Chama cha Wananchi (CUF) kimesema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin kusema kuwa Wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa au vinginevyo.
Salmin aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja kwa kuwa wanaona kwamba lengo la kuundwa kwake halina dalili njema kwa siku za usoni.