Friday, October 24, 2014

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda wakamilika

Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Na Mwandishi wetu, Mpanda
Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.
Aliiambia timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.
Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.
Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.

Wednesday, October 22, 2014

MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO - TANZANIA BROADCASTING CORPORATION (TBC) 21/10/2014.

MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO - TBC 21/10/2014
 WASILIWA WALIOFANIKIWA KUENDELEA NA USAILI WA MAHOJIANO WANATAKIWA KUZINGATIA MAHALI NA MUDA WA USAILI.
KADA: PRODUCER II               
MWAJIRI: TANZANIA BROADCASTING CORPORATION (TBC)
TAREHE: USAILI WA MAHOJIANO 22/10/2014, SAA MOJA KAMILI ASUBUHI
MAHALI: TBC TAIFA - NYERERE ROAD               

EXAM NUMBERS        SCORE    REMARKS
PSRS-TBC-PRD-031    60       SELECTED
PSRS-TBC-PRD-013    55.5    SELECTED

Monday, October 20, 2014

UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.

ADDITIONAL LIST OF SELECTED CANDIDATES 2014/2015 MZUMBE - BATCH ELEVEN.

CANDIDATES SELECTED TO JOIN BACHELOR DEGREE PROGRAMMES 2014/2015 - DIT.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...