Tuesday, April 30, 2013

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MCH.PETER MSIGWA JUU YA MALIASILI NA UTALII.

Mchugaji Peter Msigwa.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI MHE. MCHUNGAJI PETER MSIGWA, (MB) WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014. (Yanatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) toleo la mwaka 2013)



1.0 UTANGULIZI.
Mheshimiwa Spika,dhima kuu ya wizara hii ni uhifadhi endelevu wa maliasili na malikale na kuendeleza utalii kwa manufaa ya kizazi kijacho. Katika kufanikisha dhima hii wizara ina idara za wanyamapori, utalii, mambo ya kale, utawala na usimamizi wa rasilimali watu na sera na mipango, pamoja na taasisi, vyuo na wakala na mifuko ya uhifadhi inayosimamiwa chini ya wizara hii. Hotuba yangu imelenga kupitia changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili wizara pamoja na kutoa mapendekezo mbalimbali. 

Mheshimiwa Spika, sisi kama wabunge bila kujali CHADEMA, CUF,TLP,UDP CCM au NCCR MAGEUZI tunaamini kwa dhati tunajua kipi ni chema kwa watu wetu na kwa ujumla kushawishika katika uendelevu wa maliasili zetu, haya hayawezi kufikia kwa kutetea maslahi ya sisi binafsi na vyama vyetu pasipo kujifanya kuingiwa na upofu na kutenda kile tunachokiamini. 

UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2012/2013 

Mheshimiwa Spika,Taarifa za wizara juu ya utekelezaji wa bajeti ya 2012/2013 mbele ya kamati na vile zinavyoonekana katika randama ya mapato na matumizi, inaonesha wazi jinsi wizara na serikali ilivyoweka nyuma swala la miradi ya maendeleo na ulinzi wa rasilimali asili za kitanzania hasa kwa manufaa ya Taifa. 

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2012/2013 bunge lilipitisha na kuidhinisha fedha za miradi ya maendeleo kutoka katika mapato ya ndani na nje, na hadi kufikia February 2013 wizara ili pokea sehemu ya fedha za nje tuu na hakuna fedha za ndani zilizoelekezwa katika miradi ya maendeleo, pamoja na kupata fedha za nje ambazo ni shilingi 360,002,100 kati ya shilingi 12,712,682,390 bado fedha hizo zilizopokelewa na wizara zinajumuisha fedha za mwaka 2011/2012 shilingi 3,288,835,448/- huu ni uthibitisho dhahiri wa serikali kutoweka kipaumbele miradi ya maendeleo na kuweka rehani kwa wahisani swala la kuendeleza Taifa.

Mheshimiwa Spika,Pamoja na wizara kutoa taarifa imeainisha changamoto zilizopo katika utekelezaji ikiwa ni pamoja na kukabiliana na ujangili,uhaba wa fedha, viendea kazi hafifu, je changamoto kuelezea chanagamoto hizi kwa serikali inayotangaza kukabiliana na tatizo la ujangili pasipo kutenga fedha za kuiwezesha wizara ni nia ya dhati kwa serikali kudhibiti ujangili unaofanywa na mitandao yenye kutumia fedha nyingi? 

Mheshimiwa Spika, katika miradi saba iliyopangwa kutekelezwa na wizara ni pamoja na miradi ya idara ya wanyamapori na idara ya misitu na nyuki kama ilivyoanishwa katika kasma namba 2001 na 3001, na serikali kutoipatia wizara fedha za ndani mpaka sasa ni dhahiri serikali kutotambua na kutoona wazi tatizo la ujangili na uharibifu wa misitu katika nchi yetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kupitia ahadi zake za kutokomeza ujangili ni vema sasa ikatekeleza kwa vitendo, hivyo basi hatuwezi tegemea wahisani kulinda rasilimali zetu huku taarifa kuonesha uhusikaji mkubwa wa mitandao ya ujangili kutoka nje ya nchi.

HISTORIA YA UHIFADHI KATIKA JAMII ZA WAFUGAJI


Mheshimiwa Spika, uhifadhi wa wanyamapori katika historia tangu utawala wa kikoloni sera na sheria zilizotumika kwa miaka mingi hususani maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro, mfumo uliopo sasa pamoja na kutishia mustakabali wa wanyamapori nchini pia umekuwa ikidhoofisha usalama wa nchi na umiliki wa rasilimali za wafugaji wa Kimasai.

Mheshimiwa Spika, taasisi za uhifadhi wa wanyamapori zilizoongozwa kwa misingi ya kikoloni, hazikumtenganisha mtu kutoka katika mazingira yake ya asili, kwa kutozingatia yale yaliofanywa na Serikali za kikoloni katika hifadhi hizi mambo ya ulinzi dhidi ya mtu kutozingatiwa na kusababisha binadamu kutengwa na makazi yao moja kwa moja hususani jamii za kimasai katika maeneo ya Ngorongoro na raslimali zao za asili kuchukuliwa na wao kuachwa pasipo kupewa ardhi mbadala kwa matumizi ya shughuli zao za ufugaji.

Mheshimiwa Spika,wakati hoja ya kuundwa kwa maeneo ya hifadhi kama vile Eneo la hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kipindi cha utawala wa kikoloni ni dhahiri serikali ya kikoloni ilipata kigugumizi cha kufanya maamuzi ya kutowashirikisha wamasai katika mchakato,lakini waliweza kuwashirikisha wanajamii ya kimasai na kuamua kwa pamoja juu ya uanzishwaji wa eneo la hifadhi pasipo kuwepo malumbano na serikali ya kikoloni, hivyo tofauti tunayoiona sasa ni jinsi serikali ya kikoloni ilivyotii na kuheshimu jamii za kimasai na kuwaacha wakiendelea na maisha yao. 


BOFYA READ MORE KUENDELEA

Monday, April 29, 2013

ZITTO KABWE ASIGINA BAJETI YA WIZARA YA MAJI ILIYOONGEZEWA BIL.184.5

Baada ya bajeti ya Wizara ya maji kuongezewa kiasi cha Tsh.bilioni 184.5 kama ilivyokuwa imeshauriwa na kamati ya bunge hapo awali,bado mgawanyo wa kifedha kwenye bajeti hiyo umeonekana kutokuwa na usawa kulingana na mgawanyo wa watu kati ya mijini na vijijini.
Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh.Zitto Kabwe (CHADEMA) ametoa muhtasari wa mgawanyo wa kifedha katika bajeti hiyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kama ifuatavyo:- 
"Maji Bajeti yake ya 2013/14 licha ya nyongeza ya tshs 184.5 bilioni, bado mgawanyo wa Bajeti ya Maji umeegemea sana mijini. Kabla ya nyongeza ya bajeti, miradi ya mijini ilikuwa imepangiwa tshs 254bn wakati miradi ya vijijini ilipangiwa tshs 75bn tu. Baada ya kelele za Wabunge, miradi ya vijijini imepangiwa tshs 237bn wakati mijini imepanda mpaka tshs 266bn. Watanzania 74% wanaishi vijijini, lakini mgawo mkubwa unakwenda mijini. Lazima sasa tuweke uwiano wa mgawo wa rasilimali za kibajeti kulingana na wapi wapo Watanzania wengi. Watu wa vijijini wanaminywa sana. Mwalimu aliwahi kuonya kuwa "tusisahau maendeleo ya vijiji" tusiruhusu miji kunyonya vijiji kimaendeleo."

WATU 19 WAUAWA IRAQ

Bendera ya Iraq.
Watu 19 wameuwa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya mabomu matatu ya kutegwa kwenye gari kuripuka leo kwenye miji miwili ya Iraq, yenye wakaazi wengi wa waumini wa Kiislamu wa madhehebu ya Kishia.
Shambulio hilo limetokea kwenye miji ya Amarah na Diwaniyah, huku kukiwa na mfululizo wa ghasia za kidini kufuatia mapigano kwenye kambi ya Waislamu wa madhehebu ya Suni, kaskazini mwa Iraq.
Ghasia za kimadhehebu, zimeongezeka tangu Jumanne iliyopita, wakati vikosi vya usalama vilipojaribu kuwakamata waandamanaji katika kambi ya Waislamu wa madhdhebu ya Sunni kwenye mji wa Hawija. Hatua hiyo ilisabisha mauaji ya watu 32, wakiwemo wanajeshi watatu. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na mashambulio ya leo.

Chanzo: Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani

JOB VACANCIES- EAST AFRICAN COMMUNITY.

BOFYA HAPA KUPATA MAELEZO YA NAFASI ZA KAZI
Nafasi za kazi zifuatazo zimetangazwa:-

Principal Health Officer,

Senior e-Health & Informatics Officer,

National Open Health Initiative Officer,

Health Statistics & Data Management Assistant,

Programme Officer,

Monitoring & Evaluation Officer,

Knowledge Management & Communications Officer,

Programme Accountant,

Programme Administrative Assistant 


 



JACOB ZUMA AKUTANA NA TIANGAYE PRITORIA.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa mwezi Machi wakati wapiganaji walipoiteka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo.

Chanzo: BBC

KIPANYA NA BODA BODA ZA BONGO

Saturday, April 27, 2013

DIAMOND AWASILI SALAMA UINGEREZA KWA AJILI YA SHOO.

Baada ya Msanii Nasibu maarufu Diamond kuwasili salama huko Uingereza tayari kwa shoo anayotarajia kuanza kuionyesha leo ameandika maneno yafuatayo kwenye mtandao wake wa kijamii:-
"Napenda kumshukuru mungu kwa siku ya leo....... Jumamosi mwanana.....nikiwa mbali na uso wa nyumbani, nikiwa ugenini kutafuta riziki......Shukrani za pekee pia kwenu mashabiki zangu wa dhati....mahana bila nyinyi si Mimi.....Nashukuru mungu kwa ulinzi wake... nipo salama salimini kwenye jiji la Malkia elizabeth....nashukuru uongozi mzima kwa  mapkezi mazuri na huduma nzuri mimi na dancers wngu.......!!

Nashukuru mungu kwa brekfast mwanana niliyopata na kunifanya nijiskie mwenye hari zaidi...kabla ya kuanza kukatiza mitaa ya jiji ili leye watu zaidi ya maelfu ya wanachi wanaotokea nchini mbalimbali duniani....!!"


Na hizi ndo picha mbali mbali za Diamond akiwa Ughaibuni hii leo.


Picha kwa hisani ya Mtandao wa kijamii wa Diamond.

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA


                                            JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
                                         WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
                                                            TANGAZO LA KAZI

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa wote wenye taaluma za Kada za Afya ambao wako tayari kufanya kazi katika Utumishi wa Umma.
Vigezo na Masharti:
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Watumishi wa Kada za Afya waliojiendeleza wakiwa kazini wasitume maombi bali waombe kwa waajiri wao kubadilishwa vyeo kulingana na sifa walizopata.
4. Watumishi ambao walikwishapangiwa vituo vya kazi miaka ya nyuma na hawakuripoti au kuacha kazi hawatapangiwa vituo vya kazi, kwa sababu hawataweza kuingia kwenye ‘Payroll’ ya Serikali.
5. Maombi yote yaambatanishwe na:- Nakala ya Cheti cha Taaluma, Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita, Maelezo binafsi (CV), Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni, Nakala ya cheti cha usajili.
6. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au Wakili anayetambuliwa na Serikali.
7. Waombaji wanatakiwa kuchagua/kupendekeza maeneo matatu (Mikoa na Halmashauri) ambayo wangependa kupangiwa kazi kwa kuzingatia nafasi zilizoainishwa kwenye Kibali (Tazama Tovuti ya Wizara).
2
Waajiri wote wanatakiwa kuharakisha zoezi la kuwaajiri na kuwaingiza kwenye ‘Payroll’ ya Serikali wataalam wote watakaopangiwa vituo vya kazi kwenye mamlaka zao ikiwa ni pamoja na kuwalipa posho za kujikimu kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima watumishi husika.
Aidha, Waajiri wanakumbushwa kukagua na kuthibitisha uhalali wa vyeti vya kidato cha Nne na Sita vya wataalam hao kabla ya kuwaajiri.
Kwa utaratibu wa mwaka huu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hatatoa barua za kupangiwa Vituo vya kazi. Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz). Ukiona jina lako kwenye Tovuti au Gazeti nenda karipoti kwenye kituo ulichopangiwa kabla ya tarehe 25 Juni, 2013 ambako taratibu za ajira yako zitakamilishwa.
Maombi yote yatakayowasilishwa kwa mkono au barua pepe hayatafanyiwa kazi.
Barua zote zitumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Mei, 2013.
Tangazo hili pamoja na mchanganuo wa nafasi za kazi vinapatikana katika tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz)

YANGA BAADA YA KUWA BINGWA WA LIGI KUU YAENDELEA NA MAZOEZI YA "GYM" KUIKABLI COASTAL UNION.

Pamoja na jana kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013, kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi ya viungo na kujenga misuli (GYM) katika kituo cha mazoezi kilichopo jengo la Quality Cetntre kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo jana imetangazwa rasmi kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013 baada ya timu za Coastal Union na Azam FC kutoka sare ya bao 1-1, imeendelea kujifua kuhakikisha inamalizia mzunguko wa pili wa VPL kwa ushindi kama ilivyofanya tangu kuanza duru la pili.
Azam FC iliyokua na ndoto za kuweza kufikia pointi 56 za Yanga, ilikua ikiombea yenyewe kushinda michezo yake yote mitatu huku iikiombea Yanga kupoteza michezo yake miwili iliyosalia hali ambayo ilikwenda kinyume hapo jana kwa wauza mikate kupata sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union na kuifanya Yanga itangazwe mabingwa wapya wa VPL kwa kuwa na ponti 56 ponti 8 mbele ya Azam yenye pointi 48. 
Huu unakua ni Ubingwa wa 24 kwa Yanga tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania bara rekodi ambayo hakuna timu yoyote inayokaribia kufuatia watani wa jadi Simba SC kuwa wametwaa ubingwa huo mara 18 tu.
Rekodi ya Ubingwa wa Yanga :1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013 
Baada ya kufanya mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya jumatano, jana wachezaji waliingia kambini katika hosteli za klabu zilizopo makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo wa jumatano.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amekiongoza kikosi cha wachezaji 26 kufanya mazoezi ya gym leo katika kituo cha Quality Centre ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Coastal Union siku ya mei mosi jumatano  katika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam.
Yanga imebakisha michezo miwili (Costal Union 01.05.2013) na (Simba SC 18.05.2013) kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodaom huku ikiwa tayari imeshatwaa Ubingwa mapema kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom. 
Uongozi wa klabu ya Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya jumatano (mei mosi) katika dimba la uwanja wa Taifa ili kuja kuwashangilia vijana wakiendeleza furaha ya kutwaa Ubingwa wa VPL msimu huu.
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD, BACKWARD NEVER (EFBN) 

Chanzo: Mtandao wa kijamii wa Timu ya Yanga.

CHADEMA KUWASHA MOTO TABORA MJINI LEO,MNYIKA AMUANIKA NDUGAI KWA WAPIGA KURA WAKE.

Mh.Zitto Zuberi Kabwe.
Ikiwa ni katika muendelezo wa M4C na ufunguzi wa kanda ya magharibi, ambapo inatarajiwa kufanyika leo tarehe 27 Aprili 2013 ktk viwanja vya shule Town school karibu na kwa Papa Wemba Tabora mjini,Tayari viongozi wa kitaifa wameanza kuwasili usiku wa leo ambapo tayari Mhe. Zitto Kabwe ambaye ni mlezi wa kanda hiyo ameshawasili tayari kwa kuwasha moto wa kufa mtu leo ambapo tutakwenda kushuhudia Tabora kuwa kama Arusha kwa muamko kwani vijana wengi na wakazi wa hapo wana hamasa kubwa ya kufika ktk mkutano huo ili kukata kiu yao ya muda mrefu ya kukosa elimu ya uraia.

KUSHITAKIWA KWA NDUGAI.
 
Katika upande wa pili,Naibu Spika Mh.Jobu Ndugai ameshitakiwa kwa wapiga kura wake na Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwahoji iwapo walimtuma bungeni kufanya Ubabe wa  kuwatoa nje wabunge wenzie badala ya kuwatetea.
Mnyika alitoa Mashitaka hayo jana Aprilli 26, 2013 katika kijiji cha Iyegu, Kata ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, ambapo alisema amemkatia Rufaa Ndugai mara Tano bungeni bila majibu, kwa hiyo jana aliamua kumshitaki kwao ili wafanye maamuzi magumu juu ya mbunge wao asiyefanya kazi waliyomtuma.
Akizungumza katika Mkutano huo Mnyika alimshitaki Ndugai akiwahoji kama walimtuma kufanya hivyo, na waliposema Laa, aliwataka kufanya mabadiliko ya mwakilishi wa Jimbo lao kama wanataka kumaliziwa Kero zao zikiwepo Haki na Maendeleo ya kiuchumi na Matumizi bora ya Rasilimali zao.
Mwananchi mmoja alimhoji Mnyika “Je, ni nani aliyetayarisha, kulinda, kusimamia na kusafirisha Twiga wetu kwenda nje, lini watarejeshwa na waliohusika watafanywaje?.
Mnyika aliwajibu wananchi kwamba, wahusika wa usafirishaji wa Twiga wao ni vigogo walioko madarakani, na Twiga hao wako nchi mmoja ya Kiarabu, na mbali ya Twiga hao hivi karibuni Chadema itaibua suala la Tembo, na kuwaambia suluhisho la haraka kwa yote hayo ni kufanya mabadiliko ya viongozi mafisadi haraka.
Alipoulizwa Mauaji na Vitisho wanavyofanyiwa na Kundi linalojiita Kanyaga Twende, wanapoamua kujiunga na  vyama Upinzani, Mnyika aliwauliza kama wanayo simu ya Mbunge wao wamuulize ila wasimtukane, na waliposema hawana aliwatajia namba ya Ndugai na ya Mkurugenzi wa Usalama Chadema ambaye alidai atawawasaidia dhidi ya vitisho .
Aidha Mnyika kabla ya kushuka Jukwani saa 11.30 jioni, aliuuliza umati uliokuwepo uwanjani hapo, wangapi wapo tayari kwa mabadiliko ya M4C, watu wote karibu 1,000 walinyosha mikono na Mnyika akashuka kuelekea Kongwa kuungana na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, kuendelea na Mikutano mingine.
 
Chanzo:Mtandao wa Kijamii wa CHADEMA.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...