Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, January 13, 2014

Waandamanaji wafunga barabara Bangkok.


Waandamanaji nchini Thailand wameanza kuweka vizuizi barabarani katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu Bangkok, katika harakati za kuiangusha serikali kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Februari Pili mwaka huu.

Sunday, January 12, 2014

Waziri wa serikali Libya auawa


Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.

Friday, December 6, 2013

MANDELA KUZIKWA JUMAPILI TAR. 15 DESEMBA, 2013.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde, endelea kutembelea blogu hii.

HATIMAYE MZEE NELSON MANDELA AIAGA DUNIA .

Nelson Mandela mwaka 2008
Hatimaye Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela aiaga dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuzaliwa mnamo mwaka 1918.
Habari kamili tutazidi kukuletea kadiri tutakavyokuwa tunazipata, endelea kutembelea blogu hii.

Sunday, October 13, 2013

Waumini wafa India ktk sherehe ya kidini.


Polisi nchini India wanasema watu kama 89 wamekufa kwenye mkanyagano katika sherehe ya Kihindu.
Maelfu ya waumini walivuka daraja nyembamba kufikia hekalu la Madhya Pradesh.

Baadhi ya watu walikanyagwa, wengine walizama waliporuka kutoka daraja kwenye mto uliofurika.
Afisa wa eneo hilo alisema watu wengi walijeruhiwa na waokozi wanatafuta miili mtoni.
Polisi wanasema msongamano ulianza kulipozuka tetesi kwamba daraja ilikuwa inakaribia kuporomoka.
Lakini mashirika ya habari ya huko yanasema chanzo ni polisi kuanza kutumia virungu, kudhibiti umati.
Mikanyagano kama hiyo hutokea mara kwa mara nchini India katika sherehe za kidini ambazo huwa na mtafaruku.

Chanzo: BBC

Friday, October 11, 2013

AU yalaani ICC kwa uonevu Afrika

AU inajadili swala hili baada ya ICC kupuuza ombi la kutaka kuhamisha kesi za Kenyatta na Ruto

Mawaziri wa mambo ya nje Afrika wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili uhusiano wa bara la Afrika na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ethiopia Tedros Adhanom Ghebreyesus ameilaani mahakama ya ICC kwa kusema ina mapendeleo sana na hicho sio kitu kinachokubalika na kuwa ina uonevu kwa nchi za Afrika.

Tuesday, October 1, 2013

Wabunge, Kenya - wakimbizi waondolewe !


Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndungu Githinji amesema kuwa wana habari kuwa kambi zilizoko kwenye mipaka ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kiislamu.
Kenya inahifadhi wakimbizi wa kisomali zaidi ya nusu milioni katika kambi za Dadaab zilizoko kwenye mpaka na Somalia.

Friday, September 27, 2013

Wakuu wa usalama kuhojiwa Kenya.


Maafisa wakuu wa ujasusi wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.

Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.
Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.

Walipuuza onyo?

Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.

Chanzo: BBC

Sunday, August 18, 2013

Djotodia aapishwa kama rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kiongozi wa zamani wa waasi ambaye alifanya mapinduzi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia ameapishwa kama rais.
Bwana Djotodia ameahidi kuandaa uchaguzi kufikia mwanzo wa mwaka ujao. Tangu achukue uongozi mwezi Machi kupitia kikundi cha waasi wa Seleka nchi hiyo imetajwa kutumbukia zaidi katika umaskini na utovu wa sheria.
Shirika la Umoja wa mataifa linakadiria kuwa zaidi ya thuluthi moja ya raia wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa dharura.
Baraza la uslama la Umoja wa mataifa limeonya kuwa kuongezeka kwa ukatili na uvunjifu wa sheria katika Jamhuri ya Afrika ya Kati inatishia usalama na uthabiti wa eneo lote.
Msemaji wa rais wa zamani Francois Bozize ambaye aling'olewa madarakani na bwana Djotodia amemtaja kiongozi huyo mpya kama 'kibaraka'.
Msemaji huyo Levi Yakete, amenukuliwa katika Redio Ufaransa kusema:
'Bwana Djotodia, ambaye ameingia madarakani kwa njia ambazo sote tunaelewa, ni kibaraka tu wa Chad na Sudan. Aliingia madarakani kupitia njia ambazo hazikubaliki na watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Alipindua utawala wa kisheria na katiba, ambao ulikuwa unaongozwa na Francois Bozize.'

Chanzo : BBC

Monday, July 29, 2013

KAMPENI ZA UCHAGUZI KUFUNGWA LEO ZIMBABWE.

Rais mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo yuko nchini Zimbabwe kama mwangalizi wa uchaguzi mkuu.
Kampeini za kisiasa nchini Zimbabwe zinamalizika hii leo kabla ya uchaguzi mkuu hapo Jumatano wiki hii.
Kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change ambaye pia ni Waziri MKuu ,Morgan Tsvangirai, hii leo atahutubia mkutano wa hadhara mjini Harare katika uwanja alikofanya mkutano wake hio jana Rais Robert Mugabe.
Viongozi hao wawili wamekua katika serikali ya muungano tangu mwaka wa 2008 na wametofautiana kuhusu muda uliowekwa kufanyika uchaguzi. Kumekua pia na madai ya wizi wa kura, na vitisho dhidi ya wafuasi wa MDC.
Shirika la kimataifa linalotathmini hali ya mizozo The International Crisis Group limeonya kwamba hakuna mazingira ya uchaguzi huru na haki Zimbabwe.

CHANZO:BBC.

Friday, July 26, 2013

JESHI LA POLISI MISRI LATOA ONYO KALI KWA RAIA.

Maandamano Nchini Misri.
Jeshi la Misri limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya makundi yatakayosababisha ghasia na machafuko wakati wa maandamano ya leo.
Mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Sisi ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuandamana katika b arabara za mji kuunga mkono juhudi zao za kukabiliana na vitendo vya kigaidi.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi vile vile wanatarajiwa kushiriki katika maandamano hayo.
Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi tangu tarehe tatu mwezi huu.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali amesema, Bwana Morsi anazuiliwa kuhusiana na uhusiano na wapiganaji wa Kiislamu wa Hamas nchini Palestina.
Shirika la habari la serikali, Mena, limesema Bwana Morsi anachunguzwa kufuatia madai kuwa anashirikiana na kundi hilo la Hamas kushambulia vituo kadhaa vya polisi na magereza wakati wa mageuzi ya mwaka wa 2011.

Lakini chama chake cha Muslim Brotherhood, kimesema kuwa kilipata msaada kutoka kwa raia wa nchi hiyo kushambulia magereza na wala sio raia wa kigeni kama inavyodaiwa.
Maandamano nchini Misri
Kiongozi huyo kwa kwanza kuwahi kuchaguliwa kwa njia ya Kidemokrasia kuongoza Misri, aliondolewa madarakani baada ya raia wa nchi hiyo kuandamana wakati wa sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu alipochukua madaraka.
Tangu wakati huo, Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi la nchi hiyo katika eneo lisilojulikana.
Shirika hilo la Mena limesema agizo lilitolewa kwa rais huyo kuzuiliwa kwa muda wa siku kumi na tano.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa tangazo hilo sasa limeondoa wasi wasi kuhusiana na hatma yake, hasa kufuatia shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa ya kutaka rais huyo wa zamani kauchiliwa huru an kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi Kanali Ahmed Mohammed Ali amesema jeshi la nchi hiyo litaruhusu maandamano ya amani lakini ameonya kuwa watakabiliana vikali na kundi lolote ambalo litajaribu kusababisha machafuko.

Chanzo:BBC

Wednesday, July 24, 2013

Mkuu wa jeshi Misri aitisha maandamano.

Mkuu wa jeshi la Misri Abdel Fattah al-Sisi.

Mkuu wa Jeshi la Misri amewataka wananchi kujitokeza kuandamana siku ya Ijumaa dhidi ya kile anachokiita ugaidi.
Abdel Fattah al-Sisi amesema anawataka watu kuunga mkono jeshi na kulikabidhi jukumu la kukabiliana na ghasia pamoja na ugaidi.
Wafuasi wa Mohammed Morsi aliyeondolewa mamlakani na jeshi, wamekuwa wakiandamana dhidi ya jeshi ambalo lilimuondoa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Lakini Generali Sisi alisema wito wake sio wa ghasia bali anataka kuwepo maridhiano ya kitaifa.

Source:BBC

RAIS WA SUDANI KUSINI AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI, MAREKANI YAIONYA RWANDA NA MABOMU YA TANZANIA KENYA.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa mawaziri wote kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa wale waliofutwa kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri litakalobuniwa.
Pia hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais kuwafuta kazi maafisa hao , lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu wake Machar wamekuwa na mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi tangu kujitenga na Sudan mwaka 2011.

Tuesday, July 23, 2013

M23 WADAIWA KUUA NA KUBAKA WANAWAKE ZAIDI YA 40 CONGO


Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi la wapiganaji la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrsia ya Congo limewaua zaidi ya watu arobaini na kuwabaka zaidi ya wanawake na wasichana sitini tangu Machi mwaka huu.
Baada ya kuwahoji zaidi ya watu mia moja eneo hilo, shirika hilo lilisema kuwa waasi hao wanawasajili kwa nguvu vijana huko DRC na wengine kutoka nchi jirani ya Rwanda.

Kundi hilo limeongeza kuwa Jeshi la Rwanda bado linawasadia moja kwa moja waasi hao licha ya serikali ya Kigali kupinga hilo mara kwa mara.
Wakati huohuo, jeshi la DRC hapo jana lilishambulia ngome za waasi hao karibu na mji wa Goma Mashariki mwa DRC.
Haya yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu vita kati ya pande hizo mbili kuanza Jumatatu asubuhi na kusitishwa siku hiyo mchana.
Kundi hilo limesema liko umbali wa kilomita nne kutoka mji wa Goma, ingawa limesema lengo lake ni kulazimisha serikali kufanya mazungumzo nao wala sio kuteka mji wa Goma.
M23 liliuteka mji wa Goma, kwa siku kumi mwezi Novemba kabla ya kuondoka mjini humo kufuatia shinikizo za jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na serikali ya rais Joseph Kabila.
Mazungumzo na serikali yalianza mjini Kampala mwezi Disemba ingawa baada ya miezi miwili jeshi likaanza tena mapigano na waasi hao mwezi Julai tarehe 14.
Kulingana na Umoja wa Mataifa mapigano hayo yamesababisha takriban watu 4,200 kutoroka makwao.
Chanzo: BBC

Maelfu wajitokeza kumlaki Papa Rio De Janeiro.


Baba Mtakatifu Francis amelakiwa na maelfu ya mahujaji wa Brazil wakati akianza ziara yake ya kwanza ya nje tangu achaguliwe kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki.
Baba Mtakatifu huyo wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini alitembelea jiji la Rio De Janeiro, akiwa kwenye gari la wazi na kisha kukutana na Rais Dilma Rousseff , katika kasri la taifa la gavana.

Baada ya kuondoka, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi, kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali na gharama kubwa za ziara hiyo.
Yuko Brazil kuhudhuria Sherehe za Siku ya Vijana Wakatoliki Duniani.
Katika hotuba yake mara baada ya kuwasili, Baba Mtakatifu alitoa wito kwa vijana Wakatoliki kuwa manabii wa mataifa yote.
“Nimekuja kukutana na vijana kutoka sehemu zote duniani, waliovutika kwenye mikono ya Yesu Kristo Mwokozi,” amesema akiimanisha sanamu maarufu ya Yesu iliyopo katika jiji la Rio.
“Wanataka kutafuta hifadhi katika mikono yake, karibu kabisa na moyo wake ili wasikie wito wake kwa nguvu na wazi.”
Takriban saa moja mara baada ya sherehe za kumkaribisha, polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na yale ya kushtua dhidi ya waandamanaji nje ya kasri.
Yalikuwa ni maandamano ya hivi karibuni ambayo waandamanaji wanasema ni ya kupinga vitendo vilivyokithri vya rushwa ndani ya serikali na nchi nzima.
Lakini baadhi yao wamechukizwa na dola za Kimarekani milioni 53 zilizotumika kuandaa ziara ya Baba Mtakatifu.
Kulikuwa na uharibifu kiasi na watu kadhaa kukamatwa, lakini ilikuwa kama ishara kwamba, upo uwezekano wa ziara hiyo ya kihistoria ya Baba Mtakatifu ikagubikwa na matukio yasiyo ya kawaida ya kisiasa.
Katika hatua nyingine, jeshi la Brazil limesema, bomu la kutengeneza nyumbani limegunduliwa karibu na eneo moja takatifu kati ya Rio na Sao Paulo ambalo kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anatarajiwa kulitembelea siku ya Jumatano.
Bomu hilo lilikowa na nguvu kidogo, lilidhibitiwa baada ye.
Wakati Baba Mtakatifu Francis akiteremka kutoka kwenye ndege ya shirika la Alitalia, kwenye uwanja wa ndege wa Rio, mapema Jumatatu, alilakiwa na Rais Rousseff huku umati wa watu ukishangilia na alikabidhiwa shada la maua, huku kwaya ya vijana ikiimba wimbo unaohusu siku ya vijana.
Aliwapungia mkono watu na msafara wake kuelekea katikati ya Rio ambako maelfu ya mahujaji walikuwa wamekusanyika.
Baba Mtakatifu Francis alionekana mwenye furaha na kutulia wakati akielekea jijini Rio akiwa ndani ya gari la kawaida huku dirisha likiwa limefunguliwa na maafisa usalama wakihangaika kuudhibiti umati.

Kulikuwa na matukio ya fujo wakati gari lake lilipokwama kwenye moja ya msongamano wa magari katika jiji la Rio, baada ya dereva wake kukosea njia na kuzikosa zile zilioandaliwa kwa ajili ya msafara wa Papa.

Mara umati ulizingira gari lake ukiwa na matumaini ya kumuona kwa karibu ama kumgusa. Mwanamke mmoja alimpitisha mtoto wake kwenye dirisha la gari ili Baba Mtakatifu ambusu.
Alipofika katikati ya jiji Papa alipanda gari la wazi lililoandaliwa maalum kwa ajili yake, huku akipunga mkono kwa maelfu ya watu waliojipanga pembezoni mwa barabara.
“Siwezi kusafiri kwenda Rome, lakini amekuja kuifanya nchi yangu kuwa njema na kuimarisha imani yetu,” alisema mzee mmoja wa miaka 73, Idaclea Rangel, huku akibubujikwa na machozi.
Mamlaka imeimarisha ulinzi wakati wa ziara ya siku saba ya Papa, kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchi nzima kupinga rushwa na utawala mbovu.
Papa Francis alikataa kutumia gari maalum lisilopenyeza risasi, licha ya maombi kutoka kwa maafisa wa Brazil, maafisa wa usalama wapatao 30,000, jeshi na polisi wataimarisha ulinzi wakati wa ziara hiyo.
Zaidi ya vijana Wakatoliki milioni moja wanatarajiwa kukusanyika Rio kwa ajili ya Siku ya Vijana Duniani, ambyo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili, ni sherehe za waumini Wakatoliki.
Papa huyo mzaliwa wa Argentina, ambaye alishika wadhifa huo Machi mwaka huu, anatarajiwa kuongoza ibada katika ufukwe wa pwani ya Copacabana siku ya Alhamisi na pia kutembelea moja ya vitongoji masikini.
Chanzo:BBC

WATU 9 WAUAWA NCHINI MISRI.


Watu tisa wameuawa mjini Cairo, Misri katika makabiliano yaliyodumu usiku kucha kati ya wafuasi na wapinzani wa rais aliyengo'lewa mamlakani Mohammed Morsi.
Maafisa wanasema kuwa , ghasia zilitokea wakati wa maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa Morsi.

Familia ya Bwana Morsi imetuhumu jeshi kwa kumteka nyara kiongozi huyo wa zamani.
Rais huyo wa zamani amezuiliwa na jeshi katika sehemu isiyojulikana bila ya kufunguliwa mashtaka yoyote, tangu mkuu wa majeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi, kutangaza kung'olewa mamlakani kwa Morsi tarehe 3 Julai.
Chama cha Bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kimekataa kutambua serikali ya kijeshi huku kikifanya maandamano karibu kila siku kote nchini Misri.
Ghasia hizo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 tangu kuondolewa mamlakani kwa Morsi.
Siku ya Jumatatu mtu mmoja alifariki na wengine wengi wakijeruhiwa wakati wa maandamano mjini Cairo, kwa mujibu wa maafisa wa afya.
Televisheni ya taifa iliripoti kuwa wafuasi wa Morsi waliokuwa wanaandamana walikamatwa kwa umiliki haramu wa silaha.
Vifo zaidi vimeripotiwa katika makabiliano mengine tofauti katika mkoa wa Qalyubiya Kaskazini mwa Cairo.
Wakati huohuo, familia ya Morsi ilisema hawajawasiliana kamwe na Morsi, na ikathibitisha kuwa wanaitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kuanzisha uchunguzi juu ya kupinduliwa kwake.
Nchi kadhaa ikiwemo Marekani zimetaka Morsi aachiliwe.
Lakini maafisa wa kijeshi wanasisitiza kuwa anazuiliwa katika eneo salama.

Source: BBC

Monday, July 22, 2013

UKATAJI HARAMU WA MITI WAPUNGUA - CONGO.

Ukataji haramu wa miti katika moja ya misitu mikubwa duniani ,umepungua
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, picha za Satelite za msitu wa Congo, zinaonyesha kuwa zilionyesha ukataji haramu wa miti umepungua kwa thuluthi moja tangu mwaka 2000.
Watafiti wanaamini kuwa sababu iliyochangia kupungua kwa ukataji haramu wa miti ni watu kuzingatia zaidi uchimbaji wa mdini na mafuta kuliko kilimo ambacho husababisha kukatwa kwa miti.
Daktari Simon Lewis, kutoka chuo kikuu cha Leeds na kile cha College London, alisema kuwa: "matukio yamekuwa yakilenga zaidi msitu wa Amazon na Kusini Mashariki mwa
"lakini katika utafiti wetu, tuliegemea zaidi katika kutaka kujua mengi kuhusu msitu huu ambao hatuna taarifa zaidi kuuhusu,'' alisema daktari Simon Lewis
Miti mikubwa zaidi
Msitu huo wa Congo ambao ni mkubwa zaidi Afrika, unakaribia msitu wa Amazon kwa ukubwa. Una upana wa kilomita milioni mbili .
Utafiti huu umefichua kuwa msitu huo uko katika hali nzuri kiliko ilivyotarajiwa.
Picha zilizopigwa kutoka anga za juu, ziliwaruhusu watafiti kuangalia zaidi hali ya msitu na miti iliyokatwa kwa kipindi kirefu na kuwa hali ilikuwa inabadilika mara kwa mara.
Misitu mikubwa wakati mwingi hukatwa kuwezesha watu kufanya biashara ya kilimo.
Waligindua kuwa mapema miaka ya tisini misitu ilikuwa inakatwa kila mwaka.
Lakini kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2010, kiasi cha kukatwa miti kilipungua.
Chini ya ukubwa wa kilomita 2,000 ya msitu hukatwa kila mwaka.
"matokeo yalikuwa ya kushangaza sana,'' alisema Dokta Lewis.
"moja ya sababu inayopelekea hali hii ni sehemu ya misitu ambayo inapewa ulinzi mkali.
Lakini pia ni kwa sababu hakuna wakulima wanakata miti kwa sababu ya kutaka kufanya kilimo pamoja na ambavyo nchi hizi zimepanga uchumi wao.
"zinategemea sana mafuta na madini na zinawekeza katika sekta hiyo wala sio kupanua kilimo,'' aliongeza dokta Lewis.
Utafiti mwingine ulionyesha tofauti kubwa sana kati ya miti iliyo katika msitu wa Congo na ile inayopatikana katika misitu mingine kote duniani.

Chanzo:BBC 

Friday, July 19, 2013

MAPIGANO YA KIKABILA YAZUKA KIDAL - MALI.

Waandamanaji wachoma magurudumu kupinga hatua ya jeshi kuingia mji wa Kidal Kaskazini mwa Mali.
Machafuko hayo yanajiri wiki moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi wa urais katika taifa hilo lililotekwa na wanamgambo wa kiislamu mwaka uliopita.
Wanajeshi wa Ufaransa walioko katika eneo hilo wameripotiwa kufyatua risasi hewani kutawanya makundi hayo mawili.Wakati huo huo shirika la kutoa msaada, Islamic Relief, lenye makaazi yake nchini Uingereza limeonya kwamba licha ya mzozo kumalizika, eneo la kaskazini mwa Mali bado linakubwa na mkasa wa kibinadamu huku shule nyingi zikibaki kufungwa na masoko mengi kuahirishwa.
Mzozo uliopo kaskazini mwa mali umebuni kisiwa cha umaskini mkubwa katika eneo ambalo tayari limeathirika na kiangazi na uhaba wa chakula kabla ya vita kuzuka.
Shirika la Islamic Relief linasema watu milioni moja unusu sasa wanategemea chakula cha msaada , huku wengine milioni mbili wakikabiliwa na tishio la baa la njaa.
Waandamanaji wachoma magurudumu kupinga hatua ya jeshi kuingia mji wa Kidal Kaskazini mwa Mali
Hata kabla ya kampeni ya kuwatimua wanamgambo wa kiislamu iliyoongozwa na Ufaransa kuanza, takriban asilimia themanini ya chakula cha eneo hilo kilitoka maeneo ya kusini yenye rutuba nyingi au kutoka mataifa jirani ya Algeria na Libya.
Nyingi ya barabara za kufanyia biashara kuelekea kaskazini zimefungwa kutokana na hali duni ya usalama na masoko kuahirishwa. Shirika la Islamic Relief linasema vita vimesababisha uharibifu wa mfumo wa usambazaji maji huku mabomba pamoja na visima vya maji vikiharibiwa kabisa.
Shirika hilo linasema kiwango cha mateso wanayokumbana nao wakaasi wa kaskazini mwa Mali kinafumbiwa macho. Limetowa wito kwa jamii ya kimataifa kufadhili mpango wa dharura wa kutoa msaada pamoja na miradi ya maendeleo ya kudumu.
Islamic Relief limesema kuwa kwa upande wake, limetowa chakula cha msaada pamoja na mbegu kwa wakulima.
Wapiganaji wa kundi la waasi la MNLA nchini Mali

Chanzo: BBC

Thursday, July 18, 2013

HAPPY BIRTH DAY NELSON MANDELA (18,JULAI), ATIMIZA MIAKA 95 YA KUZALIWA..


Rais mtaafu wa Afrika Kusini Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18, Julai 1918 huko Mvezo Afrika Kusini na hii leo anatimiza umri wa miaka 95. Katika maisha yake ameweza kuoa wake watatu mpaka sasa wa kwanza ni Evelyn Ntoko Mase (1944–1957), wa pili ni Winnie Madikizela (1958–1996) na wa mwisho na ambaye anaendelea kuishi naye mpaka sasa ni Graça Machel (1998–present).

Uzazi wa Mzee Mandela ni wa watoto Madiba Thembekile,Makgatho Lewanika, Makaziwe, Maki,Zenani na Zindziswa.
Leo Afrika Kusini wanasherehekea kuzaliwa kwa Mandela na kutimiza umri wa miaka 95 ya kuzaliwa. Katika hatua nyingine Rais Obama wa M&arekani amemtumia salamu za pongezi na ameitaka dunia kuheshimu mchango wake.
Mzee Mandela  amekuwa Rais wa Afrika Kusini tangu 10, Mei 1994 – 14, Juni 1999 na ndiye Rais wa kwanza wa Asili ya Kiafrika kuongoza Afrika Kusini.
Kwa sasa Mzee Mandela bado amelazwa katika hospitali akiendelea na matibabu.

Na hii hapa ndiyo taarifa kamili ya Mandela.
Personal details
Born Rolihlahla Mandela
(1918-07-18) 18 July 1918 (age 94)
Mvezo, South Africa
Nationality South African
Political party African National Congress
Spouse(s) Evelyn Ntoko Mase (1944–1957)
Winnie Madikizela (1958–1996)
Graça Machel (1998–present)
Children Madiba Thembekile
Makgatho Lewanika
Makaziwe
Maki
Zenani
Zindziswa
Josina Z. Machel (step daughter)
Malengani Machel (step son)
Residence Houghton Estate, Johannesburg, Gauteng, South Africa
Alma mater University of Fort Hare
University of London External System
University of South Africa
University of the Witwatersrand
Religion Christianity (Methodism)
Signature Signature of 
Nelson Mandela
Website www.nelsonmandela.org

Monday, July 8, 2013

Ndege ya Rais wa Somalia 'yashika moto'


Ndege iliyokuwa inambeba rais wa Somalia, imelazimika kutua kwa dharura mjini Mogadishu baada ya moja ya mabawa yake kushika moto.
Msemaji wa Hassan Sheikh Mohamud, alisema kuwa haijulikani kwa nini injini ya ndege ilisita kufanya kazi.
Rais Hassan Sheikh Mohamud, alielezea kuwa rais hakujeruhiwa lakini wazima moto walifanya kila hali kuzima moto huo.
Bwana Mohamud alichaguliwa kama rais wa Somalia mwaka jana katika mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, katika hatua za kumaliza vita vya miaka mingi.
Mwandishi wa BBC Mohamed Mwalimu, alisema kuwa magurugumu ya ndege yaliharibiwa vibaya baada ya tukio hilo.
Rais alikuwa anaelekea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, wakati ndege hiyo ilipolazimika kurejea Mogadishu.
Moja ya ripoti zilizotolewa za mwanzo kuhusu tukio hilo, ilitoka kwa akaunti ya Twitter ya kundi la al-Shabab lakini haikusema kama imeshambulia ndege hiyo.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika pamoja na wale wa Somalia, wanaounga mkono bwana Mohamud wamewaondoa wapiganaji wa al-Shabab kutoka mji mkuu Mogadishu, mwaka jana ingawa kundi hilo bado hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia.
Serikali mpya ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kutambuliwa na serikali ya Marekani na shirika la fedha duniani (IMF).

source...BBC

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...