Sunday, January 12, 2014

TANGAZO LA SKOLASHIPU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI YA INDONESIA KWA TANZANIA KWA MWAKA 2014/2015.

Serikali ya Tanzania imepokea mwaliko wa Skolashipu kutoka kwa Serikali ya Indonesia kwa mwaka 2014/2015. Skolashipu hizo ni kwa kipindi cha kati ya miezi sita na/au mwaka mmoja.

Wadau wote, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa wanashauriwa wasome mwongozo na wajaze fomu za maombi zinazopatikana kwenye Mtandao wa Serikali ya INDONESIA ufuatao ”http://darmasiswa.kemdiknas.go.id ”

Fomu za maombi zilizokamilika kujazwa pamoja na viambatisho vilivyoainishwa ziwasilishwe kwenye Ubalozi wa Indonesia hapa Tanzania kabla ya tarehe 24/01/2014.

Katibu Mkuu,
Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
S. L. P 9121,
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...