamiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.”
Hivyo, kwa mfano, ukaguzi wa vitega uchumi vya NSSF ulionyesha kwamba licha ya Mfuko huo kuwekeza zaidi shilingi bilioni 269.272 za wafanyakazi katika ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), sio tu Mfuko huo ‘“… ulikuwa haujasaini mkataba na Serikali juu ya fedha za mradi huo”’, bali pia ulikuwa ‘“… haujapokea fedha ya pango, au malipo ya mkopo kutoka Serikalini ambao tayari umelimbikiza riba ya shilingi bilioni 14.157.”’

Wednesday, May 29, 2013

VACANCIES ANNOUNCEMENT - MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL


MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL
VACANCIES ANNOUNCEMENT

1.0 MEDICAL SPECIALIST I (5 POSITIONS)
1.1 Reports to: Head of Firm
1.2 Duties and Responsibilities
 To participate in the planning and implementation of quality improvement strategies.
 To coordinate preparation of department budget input.
 To review inputs for, and coordinate preparation of periodical reports.
 To carry out operational and investigative research and issue reports accordingly.
 To review conditions of hospitalized staff and advise on appropriate medication.
 To supervise patients’ case presentation and participate in training other staff.
 To plan and carry out research.
 To attend to IPPM Clinics.
 To set performance targets for all staff in the unit and ensure that all staff have elaborate job plans.
 To supervise, appraise staff and identify development and training needs.
 To perform any other duty assigned from time to time by the supervisor.
1.3 Required Qualifications
 Holder of three or more years Postgraduate Degree (M.Med/M.Dent.) in one of the medical fields.
 Must be registered with the Medical Council of Tanganyika
 Mmust have worked as a specialist Medical Doctor for not less than three years
 Must have published not less than two research papers in their areas of specialization in the last six years, one of which he must be the principal author.
 Must be computer literate

2.0. MEDICAL SPECIALIST II (57 POSITIONS)
 Cardiac Anesthesiologists – 6 positions
 Surgeons - Training - 4 positions
 Cardiothoracic Surgery Trainees - 6 positions
 Cardiac Surgeons(Adults /Paediatric - 8 positions
 Vascular Surgeons - 2 positions
 Paeditricians –Training - 2 positions
 Physicians –Training - 2 positions
 Paediatric Cardiologist (Trainees ) - 10 positions
 Adult Cardiologists - 6 positions
 Anesthesiologists-Training - 2 positions
 Other specialties - 9 Positions
2.1 Reports to: Head of Firm
2.2 Duties and Responsibilities
 To provide routine specialized medical services for in-patients and out patients in their areas of specialization.
 To participate in the training of student doctors in their areas of specialization.
 To plan, supervise and evaluate medical services offered in their respective fields.
 To prepare periodic reports regarding medical services
 To carry out research in the medical field and publish results for use by other experts.
 To supervise junior medical doctors and give them needed technical advice in their respective areas of specialization.
 To plan and supervise outreach programmes in their areas of specialization.
 To carry out any other duties as assigned from time to time by their supervisors.
2.3 Required Qualifications
Holder of Doctor of Medicine degree with three or more years Masters Degree in one of the medical fields.
Must be registered with the Medical Council of Tanganyika.

MDIS MERIT SCHOLARSHIP FOR INTERNATIONAL STUDENTS, 2013/14


Management Development Institute of Singapore (MDIS), Singapore offers merit scholarship for international students. These scholarships are open to new students for pursuing a pre degree, degree or master’s degree programme at five renowned university partners from the United Kingdom, Australia and France.  Each scholarship is tenable only for the academic years for which it is awarded and will cover the subsidised portion of the tuition fee. Applicants can apply till 31st August 2013 for Phase 1 and 31st March 2014 for Phase 2.


CHUO CHA VETA - MIKUMI CHAVUNJWA KUPISHA UPANUZI WA BARABARA.

Chuo cha VETA Mikumi kimevunjwa ukuta wote wa mbele hasa upande wa kukaa wateja Hoteli ya VETA Mikumi baada ya kuonekana kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara.
Swali langu hapa ni kwanini hata Taasisi za serikali zinavunja sheria kwa kujenga hata kwenye hifadhi ya barabara?
Pongezi zangu za dhati ziwafikie wale wote waliofikia uamuzi huo wa kuvunja kuta hizo bila kujali kuwa hiyo ni Taasisi ya Serikali.







Tuesday, May 28, 2013

TENDER: SUPPLY OF WATER TREATMENT CHEMICALS DAWASCO


TENDER No. AE/032/ 2013-2014/HQ/G/01

FOR

SUPPLY OF WATER TREATMENT CHEMICALS


                            INVITATION FOR TENDERS



1.      The   Dare s salaam Water and Sewerage Corporation (DAWASCO)   has set aside funds for financial year 2013/2014 towards the cost of supplying water chemicals, and it intends to apply part of the proceeds of these funds to cover eligible payments under the contract for Procurement of Various Water Treatment Chemicals.

2.      The Dare s salaam Water and Sewerage Corporation now invites sealed tenders from eligible Suppliers for supplying water treatment chemicals as follows:

Lot No
Description
Unit
Quantity
1
Supply of water  chemical treatment Polymer Blend
Metric Tone
911
2
Supply of water Chemical Disinfectants case No. 1
Metric Tone
97.65
3
Supply of water Chemical Disinfectants case No. 2
Metric Tone
188.1
4
Supply of Poly Aluminum Chloride (PAC) powder
Metric Tone
740
5
Supply of Aluminum sulphate
Metric Tone
400
6
Supply of water treatment chemicals ( soda Ash)
Metric Tone
30

Tenderer may tender for a single lot or a combination of any lots, but in any case Tenderer must quote for full quantities in each lot. The purchaser shall evaluate   the Tender for each lot and award the contract on a lot- by – lot basis or a combination of lots whichever is more economical. Tenders not quoting full quantities in a lot will be considered as non-responsive.

  1. Tendering will be conducted through the International Competitive Tendering procedures specified in the Public Procurement (Goods, Works, Non-Consultant Service and Disposal of Public Assets by Tender) Regulations, 2005 – Government Notice No. 97 and are open to all Tenderers as defined in the Regulations.
  2. Eligible Tenderers may obtain further information from and inspect the Tendering Documents at the office of the  Secretary, DAWASCO Tender Board, DAWASCO House 2453/188 Sokoine Drive P.O. Box 5340 Dar es Salaam from 8:00 toAM 04:00pm on Monday to Friday inclusive, except on public holidays.

5.      A complete set of Tendering Documents may be purchased by any interested Tenderer upon submission of a written application to the address given under paragraph 4 above and upon payment of a non-refundable fee of Tsh.50,000.00 (Tanzanian Shillings fifty thousand Only) or equivalent in freely convertible currency. Payments shall be made either be by Banker’s Cheque, Banker’s Draft or Cash to be paid to the cashier’s office near reception office at DAWASCO Headquarters’ office.

6.      All Tenders must be accompanied by a Tender security in an acceptable form in the amount of 1% of the tender value or freely convertible currencies in case of foreign Tenderers

  1. All tenders in one original plus two copies properly filled in, and enclosed in plain envelopes must be delivered to the address below clearly marked Tender number AE/032/2013-2014/HQ/G/01 at or before WEDNESDAY 12 JUNE.2013 at 14:00pm HRS local time. Tenders will be opened promptly thereafter in public and in the presence of Tenderers’ representatives who choose to attend in the opening at the DAWASCO Boardroom, DAWASCO House, Plot No.2453/188 Sokoine Drive.

8.      Late Tenders, Portion of Tenders, Electronic Tenders, Tenders not received, Tenders not opened and not read out in public at the tender opening ceremony shall not be accepted for evaluation irrespective of the circumstances.




                                                        CHIEF EXECUTIVE OFFICE


DAWASCO HOUSE, 2453/188 SOKOINE DRIVE

P.O.BOX 5340

                                                                   DAR ES SALAAM

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...