Monday, May 27, 2013

KINANA NA NAPE NAUYE KUWASHA MOTO MKOANI NJOMBE.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii (jana), kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.

Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi hii (jana). Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu

Nape akisaini kitabu cha wageni

ENGINEERING SCHOLARSHIP AT UNIVERSITY OF ABERDEEN IN UK, 2013

The University of Aberdeen, UK is offering Engineering scholarship for international students.This scholarship is available for pursuing  full time MSc degree in Safety & Reliability Engineering. This scholarship is valued at £15,000 for the one year duration of the programme. Applicants must receive and then firmly accept an unconditional offer of a place for programme at university before applying this scholarship.The application deadline is 2nd of August 2013.


HUU NDIO USAJILI WA SIMBA NA YANGA MSIMU UJAO.

Huu ndo ukweli usiopingika kuwa Wekundu wa Msimbazi wanatafuta silaha kutoka sehemu nyingine huku wazee wa Jangwani wakiwa wameweka mlija wao klabuni hapo na kunyonya silaha kutoka kwa wekundu hao.
Tafakari,chukua hatua.

BREAKING NEWS:TRENI YAUA UKONGA DAR.

Muda si mrefu uliopita treni ya abiria imegonga gari ndogo aina ya RAV 4 na kuua dereva ambaye ni mwanaume na abiria mmoja wa kike bado yuko mahututi.


Sunday, May 26, 2013

UKWELI KUHUSU VURUGU ZA MTWARA



WACHEZAJI 30 WA TWIGA STARS WAITWA KAMBINI.

Twiga Stars.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.

Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili hii (Mei 26 mwaka huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao.

Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.

Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).
Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).
Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

TAIFA STARS WABADILI MUONEKANO NA SASA NI NDANI YA SUTI KALI.

Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja wakionesha suti zao ambazo zimebuniwa na mbunifu Sheria Ngowi.

Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya


John Bocco na Erasto Nyoni


Saturday, May 25, 2013

MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO ULIOFANYIKA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE-25-05-2013

Wasailiwa waliochaguliwa kuendelea na usaili kwa Kada ya Internal Auditor II (NAO) wanatakiwa kufika katika chuo cha uhasibu (Tanzania Institute of Accountancy-TIA) tarehe 27-05-2013 saa moja na nusu asubuhi, kwa ajili ya usaili wa vitendo (PRACTICAL)
Wasailiwa waliochaguliwa kuendea na usaili kwa kada ya Computer Systems Analyst-(e-GA) wanatakiwa kufika katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira (Maktaba kuu ya Taifa) tarehe 27-05-2013 saa moja na nusu asubuhi, kwa ajili ya usaili wa ana kwa ana
Wasailiwa waliochaguliwa kuendelea na usaili kwa kada ya Chemical Laboratory Technologist-(GCLA) wanatakiwa kufika katika ofisi za GCLA tarehe 27-05-2013 saa moja na nusu asubuhi kwa ajili ya usaili wa ana kwa ana.

Na matokeo kamili ni:-
S/N EXAM NUMBER         SCORE REMARKS
1 PSRS AUD II NAO - 0520 96.00 SELECTED
2 PSRS AUD II NAO - 0513 95.00 SELECTED
3 PSRS AUD II NAO - 0701 93.00 SELECTED
4 PSRS AUD II NAO - 0498 92.00 SELECTED
5 PSRS AUD II NAO - 0174 90.00 SELECTED
6 PSRS AUD II NAO - 0869 90.00 SELECTED
7 PSRS AUD II NAO - 0574 87.00 SELECTED
8 PSRS AUD II NAO - 0780 87.00 SELECTED
9 PSRS AUD II NAO - 0266 86.00 SELECTED
10 PSRS AUD II NAO - 0194 85.00 SELECTED
11 PSRS AUD II NAO - 0197 85.00 SELECTED

Leo ni leo,Bayern Munich vs Borussia Dortmund zapambana finali UEFA.


Miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern Munich na Borussia Dortmund leo usiku minamo saa 3.45 inapambana katika fainali ya  kugombea kombe la klabu bingwa barani Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley mjini London.
Bayern Munich iliitoa Barcelona ya Uhispania katika nusu fainali na Borussia iliishinda Real Madrid pia ya Uhispania.Kocha wa Bayern Jupp Heynckes amesema fainali ya leo ni fursa yake ya mwisho ya kulitwaa taji la klabu bingwa za Ulaya-champions League.
Kwa upande wake kocha wa Borussia Jürgen Klopp amesema ni Bayern iliyojawa shinikizo.

Friday, May 24, 2013

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE . EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB)

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE . EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014


1.0       UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Afrika Mashariki imeundwa na Ibara ya 2(1) ya Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia makubaliano ya wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Aidha Ibara ya 8(3) (a) ya Mkataba wa kuanzishwa kwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki imezipa mamlaka nchi wanachama kuanzisha Wizara mahsusi,  itakayoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa ibara hiyo,  Tanzania, ilianzisha  Wizara ya Afrika Mashariki ambayo  majukumu yake ni pamoja utekelezaji wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mikataba Midogo (Protocols)  Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja la Afrika Mashariki  na Mazungumzo ya uundwaji wa Shirikisho la kisiasa la  Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika, ni mategemeo ya Watanzania kwamba, Wizara hii ya Afrika Mashariki italitendea haki taifa hili, kwa kuwashirikisha wananchi kwenye kila hatua na kwa kusimamia kwa dhati na kikamilifu michakato yote ya mtangamano wa Afrika Mashariki, kwa maslahi ya nchi yetu, ili kuhakikisha kwamba Tanzania inanufaika vilivyo na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani kipindi hiki itajielekeza kwenye mambo machache ambayo tunaamini yakizingatiwa, Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa imara, na nchi zote wanachama watafurahia matunda ya jumuiya hiyo.
2.0 MADAI YA MAFAO YA WASTAAFU WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ILIYOVUNJIKA 1977
Mheshimiwa Spika, madai ya mafao ya wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa ni aibu kwa Taifa. Wastaafu hawa wameyumbishwa kiasi cha kutosha, wamepuuzwa kiasi cha kutosha, wamedhalilishwa kiasi cha kutosha na wameonewa kiasi cha kutosha na serikali hii ya CCM inayojiita sikivu.  Hakika  laana ya wastaafu hawa wanaodhulumiwa haki yao wazi wazi namna hii  itaendelea kulitafuna taifa hili kwa kwa miaka mingi ijayo kama Serikali haitawatendea haki.
Mheshimiwa Spika, Baada ya Jumuiya hiyo kuvunjika ghafla tarehe 30 Juni, 1977 ulizuka mgogoro wa mgawanyo wa mali na madeni yake. Ili kuumaliza mgogoro huo, Umoja wa Mataifa uliiteua Benki ya Dunia kusuluhisha mgogoro huo. Benki ya dunia ilimteua mtaalamu wake, mwanadiplomasia, Dkt. Umbricht (sasa marehemu) ambaye alifanikisha kuwanzishwa kwa Mkataba wa Kimataifa uliojulikana kama “East African Community Mediation Agreement 1984” kuhusu mgawanyo wa mali na madeni ya Jumuiya yakiwemo mafao ya wafanyakazi wa Jumuiya hiyo.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kazi kubwa aliyofanya msuluhishi, Dkt. Umbritch ilikuwa ni kuzigawanya fedha za pensheni na provident funds za Jumuiya kwa nchi tatu wanachama yaani Kenya, Uganda na Tanzania kulingana na idadi ya raia wake katika Jumuiya, kwa madhumuni ya kuwalipa mafao raia wake. Katika mgawo huo, Tanzania ilikabidhiwa paundi za Uingereza milioni 14 kwa ajili ya kulipa mafao ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza bunge hili na wananchi wote fedha hizo zilitumika kufanyia nini­ kama walengwa hawakulipwa mafao yao?
Mheshimiwa Spika, nchi za Kenya na Uganda tayari zilishawalipa wastaafu wa Afrika ya Mashariki stahili zao na hali huko ni shwari, lakini kwa Tanzania jambo hili limegubikwa na wingu zito la ufisadi kwa kuwa fedha ya kuwalipa wastaafu hao ilishatolewa. Kwanini wastaafu hao hawakulipwa, na wale waliolipwa, walipewa cheki za silingi 10 na shilingi 130 za kitanzania jambo ambalo ni aibu na fedheha kwa Serikali hii ya CCM inayojiita sikivu kwa wananchi wake.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali hii ya CCM inayojiita sikivu, kutoa tamko leo,  mbele ya bunge hili kuhusu mafao ya wastaafu hao ili wajue moja: kama wanalipwa au hawalipwi. Kama Serikali haitatoa tamko leo,  kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wastaafu wa Afrika Mashariki, basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimika kuleta hoja binafsi bungeni kwa hatua za kibunge kuhusu mafao ya wastaafu wa iliyokuwa Afrika Mashariki.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...