Wednesday, March 19, 2014

MGOMO WA DALADALA WAZUA TAFRAN MOROGORO ASUBUHI YA LEO.

Watu wakiwa wamejaa barabara ya Kihonda - Mjini.
Hali ya usafiri kwa abiria wa Manispaa ya Morogoro wamekuwa katika wakati mgumu asubuhi ya leo baada ya Daladala kugoma kutoa huduma ya usafirishaji kutokana na sababu ambazo hazikufahamika mara moja. Lakini kutokana na maneno yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu waliokuwa kwenye daladala zilizokuwa zikipita zikiwa hazina abiria, wamesema kuwa wamechoshwa na kubambikiziwa makosa na maaskari wa usalama barabarani.
Abiria wakiwa kwenye pick up ambazo zilikuwa zinasafirisha kwa Tsh.500/= 
Abiria wakiwa kwenye bajaj kwa nauli ya Tsh.500/=
Noah nazo zimetoa huduma ya usafirishaji kwa Tsh.1000/=

Abiria wakipakiwa kwenye Noah.
Wanafunzi nao wakiwa wanatembea kwa mguu

Watu wakiwa wanatembea kwa mguu

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...