Wednesday, December 17, 2014

WAKURUGENZI 6 WAFUKUZWA KAZI KWA KUBORONGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, AISHA MADINDA AFARIKI.

WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia 
WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia leo amewavua madaraka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliua, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda kufuatia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba, 14 mwaka huu. Wakurugenzi wengine watano (5) bado wanachunguzwa.
Aidha Waziri Ghasia amesema kuwa hawezi kujiuzulu kama alivyoahidi baada ya watendaji waliozembea kugundulika.

Kifo cha Madinda.
 Msanii mnenguaji wa bendi ya Extra Bongo, Aisha Mbegu "Madinda" amefariki leo mchana katika Hospitali ya Mwananyamala na chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika.

Kwa taarifa zaidi, endelea kutembelea blogu hii.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...