Friday, March 21, 2014

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE.

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakitazama bidhaa zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho kilisimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha


Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyeusi) akioneshwa moja ya mashine zilizokuwa zinatumika kutengenezea matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichopo katika jiji la Arusha na Mwangalizi wa Kiwanda hich, Bw. Leonald Mgoyo. Serikali ina mpango wa kukifufua kiwanda hicho baada ya kusimama uzalishaji tangu mwaka 2007.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (mwenye suti nyusi) akiagana na Mwangalizi wa Kiwanda hicho, Bw Leonald Mgoyo baada ya ukaguzi wa kiwanda hicho. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Gideon Nasari na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uzalishaji, Bw Maduka Kessy.

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakifurahia jambo wakati wa ukaguzi huo
(
Picha na Joyce Mkinga,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO).

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...