Tuesday, June 11, 2013

HATIMAYE LWAKATARE APATA DHAMANA.



Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare ameachiwa kwa dhamana ya Shilingi milioni kumi kwa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Masharti mengine ya dhamana yaliyotimizwa ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na pia kuikabidhi mahakama pasi yake ya kusafiria.

HIVI NDIVYO SIMBA SPORTS CLUB ILIVYOJITOA KAGAME CUP.


SCHOLARSHIPS FOR MASTER'S STUDENTS IN SWEDEN, 2014.


University of Skovde offers Scholarships IPK/UHR for international master’s students liable for tuition fees. The scholarships are tuition fee waivers of SEK 60 000 / year (50% of the tuition fee). The amount of the scholarships will be deducted from the tuition fee when applicants receive the invoice. Students have to be able to finance the rest of the tuition fee themselves and to cover all the living expenses during their stay in Sweden. Prior to applying for a scholarship students first apply for studies at University of Skövde. Applicants must also apply for one of the master’s programmes at the Swedish official online application service University Admissions. The scholarship application deadline for the master’s programmes that start in the spring semester (January 2014) is September 15th, 2013.


Monday, June 10, 2013

GAKONDO GROUP- KIGALI RWANDA KUACHIA ALBUM MPYA.

Kikundi maarufu cha ngoma za kiutamaduni na asili nchini Rwanda - Kigali kinachoitwa Gakondo Group, ambacho ni moja kati ya vikundi maarufu kinachoongoza nchini humo wapo mbioni kutoa albamu yao ya kwanza kabisa kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.

Kiongozi wa kikundi hicho Intore Masamba, ameelezea kuwa hivi sasa albamu hiyo ipo katika matayarisho makubwa na tarehe rasmi ya uzinduzi wa albamu hiyo itatolewa muda wowote kuanzia sasa.

Aidha albamu hiyo inatarajiwa kusheheni nyimbo 12  zikiwemo Inanga, Icyembe, Ingoma na Umuduri, ambazo zote zimerekodiwa kwa kutumia vyombo vya asili akiweka wazi kuwa dhumuni la kutoa albamu hiyo ni kulinda na kuthamini utamaduni wa Rwanda kupitia muziki huku akiwahimiza vijana kutambua na kuipenda asili yao badala ya kupotoshwa na tamaduni za nje.

WATU ZAIDI YA 15 WAJERUHIWA KENYA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI YA MAGURUNETI.

Takribani watu 15 wamejeruhiwa katika milipuko ya maguruneti nchini Kenya Jumapili usiku. Mashambulizi hayo yalifanywa mjini Mombasa mtaa wa Likoni na Nairobi katika mtaa wa Eastleigh yote chini ya kipindi cha masaa mawili.
Shambulizi la mjini Mombasa, lilifanyika katika kanisa moja saa moja usiku Jumapili na kuwajeruhi watu 12 wakati shambulizi la Niarobi lilitokea katika hoteli moja huku watu watatu wakijeruhiwa.




Waathiriwa mjini Nairobi walikimbizwa hospitalini kwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta kwa matibabu zaidi.

Maafisa wakuu mjini Mombasa walielezea kuwa hakuna mtu aliyefariki kutokana na shambulizi hilo lakini kulikuwa na ripoti kuwa baadhi ya waathiriwa walilazwa katika hospitali kuu mjini Mombasa wakiwa hali mahututi.
Polisi walisema kuwa watu sita akiwemo mwanfunzi wa darasa la nne pamoja na mhubiri walijeruhiwa katika kile kilichosemekana kuwa shambulizi la guruneti katika kanisa la Earthquake Miracle Ministries.
Waathiriwa zaidi walijeruhiwa katika msongamano wa watu waliokuwa wanakimbilia usalama wao baada ya kuzuka kwa moto kufuatia gurunti hilo.
Matukio hayo ya usiku wa kuamkia leo, yanazua wasiwasi kuhusu kuibuka tena kwa mashambulizi ya kigaidi katika miji hiyo miwili baada ya miezi kadhaa ya kutokuwepo mashambulizi.
Duru zinasema kuwa shambulizi la Nairobi lilitokana na guruneti lililorushwa kutoka kwa gari iliyokuwa inakwenda kwa kasi, wakati shambulizi la mjini Mombasa lilitokea wakati mtu aliyekuwa anaendesha pikipiki aliporushia guruneti kikundi cha watu.
Duru zinasema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na mashambulizi hayo.
Kufikia Jumapili, usiku, wataalamu walikuwa bado wanakusanya ushahidi mjini Mombasa kubaini nia ya mlipuko uliotokea na ikiwa lilikuwa shambulizi la guruneti au kifaa kilichotengezwa mfano wa bomu.
Mashambulizi kama haya yamekuwa yakishuhudiwa tangu jeshi la Kenya kujiunga na majeshi ya AU katia harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram.

Source:BBC

Green Economy in the South: An International Conference at the University of Dodoma

click here

CHAMA KIKUU NA MTAZAMO WAKE KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA.

Tafakari,chukua hatua.

MKUU WA MAJESHI LIBYA AJIUZURU.

Mkuu wa majeshi nchini Libya Youseff al Man Gous amejiuzulu siku moja baada ya ghasia mashariki mwa mji wa Benghazi kusababisha vifo vya watu 31.Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumamosi wakati waandamanaji walipovamia kambi ya kundi la wanamgambo wanaojulikana Shield wanaoiunga mkono serikali.Kundi hilo pia ndilo lililo na jukumu la  kulinda amani katika eneo hilo la Benghazi.Waandamanaji hao walikuwa wanataka wanamgambo hao wakabidhi madaraka ya kiusalama kwa  kikosi rasmi cha usalama cha Libya na wasalimishe silaha zao. Bunge la kitaifa la Libya limetangaza kujiuzulu kwa Youseff  ambaye ameshutumiwa kwa kuchelewa kuunda jeshi la kitaifa na kutangaza pia siku tatu za maombolezi.

Source:DW

RHODES SCHOLARSHIPS AT UNIVERSITY OF OXFORD IN UK, 2014.

Each year, Rhodes scholarships are awarded for pursuing full-time postgraduate studies at the University of Oxford, UK. 83 Rhodes scholars are selected annually from 14 countries or groupings of countries around the world. Each scholarship covers all University and College fees, a personal stipend and one economy class airfare to Oxford at the start of the scholarship, as well as an economy flight back to the student’s home country at the conclusion of the scholarship. Applications are open for 2014 round with different deadlines for each country.

Study Subject(s): These scholarships are awarded to study any course offered by the University of Oxford at postgraduate level.
 
Course Level: Rhodes Scholars may read for any full-time postgraduate degree (including the BA with senior status over two years) at the University of Oxford.
 
Scholarship Provider: Rhodes Trust
 

CHADEMA YAIKUBALI RASIMU YA KATIBA MPYA,LIPUMBA AITOA KASORO.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa CHADEMA, Charles Mkela.
Alisema CHADEMA kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”
Msimamo wa Sumaye
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.
Sumaye anaungana na wanasiasa wengine waliopinga muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wengine wakiwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Daftari.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali tatu zinaweza kutikisa Muungano.
“Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu... unaweza kuyaongeza kwani kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu... kama kuna mvutano baina ya Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa na mvutano zaidi,” alisema na kuongeza:
Lipumba: Katiba ya Bara kwanza
Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni ya Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba, kura ya maoni isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya kazi nzuri ya kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya CCM, kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.
“Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa ardhi, maliasili na rasilimali za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza uchumi na uhuru wa Serikali za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya Muungano.”
“Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa Serikali tatu, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na mengineyo yamepata nafasi.”

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...