Thursday, January 9, 2014

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA HITIRAFU YA UMEME - MOROGORO.

Wananchi wakiwa wanajaribu kuvunja dirisha ili waweze kuzima moto .

Nyumba moja ailiyotambulika kuwa mmiliki wake ni Mama Mkambala mtaa wa Uhuru Manispaa ya Morogoro, jana jioni iliteketea kwa moto baada ya kutokea hitirafu ya umeme. Kutokana na juhudi zilizofanywa na Wananchi kwa kushirikiana na Kikosi cha zima moto, moto uliweza kudhibitiwa usiweze kusambaa kwenye nyumba za jirani. Katika kazi hiyo ya kuzima moto changamoto ilikuwa ni namna ya kuingia ndani ya nyumba baada ya nyumba hiyo kuwa imefungwa.
Hata hivyo, thamani halisi ya mali zilizoteketea bado haijafahamika na hakuna majeruhi yeyote kutokana na moto huo.



Fundi wa TANESCO akiwa anakata umeme.


Wananchi wakiwa wanazima moto kwa ndoo.


Muonekano wa nyumba baada ya moto kuzimwa.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...