Friday, April 12, 2013

UKWELI KUHUSU LADY JAYDEE KUANZISHA KITUO CHA REDIO


Kutokana na uvumi na taarifa mbali mbali kuhusu mpango wa Lady Jaydee kuanzisha kituo cha redio kiitwacho KWANZA FM leo mhusika (Jidee) kaweka mambo hazarani na kusema kuwa kwanza taarifa hizo zilikuwa ni uzushi kutokana na tarehe hiyo zilipotoka kuwa ni siku ya wajinga.

Ameweka bayana maneno hayo usiku wa leo wakati akifanya mahojiano (Interview) katika kituo cha televisheni cha Channel ten. Mahojiano hayo yalikuwa ni kati ya Jay dee na Dj Tass. Lakini lady Jaydee amesema kutokana na mwitikio aliouona kwa watu ameamua kuwa na mpango huo wa kuanzisha kituo hicho cha redio.

Kuhusu wimbo wake wa Joto hasira, amesema ameutunga na kuuimba kwa kumlenga mtu ambaye hakuwa tayari kumtaja.

RAIS KIKWETE AFUNGA SEMINA KWA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU DODOMA

Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifunga semina.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete afunga semina kwa
Mawaziri na Makatibu wakuu  katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma ikiwa na mpango wa kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo . Mfumo huo unaanza kutekelezwa  kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. 


Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete  tarehe 22 Februari, 2013 na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.

UJUMBE WA FIFA KUSHUGHULIKIA UCHAGUZI WA TFF KUWASILI APRILI 15

 TANGAZO TOKA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwatangazia wadau wa mpira wa miguu kuwa ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utawasili nchini Jumatatu (Aprili 15 mwaka huu) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, ujumbe huo utaongozwa na Mkuu wa Idara ya Uanachama ya FIFA, Primo Covarro na utafanya kazi kwa siku tatu kuanzia siku ya ujio na kuondoka Aprili 18 mwaka huu.
Ukiwa nchini, ujumbe huo utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao waliomba mashauri yao yaangaliwe upya, wagombea ambao walikata rufani FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Rufani na Sekretarieti ya TFF.
Wajumbe hao wangependa kukutana na waziri anayehusika na michezo, hivyo TFF imeiandikia Wizara ikipendekeza kuwa ujumbe huo ukutane na Waziri na wakuu wengine wa michezo Aprili 16 mwaka huu 2013 kabla ya kuanza kazi zao.
Wagombea watakaosikilizwa na ujumbe huo wa FIFA ni:
1.   Farid Salim Mbaraka Nahdi: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi na baadaye rufani yake kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kutupwa na hali kadhalika ombi lake la kutaka shauri lake liangaliwe upya, kukataliwa.
2.   Elliud Peter Mvella: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kukata rufani Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kabla ya maombi yake ya kutaka shauri lake kuangaliwa upya, kukataliwa.
3.   Mbasha Matutu: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi na kukata rufani ambayo pia ilitupwa kabla ya kuomba shauri lake liangaliwe upya, ombi ambalo lilikataliwa.
4.   Hamad Yahya: Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na kuondolewa. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ikatupa ombi lake.
5.   Jamal Emily Malinzi: Mgombea wa nafasi ya urais wa TFF ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kuondolewa kwenye mchakato. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini likakataliwa. Hata hivyo, alikuwa ameshakata rufani FIFA.
6.   Michael Wambura: Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na rufani yake kukataliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF. Hakuomba shauri lake liangaliwe upya, lakini alikata rufani FIFA.
Shirikisho linawaomba wote waliotajwa hapo juu kujiandaa kwa utetezi na maelezo ya kutosha na kwamba barua za kuwaita zinafuata.

BARCELONA vs BAYERN MUNCHEN, REAL MADRID vs BORRUSIA DOTTIMOND


"The best of Spain face the best of Germany in the semi-finals after today's draw paired FC Bayern München with FC Barcelona and pitted Borussia Dortmund against Real Madrid CF."

Haya ni maneno yaliyokutwa kwenye Website ya UEFA baada ya kupanga ratiba ya nusu finali ya Kombe la UEFA.

SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ASEMA WAKRISTO WANA HAKI YA KUCHINJA.


Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum
SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, amezungumzia mzozo wa kuchinja na kusema kuwa muumini wa dini yoyote anahaki ya kuchinja. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sheikh Salumu, alisema suala la kuchinja kila mtu anaweza kuchinja kutokana na imani yake.

Alhad alisema muumini wa dhehebu lolote anaweza kuchinja, huku akitoa angalizo kuwa uchinjaji huo uzingatie imani ya watumiaji wa nyama hiyo.

Sheikh Alhad alisema kwamba Wakristo wana haki ya kuchinja ilimradi nyama hiyo ni kwa ajili ya matumizi yao wenyewe katika familia zao na si vinginevyo.

“Binafsi sina tatizo katika suala la kuchinja kwani kulingana na utamaduni tuliokuwa nao Wakristo wana haki ya kuchinja kwa matumizi yao wenyewe na kama ni kwa ajili ya matumizi ya umma basi Waislamu wafanye hivyo,”alisema.

Aidha alizidi kusisitiza kuwa suala la kuchinja linahitaji mjadala miongoni mwa viongozi wa dini wenywewe na si kuitupia lawama Serikali kwa kuibua mijadala ambayo ni vigumu kwa Serikali kuwa na majibu yake kwa wepesi zaidi.

Alisema Serikali haiwezi kusuluhisha tatizo hilo bali ni kusimamia utatuzi wake, hivyo viongozi wa dini wana wajibu wa kuandaa mijadala yenye lengo la kuweka sawa mambo hayo.

“Kwa kupitia mijadala hii itakayo waunganisha viongozi wa dini zote mbili, wananchi wataweza kupata ukweli wa mambo mbalimbali yanayoonekana kuwa kero na yanayohatarisha ustawi wa amani ya nchi yetu.

“Sote ni wadau wa amani hivyo ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini kukaa na kuzungumzia matatizo yaliyopo ili tuweze kurejesha amani ambayo kwa sasa inatetereka ,”alisema Sheikh Salum

Habari na Mtanzania

KIPANYA NA HUDUMA YA MAJI TANZANIA

Katika vijiji vilivyovingi nchini Tanzania havina huduma ya maji safi.

Serikali inatakiwa kuwapa umuhimu na kuwafikiria kwenye huduma hiyo muhimu.

Tafakari,chukua hatua!!!!!!!!

KATIKA SAKATA LA KUPANDISHWA KWA NAULI,SUMATRA YAKAMATA MAGARI 75 KWA KUPANDISHA NAULI KABLA YA MUDA


 Wakati nauli mpya zikianza kutumika leo, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) imekamata magari ya kubeba abiria (daladala) 75 katika operesheni maalum iliyoanza mwanzoni mwa wiki hii katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Uamuzi wa kukamata magari hayo umekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya abiria ya kutozwa nauli kubwa kuliko iliyotangazwa na Serikali kuwa zianze kutumika leo.

Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe alisema jana mjini Dodoma kuwa ongezeko la viwango vipya vya nauli si tatizo, la muhimu ni wahusika kufuata vigezo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki wa Sumatra, Conrad Shio alisema kuwa,daladala zilizokamatwa zilikuwa na makosa mbalimbali yakiwemo kukatisha ruti, kutoza nauli, kuiba ruti na kufanya biashara ya kusafirisha abiria bila ya kuwa na kibali.

Alisema kutokana na hali hiyo wamiliki wa daladala zilizokamatwa wametakiwa kwenda na mikataba ya madereva wapya, ili wale wa zamani waweze kukaguliwa na Jeshi la Polisi Tanzania juu ya uhalali wa leseni zao.

“Tumepata malalamiko ya daladala 105 ambazo zimekuwa zikivunja sheria ya usafiri barabarani, ambapo daladala 75 tayari tumezikamata,” alisema Shio.
Aliongeza kati ya hizo, daladala 36 zilikatisha ruti, wakati 18 ziliiba ruti na 21 zilitoza nauli kubwa, jambo ambalo limewafanya wazichukulie hatua.
Alisema kuna nyingine zimebeba abiria bila ya kuwa na kibali, ambapo wamiliki wake wamechukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kutokana na hali hiyo, wamiliki wa daladala hizo wametakiwa kulipa faini na kwenda na mikataba ya madereva wapya ili madereva waliofanya makosa wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani. Alisema daladala ambazo zilikuwa zinafanya kazi bila ya kibali hasa nyakati za usiku katika baadhi ya maeneo zimepelekwa kwenye yadi ya Serikali ili wamiliki wake waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa sababu ni kosa kubeba abiria wakati huna kibali cha usafirishaji.

Alisema kuwa, ili kupunguza ukubwa wa tatizo, wamelifanya zoezi hilo kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwataka madereva wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili kupunguza malalamiko. Alisema kutokana na hali hiyo Sumatra itaendelea kukamata magari ambayo yataonekana yanaendelea kuvunja sheria kwa makusudi.

Habari hii ni kwa mujibu wa Mwananchi

Thursday, April 11, 2013

TAIFA STARS YAPANDA NAFASI 3 VIWANGO VYA SOKA DUNIANI.

Kocha mkuu wa Taifa stars Kim Poulsen
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars imepanda nafasi 3 katika viwango vya soka Duniani.
Katika ukanda wa Afrika,Timu ya kwanza ni Ivery Coast ikishika nafasi ya 12 Duniani na Afrika Mashariki,bado timu ya Uganda inaongoza ikiwa ya 92 duniani.
Duniani timu 10 Bora ni:- 1. Hispania, 2.Ujerumani, 3.Ajentina, 4.Koratia 5.Ureno, 6.Korombia,7.Uingereza, 8.Italia, 9.Uholanzi na 10.Ekwado.


Rnk
Team
Pts
+/- Pos


1
Spain
1538
0
Equal


2
Germany
1428
0
Equal


3
Argentina
1292
0
Equal


4
Croatia
1191
5
Up


5
Portugal
1163
2
Up


6
Colombia
1154
0
Equal


7
England
1135
-3
Down


8
Italy
1117
-3
Down


9
Netherlands
1093
-1
Down


10
Ecuador
1056
1
Up


11
Russia
1052
-1
Down


12
Côte d'Ivoire
1008
1
Up


13
Greece
986
-1
Down



92
Uganda
413
-7
Down


93
Estonia
411
-4
Down


94
Angola
401
1
Up


94
Guatemala
401
-3
Down


96
Dominican Republic
396
0
Equal


96
Iraq
396
-2
Down


98
China PR
388
11
Up


99
Benin
381
-13
Down


100
Niger
362
-7
Down


101
Zimbabwe
349
-1
Down


102
Qatar
346
-4
Down


103
Oman
344
2
Up


104
Liberia
334
14
Up


105
New Caledonia
333
-2
Down


106
Mozambique
330
1
Up


107
Ethiopia
328
5
Up


108
Saudi Arabia
324
-2
Down


109
Malawi
323
2
Up


110
Latvia
322
-2
Down


111
Lithuania
316
4
Up


112
Tajikistan
312
40
Up


113
Kuwait
311
0
Equal


113
Suriname
311
-3
Down


115
Korea DPR
310
-13
Down


116
Tanzania
305
3
Up


117
Bahrain
291
0
Equal
 

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...