Thursday, January 9, 2014

TANGAZO LA KAZI UTUMISHI.

BOFYA HAPA

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA HITIRAFU YA UMEME - MOROGORO.

Wananchi wakiwa wanajaribu kuvunja dirisha ili waweze kuzima moto .

Nyumba moja ailiyotambulika kuwa mmiliki wake ni Mama Mkambala mtaa wa Uhuru Manispaa ya Morogoro, jana jioni iliteketea kwa moto baada ya kutokea hitirafu ya umeme. Kutokana na juhudi zilizofanywa na Wananchi kwa kushirikiana na Kikosi cha zima moto, moto uliweza kudhibitiwa usiweze kusambaa kwenye nyumba za jirani. Katika kazi hiyo ya kuzima moto changamoto ilikuwa ni namna ya kuingia ndani ya nyumba baada ya nyumba hiyo kuwa imefungwa.
Hata hivyo, thamani halisi ya mali zilizoteketea bado haijafahamika na hakuna majeruhi yeyote kutokana na moto huo.

Wednesday, December 11, 2013

AJIRA ZILIZOTANGAZWA UTUMISHI DESEMBA ,11.

BOFYA HAPA

JOB VACANCIES- TRAINING AND OUTREACH OFFICERS.

Training and Outreach Officers
(Burkina Faso/Ethiopia/Ghana/Nigeria/Tanzania/Uganda)
Retainer Contract (February 1- December 31, 2014)

ITOCA (Information Training & Outreach Centre for Africa) www.itoca.org is a capacity building organization aimed at enhancing information and communications technology (ICT) skills for African professionals and students in the Sub-Saharan Africa region. ITOCA (formerly, TEEAL Africa office) is an International NGO registered in South Africa. It was established in 1999 as a marketing and support office for Albert R. Mann Library TEEAL program. Now, ITOCA spearheads several ICT for development programs including the TEEAL and Research4Life programmes. The organization is looking for self-motivated and energetic information/ICT professionals based in the six listed countries. The candidates should have excellent research, training, facilitation and presentation skills. They should be friendly, responsible and are able to regularly travel nationally and with the regions for project assignments.

Job description

Friday, December 6, 2013

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2013 HAYA HAPA.

Haya ndiyo makundi ya kombe la Dunia huko Brazil 2013.

MANDELA KUZIKWA JUMAPILI TAR. 15 DESEMBA, 2013.


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde, endelea kutembelea blogu hii.

TANZANIA YATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MANDELA.


Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.Na katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.

HATIMAYE MZEE NELSON MANDELA AIAGA DUNIA .

Nelson Mandela mwaka 2008
Hatimaye Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela aiaga dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuzaliwa mnamo mwaka 1918.
Habari kamili tutazidi kukuletea kadiri tutakavyokuwa tunazipata, endelea kutembelea blogu hii.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...