Friday, April 26, 2013

TAMKO LA MH. GODBLESS LEMA

Mh.Godbless Lema.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana majira ya saa nne asubuhi nilipokea taarifa kutoka Chuo cha Uhasibu juu ya tukio la mauaji ya mwanafunzi yaliyotokea jana usiku kwa kuchomwa kisu eneo karibu na chuo , nilipita Chuoni hapo baada ya kusikia taarifa hiyo , nilikuta Wanafunzi wengi sana wakiwa wamekusanyika pamoja wakiwa na jazba huku Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya akijaribu kuwasihi watulie wakati walipokuwa wanatafuta muafaka wa kuzuia jazba ambayo ilikuwa ina lengo la kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa.

Nilipata faragha ya kuongea na Mwalimu aliyekuwa pale ( Dean of Student ) pamoja na OCD na wote walinieleza tatizo lilivyoanza na kuomba nitumie busara kuzuia jazba na maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa kuelekea kwa Mkuu wa Mkoa niliongea na wanafunzi na niliwasihi watulie na nilifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa na kwa bahati nzuri nilimpata Mkuu wa Mkoa na kumweleza juu ya kifo hicho na kile ambacho wanafunzi wanakusudia kufanya kuandamana kwenda ofisini kwake. Nilimuomba afike ili aweze kutuliza hali hile na pia atoe kauli juu ya tukio hilo baya la kuhuzunisha kwani ikizingatiwa kuwa ni zaidi ya mara moja matendo kama haya yamekuwa yakitokea na hakuna hatua zozote zimekuwa zikichukuliwa kuwahakikishia Wanafunzi Usalama wao na mali zao.

Mkuu wa Mkoa pamoja na mimi kumpa taarifa mapema aliahidi kufika mapema jambo ambalo halikufanyika na wanafunzi walianza kuwa wakali na nilifanya jitihada na hekima za hali ya juu kuvuta subira za wanafunzi hao ili Mkuu wa Mkoa afike . Baada ya Mkuu wa Mkoa kufika Makamu wa Chuo aliniomba niwaandae wanafunzi kumsikiliza Mkuu wa Mkoa na yeye alikwenda kumchukua Mkuu wa Mkoa na kumpa mukutasari wa tukio zima na hali halisi ya kilichokuwa kinaendelea na kimsingi Mkuu wa Mkoa alipofika Wanafunzi walitaka apande juu kuongea mahali ambako tulitumia kama jukwaa kwa maongezi wakati wote lakini badala yake mambo yafuatayo yalianza kutokea 

1) Mkuu wa Mkoa alikataa na kunitaka nishuke chini mahali alipokuwa yeye na timu yake ya ulinzi na usalama Mkoa kwa kweli nilitii na nilipotaka kuongea nae alinidharau na kuniambia hawezi kuongea na wanafunzi wahuni wasiokuwa na nidhamu maneno ambayo yaliwatia wanafunzi hasira zaidi na nilimsihi na kumuomba Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (RSO) kumshawishi Mkuu wa Mkoa kukubali kuongea nao kwani hali ilivyokuwa ni dhahiri kwamba wanafunzi wale walikuwa na jazba ya hali ya juu na hivyo hekima na unyenyekevu ndio ilikuwa njia pekee ya kutuliza hali hile. 

2) Mkuu wa Mkoa alitoa masharti kwamba asingeweza kuongea nao bila kipaza sauti na wanafunzi wote waende jengo lililokuwa karibu na Utawala na wakisha kaa atakuja kuongea nao jambo ambalo wanafunzi waligoma kwa imani kwamba jengo hilo lisengeweza kuchukua wanafunzi wengi na mimi niliaga naondoka kwenda msibani na wanafunzi waligoma nisiondoke mpaka watakapo sikilizwa na kwa kweli nilitii maombi baada ya kunizuia na kukaa mbele ya gari yangu.

3) Tulipokwenda eneo la kukutania na mara hii ilikuwa ni nje jirani ya jengo la utawala wanafunzi walikusanyika wakimsubiri Mkuu wa Mkoa na kabla hajafika nilitwa na yeye mwenyewe ili tuweke msimamo wa pamoja kama viongozi lakini badala yake alitumia Polisi kunitisha na kuhaidi kuwa nitamtambua kuwa yeye ni Serikali ,tulitofautiana tena nilipokataa hofu hiyo na ghafla tuliamua kwenda eneo la kuongea na wanafunzi na ndipo yafuatyo yalitokea “

Mkuu wa Mkoa wakati anaanza kuongea alianza kusema maneno yafuatayo “ Mnaona hiki Kifua na huu mwili wangu , na hapo ndipo hali ilipochafuka na kuamsha vurugu kubwa kutoka kwa Wanafunzi waliokerwa na kauli yake na Polisi wa walimchukua na tafrani kati ya Polisi na Wanafunzi ikapamba moto hali iliyosababisha mabomu ya machozi kulipuliwa kwa wingi kila kona ya chuo na kila mtu kuanza kukimbia kuangalia usalama wake nikiwemo mimi .
Nimesikiliza Mkutano wake na Waandishi wa Habari na leo nimesoma nakusikiliza vyombo mbali mbali vya habari kwamba ninatafutwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa , nimeshangaa sana japo sio kumshangaa Mkuu huyu wa Mkoa kwani ufahamu na uwezo wake naujua ulivyo katika kufikiri na kutatua mambo ya msingi na muhimu , kwa jinsi nilivyomsikia na kumuona alivyokuwa anashughulikia tatizo lile lililotukutanisha jana pale Chuoni , kwa kweli nilishangazwa sana na kuogopa kama hekima ya Mkiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa angeweza kushughulikia tatizo lile kwa namna ile ya Kiburi , Dharau na Majivuno ambayo hakika ilikuwa ni chanzo cha wanafunzi kukataa kumsikiliza na ndipo alipoamua kuondoka huku zomea zomea ikiendelea kushamiri vizuri . Mabomu yalianza kupigwa , wanafunzi walipigwa na kunyang’anywa pesa , simu , na lap top na vitu mbali mbali ambavyo Polisi walikuwa wanaona vina thamani kwao , nilikuwa ninatazama mambo haya huku roho yangu ikiwa inauma sana kwamba wanaopaswa kulinda usalama wa raia na mali zao ghafla waligeuka kuwa vibaka wa kuumiza raia na kupora mali zao .

Ninawapa pole wanafunzi kwa msiba wa rafiki yao na siku ya jana ilikuwa ni siku ya Serikali kutumia busara kurudisha matumaini kwa wanafunzi wale pamoja na raia , lakini badala yake wafiwa walipotaka kudai haki zao za kulindwa , walipigwa , walidhalilishwa na Chuo chao kufungwa bila sababu ya msingi wala kuzingatia mambo muhimu .

Ifahamike kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha kina wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii, na amri ya mkuu wa mkoa kufunga chuo na kuamuru wanafunzi watawanyike ifikapo saa kumi na mbili jioni , huu ni ukosefu wa upendo , hekima , busara na utu ikizingatiwa kuwa sababu na mchochezi wa vurugu hizi ni Mkuu wa Mkoa kukosa maarifa na hekima.

Nimepokea ujumbe katika simu yangu kutoka kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa inayonitishia na kuweka maisha yangu kwenye hali ya hatari na ujumbe huo unasema “ UMERUKA KIHUNZI CHA KWANZA , NITAKUONYESHA KUWA MIMI NI SERIKALI ULIKOJIFICHA NITAKUPATA NA NITAKUPA KESI NINAYOTAKA MIMI “ Mwisho wa kunukuu .

Mwisho, Ninamshukuru kijana aliyerekodi tukio lote kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hivi tutanza kusambaza video cd hizo Nchi ili watanzania wajue ukweli na Mh Rais aone utendaji mbovu wa wateule wake na vile nilitake Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria , maadili ,taratibu na kanuni za kazi na sio kuendesha Jeshi kwa matakwa ya kisiasa , kufanya hivi ni kuhatarisha usalama na utulivu wa Nchi yetu . 

“ Che Guavera alisema “ if you tremble indignation at every injustice then you are a comrade of mine “ 

Wanafunzi jipeni moyo bado kitambo kidogo Taifa hili litabadilika .


Godbless J Lema ( MP) 


25/4/2013.


Chanzo: Mtandao wa kijamii wa CHADEMA.

Thursday, April 25, 2013

UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA JUU YA AZIMIO LA MALI


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio linalopendekeza kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani nchini Mali.
Kikosi hicho chenye wanajeshi 12,600 kinajumuisha takriban wanajeshi 6,000 kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika ambazo tayari zina wanajeshi wao nchini humo.
Azimio hilo limependekezwa na Ufaransa ambayo iliingilia kati mzozo wa Mali mnamo mwezi Januari ili kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Mali mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya uchaguzi mkuu.
Hata hivyo duru zinasema kuwa azimio hilo limezua mjadala mkali.
Makundi ya kiisilamu yaliweza kutumia pengo la usalama lililotokea baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka jana na kuanza kushinikiza watu kufuata sheria za kiisilamu.
Miji iliyo Kaskazini mwa nchi, imeweza kudhibitiwa na jeshi la Ufaransa lakini baadhi ya wapiganaji wangali katika maficho yao.
Ufaransa ilianza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000 mapema mwezi huu kutoka nchini humo, lakini imekuwa ikishinikiza Umoja wa Mataifa kupeleka wanajeshi wake.
Aidha wanajeshi wa Chad, wanasemekana kuwa wenye uzoefu mkubwa zaidi katika kupambana na wapiganaji jangwani, lakini nchi hiyo pia imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali.
Sababu ya kikosi cha Umoja wa mataifa ni kulinda amani na kitakuwa na wanajeshi 11,200, pamoja na polisi 1,440.
Lengo lake kuu litakuwa kuweka uthibiti katika baadhi ya sehemu za Kaskazini mwa Mali ili kumaliza vitisho kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Hata hivyo rasimu ya azimio hilo haisemi ikiwa wanajeshi hao wataweza kupigana na wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, lakini wanajeshi 1,000 wa Ufaransa,wataweza kusalia Mali.

Chanzo :BBC

KIPANYA LEO NA BUNGE LA TANZANIA

TAFAKARI,CHUKUA HATUA.

RAIS UHURU KENYATTA AZIDI KUTANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameendelea kulitangaza baraza lake la mawaziri. Katika uteuzi wa leo, Balozi Raychelle Omamo, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, huku Phylis Kandie akiteuliwa kuwa waziri wa uhusiano wa Afrika Mashariki na Utalii. Wengine walioteuliwa ni Charity Ngilu, ambaye atakuwa waziri mpya wa nyumba na makaazi, pamoja na Najib Balala, atakayekuwa waziri wa madini.Jumanne iliyopita, Rais Kenyatta, aliwateuwa mawaziri wanne, akiwemo Amina Mohamed, ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na Henry Rotich, aliteuliwa kuwa waziri mpya wa Fedha. Wiki iliyopita Rais Kenyatta alielezea muundo wa baraza lake utakavyokuwa, kwa kulipunguza baraza hilo kutoka mawaziri 44 hadi kufikia 18.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI YA UJERUMANI

SHEREHE ZA MUUNGANO ZAAHIRISHA MCHEZO WA SIMBA vs RUVU SHOOTING

TANGAZO
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

SERGIO RAMOSI ACHEZA MCHEZO WA 350 AKIWA NA REAL MADRID


Sargio Ramos akiwa anakabiliana na mchezaji wa Borrusia Dortmund katika mchezo wa jana Madrid
Beki wa kutumainiwa wa Real Madris Sergio Ramos akicheza mchezo wa jana akiwa na timu yake wakati wanacheza na Borrusia Dortimund amefikisha michezo 350 akiwa na Real madrid.
Jana akiwa mchezoni katika mchezo wa jana kama nahodha wa Real Madrid,ameandika historia hiyo katika maisha yake ya kisoka na takwimu zifuatazo zinafafanua zaidi:-
SERGIO RAMOS’ 350 MATCHES
Season League European Cup Copa del Rey Spanish Super Cup TOTAL
2005/06  33  7  6 -  46
2006/07  33  6  3 -  42
2007/08  33  7  3 2  45
2008/09  32  8  0 2  42
2009/10  33  7  0 -  40
2010/11  31  8  7 -  46
2011/12  34 11  4 2  51
2012/13  26  8  2 2  38
TOTAL 255 62 25 8 350

MAANDAMANO YATEKETEZA NYUMBA 20 LIWALE

Mh.Faith Mitambo Mbunge wa Liwale (CCM)
Takriban nyumba 20 zimeteketezwa katika maandamano yaliyofanywa na wakulima wa Korosho pamoja na waandamanaji wengine Kusini mwa Tanzania.Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo.
Mbunge huyo, Faith Mitambo alisema kuwa majengo mawili nyumbani kwake mjini Liwale, yalichomwa na kuwa nyumba zingine mali ya baadhi ya wanachama wa chama tawala CCM ziliteketezwa.
Uharibifu huo ulianza baada ya wakulima kulipwa kiasi kidogo cha pesa ikilinganishwa na zile walizokuwa wamekubaliana kulipwa na serikali baada ya kuiuzia mazao yao mwaka jana.
Polisi zaidi wamepelekwa katika eneo hilo kuzuia ghasia zaidi.
Bi Mitambo, aliyekuwa mjini, Dodoma, wakati huo aliambia BBC kuwa alikuwa anazuru eneo bunge lake kudadisi hali ilivyo.
Alipokea habari kuwa waandamanaji waliokuwa wanajumuisha vijana , walianza kufanya fujo vijijini mnamo Jumanne asubuhi hadi walipofika mjini Liwale saa za jioni.
Mkaazi mmoja wa mji huo aliambia BBC kuwa mnamo Jumatano kulikuwa na hali ya wasiwasi mjini humo na kwamba polisi walikuwa wamewarushia gesi ya kutoa machozi wandamanaji ili kuwatawanya.
Maelfu ya wakulima wadogo wadogo wanaopanda Korosho nchini Tanzania na ambao huvuna mazao yao mwezi Oktoba, huyauza kwa mashirika mbali mbali kwa bei waliyokubaliana.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam, Erick Nampesya anasema kuwa wakulima walikubaliana kulipwa shilingi 1,200 pesa za Tanzania kwa kila kilo ya korosho hizo.
Mwishoni mwa mwaka jana, wakulima walilipwa sehemu ya deni lao.
Lakini pale waakilishi kutoka kwa mashirika walipokwenda katika wilaya ya Liwale, kuwalipa sehemu ya mwisho ya deni lao, wakawa wamebadilisha makubaliano waliyokuwa wameafikiana.
Wakulima walilipwa nusu au chini ya nusu ya deni lililokuwa limesalia, baada ya kuambiwa kuwa bei ya Korosho ilikuwa imeshuka sana katika soko la kimataifa.
Wanasiasa wakuu ambao wakulima hao wanawalaumu kwa kukosa kuwasaidia ndio walikuwa wamewaelekezea ghadbabu zao
Wakulima wamekuwa wakilalamika kuhusu msukosuko wa bei za Korosho ambayo huathiriwa zaidi kulingana na msimu.
CHANZO : BBC

WATU 147 WAUWAWA KATIKA MKASA BANGLADESH

Maafisa nchini Bangladesh wamesema idadi ya waliofariki katika mkasa wa jengo kuporomoka imefikia 147 huku maafisa wa uokozi wakifanya kazi usiku kucha kutafuta watu waliokwama katika vifusi vya jengo hilo.Jengo hilo la orofa nane liliporomoka hapo jana asubuhi viungani mwa mji mkuu Dhaka katika eneo la Savar na inahofiwa mamia ya watu bado wamekwama chini ya vifusi vya jengo hilo lililokuwa na viwanda vya nguo.
Mashirika ya habari nchini humo yanaarifu kuwa watu waliripoti kuweko kwa nyufa kubwa katika jengo hilo siku moja kabla ya mkasa huo lakini wasimamizi wa jengo hilo inadaiwa hawakuchukua hatua zozote.Mkuu wa polisi katika eneo hilo Mohammed Asaduzzaman amesema polisi na baraza la mji huo wamewasilisha kesi tofauti dhidi ya mwenye jengo hilo kwa kutozingatia usalama.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI YA UJERUMANI

CHADEMA WAITEKA MBEYA,WAMUONYA RAIS ASIIPIGIE DEBE CCM

Dr.Slaa akihutubia umati mkubwa katika mkutano jijini Mbeya.
  Katika kuendelea na ziara yao katika mikoa mbali mbali wabunge wa CHADEMA waliosimamishwa bungeni,jana wameendelea na ziara yao na kufanya mkutano mkubwa ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu mjini Mbeya.
Katika mkutano huo CHADEMA walimtahadharisha Rais kutokipigia debe Chama cha Mapinduzi.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi(Sugu) akihutubia mjini Mbeya.
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) 
bali afanye kazi za kiserikali.
Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya,Sugu alisema kuwa kitendo hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.
“Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.
Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda-Nzovwe, ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa, Mbunge wa Iringa, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa mjini), Ezekiel Wenje(Mwanza mjini) na Highness Kiwia wa Jimbo la Ilemela. Sugu pia alitoa miezi mitatu kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha Soko Jipya la Mwanjelwa linakamilika ifikapo Julai mwaka huu.

Alitishia iwapo kufikia muda huo halijakamilika yeye na wananchi wenzake watavamia soko hilo na kufanya kazi za ujenzi wenyewe.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, Peter Msigwa alisema kuwa wamejipanga kufanya maamuzi magumu kama Spika wa Bunge, Anne Makinda
ataendelea kuwapendelea wabunge wa CCM.

Dk Willbroad Slaa alisema sababu ya wabunge wa Chadema kufukuzwa bungeni ni
kutokana na kutekeleza majukumu waliyotumwa na wananchi.
Aliwataka Wananchi kuendelea kuwaunga mkono na watambue kuwa CCM na Serikali yake inafanya kazi ya kutetea ubovu wa Serikali na kuwafanya Watanzania kuwa katika hali ya
umasikini huku walionacho wakizidi kuneemeka.

 
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliosimamishwa bungeni wiki iliyopita wameamua kwenda kuwashitaki Spika Anna Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwa wananchi kwa njia ya kuitisha mikutano ya mihadhara.
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa CHADEMA.
 

Wednesday, April 24, 2013

REAL MADRIL YATOTA UJERUMANI,YAPIGWA 4-1 NA BORRUSIA BOTMUND

 Timu ya Real Madrid  ya Hispania ikicheza katika mchezo wa nusu fainali ya pili imekumbana na dhahama ya kufungwa na Borrusia Dotmund goli 4 kwa 1. Matokeo haya yanatofautiana kidogo na yale waliyopata wahasimu wao wakuu Barcelona iliyofungwa 4-0 jana na Bayern Munchin.
Kwa matokeo haya,ili Real Madrid aweze kufuzu kucheza fainali katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Hispania wanatakiwa washinde 3-0.

Timeline

soundEnable
Borussia Dortmund
Borussia Dortmund4 - 1Real Madrid
  • R. Lewandowski 8
  • R. Lewandowski 50
  • R. Lewandowski 55
  • R. Lewandowski 67 (P (penalty))
  • C. Ronaldo 43
Real Madrid
Borussia DortmundEvents
  • Goal: Robert Lewandowski 8min (minute symbol)
  • Goal: Robert Lewandowski 50min (minute symbol)
  • Goal: Robert Lewandowski 55min (minute symbol)
  • Penalty: Robert Lewandowski 67min (minute symbol)
  • Substitution: Sebastian Kehl (In) / Jakub Blaszczykowski (Out) 82min (minute symbol)
  • Substitution: Kevin Großkreutz (In) / Lukasz Piszczek (Out) 83min (minute symbol)
  • Substitution: Julian Schieber (In) / Ilkay Gündogan (Out) 90+2min (minute symbol)
  • Yellow Card: Robert Lewandowski 70min (minute symbol)
Real MadridEvents
  • Goal: Cristiano Ronaldo 43min (minute symbol)
  • Substitution: Karim Benzema (In) / Gonzalo Higuaín (Out) 68min (minute symbol)
  • Substitution: Ángel Di María (In) / Luka Modric (Out) 68min (minute symbol)
  • Substitution: Kaká (In) / Xabi Alonso (Out) 80min (minute symbol)
  • Yellow Card: Sami Khedira 54min (minute symbol)
  • Yellow Card: Mesut Özil 64min (minute symbol)
  • Yellow Card: Sergio Ramos 90+2min (minute symbol)
min (minute symbol)
Competition
Champions League
KO (kickoff)
24 Apr 2013 20:45
REF (referee)
Bjorn Kuipers
AT (venue)
Signal Iduna Park
FT (fulltime)

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...