Thursday, December 18, 2014
Wednesday, December 17, 2014
WAKURUGENZI 6 WAFUKUZWA KAZI KWA KUBORONGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, AISHA MADINDA AFARIKI.
WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia |
WaziriI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Hawa Ghasia leo amewavua madaraka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliua, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda kufuatia kasoro za uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba, 14 mwaka huu. Wakurugenzi wengine watano (5) bado wanachunguzwa.
Aidha Waziri Ghasia amesema kuwa hawezi kujiuzulu kama alivyoahidi baada ya watendaji waliozembea kugundulika.Kifo cha Madinda.
Msanii mnenguaji wa bendi ya Extra Bongo, Aisha Mbegu "Madinda" amefariki leo mchana katika Hospitali ya Mwananyamala na chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika.
Kwa taarifa zaidi, endelea kutembelea blogu hii.
KAGERA KUJIVUNIA UWANJA WA NDEGE WA KISASA
Na Saidi Mkabakuli, Kagera
Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani wataanza kujivunia uwanja wa ndege wa kisasa kufuatia kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
Akizungumza na Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kagera, Mhandisi Suleiman Athuman, amesema kwamba maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la kiwanja hicho upo kwenye hali nzuri na mkandarasi atabidhi kazi hiyo mapema mwakani.
“Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 kazi zilizopangwa ni ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja, ikijumuisha barabara ya kuruka na kutua ndege, maegesho ya ndege, barabara ya kiungio, kwa sasa ujenzi unaendelea vizuri na Mkandarasi atatukabidhi kazi mapema mwakani,” alisema Mhandisi Athuman.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa kiwanja hiko, Mhandisi Pius Gobolo amesema kuwa kazi za usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege, ujenzi wa jengo jipya la abiria na uzio wa usalama zimeshakamilika kwa asilimia 80.
Friday, December 12, 2014
SUALA LA ESCROW, TANZANIA YABANWA ZAIDI.
MCC Statement on Board of Directors’ Discussion of Tanzania at the December 2014 Meeting
Washington, D.C.—The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) issued the following statement after its Board of Directors (Board) held its annual country selection meeting on December 10, 2014:
“MCC takes seriously all of its country partners’ commitments to combat corruption. At today’s meeting, MCC’s Board expressed continued concern over corruption in Tanzania, including the implications of the recent case involving Independent Power Tanzania Limited (IPTL). The Board noted that Tanzania has experienced a significant decline over the past seven years on the key indicator measuring efforts to control corruption. While the Board voted to allow Tanzania to continue working to develop a compact proposal—given its passage on MCC’s policy scorecards and its strong previous performance as an MCC partner—the Board stated its expectation that the Government of Tanzania must take firm, concrete steps to combat corruption before a compact is approved. Further, the Board voted to continue MCC’s engagement with Tanzania with the understanding that, in accordance with the Tanzanian State House December 9 statement, the Tanzanian government would act promptly and decisively on the late November parliamentary resolutions regarding IPTL. The Board also reaffirmed more broadly that Tanzania must undertake a series of previously agreed upon structural reforms to improve the efficiency, effectiveness and transparency of the energy sector, and more generally to deal with wider corruption.”
Source: http://www.mcc.gov
KATIBU MKUU KIONGOZI AMUAGA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI, BW. LUDOVICK UTOUH, NA KUMKARIBISHA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU MPYA WA HESABU ZA SERIKALI PROFESA MUSSA JUMA ASSAD, ALHAMIS, 11 DESEMBA 2014
Chanzo : Ikulu
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 11 Desemba 2014, amemuaga rasmi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovick Utouh, katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya Watendaji Wakuu na Waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuwa mahsusi pia kumkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.
Katika hotuba yake ya kumpongeza Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alielezea historia ya Utumishi uliotukuka ya Bw. Utouh ambayo imeleta sifa kubwa Ofisi hiyo ndani na nje ya nchi na katika medani za kimataifa. Kwa ujumla, hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi ilijikita kuelezea mchango binafsi wa Bwana Utouh kwa taifa ndani ya miaka zaidi ya arobaini (40) ya Utumishi wake Serikalini.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea mafanikio ya Serikali kwenye eneo la utawala bora, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za umma ambayo yamechangiwa na Bw. Utouh. Balozi Sefue aliwasihi watumishi wa umma kuiga weledi, uaminifu, msimamo, bidii na maarifa ambayo Bw. Utouh alivionyesha kwa vitendo katika utumishi wake.
Katibu Mkuu Kiongozi alitumia fursa hiyo pia, kumtakia kila la kheri, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Juma Assad, katika kufanikisha majukumu aliyopewa.
Bwana Utouh alistaafu rasmi nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, tarehe 19 Septemba, 2014 baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba na miezi kumi tangu alipoteuliwa na Rais, tarehe 19 Agosti, 2006
NB: Hotuba Kamili iko katika Tovuti ya Katibu Mkuu Kiongozi.
TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YATEMBELEA MELI YA KIHISTORIA YA MV LIEMBA
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani. |
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri zaidi ya miaka 100.
Mmoja wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.
MIKOA IHAMASISHE UWEKEZAJI WA VIWANDA.
Na Oyuke Phostine - Shinyanga
Serikali imetoa wito kwa Ofisi za wakuu wa mikoa kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda kwenye mikoa yao ili kuweza kukuza uchumi wa mikoa husika na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa wakati akiongoza timu ya wataalam kutoka ofisi hiyo iliyokuwa ikifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali na sekta binafsi katika mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, na Mwanza.
Bw. Sangawe, alisema kuwa Wajibu wa Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza. Alifafanua kuwa, moja ya vipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao utekelezaji wake unaishia 2015/16, ni miundombinu ili kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi.
Thursday, December 11, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)