Friday, May 17, 2013

MAJINA YA WAGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA - KANDA YA KASKAZINI.


TAARIFA KWA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI
Tarehe 15 Mei 2013, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.
Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.
Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:

JINA LA MGOMBEA
KATA
JIMBO
MKOA
BI. YOSEPHA KOMBA
GENGE
MUHEZA
TANGA
BW. OMARI HATIBU SALIMU
TINGENI
MUHEZA
TANGA
BW. LAWRENCE SURUMBU TARA
BASHNET
BABATI VIJIJINI
MANYARA
BW. ERNEST JOROJIK
DONGOBESH
MBULU
MANYARA
ENG. JEREMIAH MPINGA
ELERAI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. RAYSON NGOWI
KIMANDOLU
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. MALANCE KINABO
THEMI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. EMMANUEL KESSY
KALOLENI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. JAPHET SIRONGA LAIRUMBE
MAKUYUNI
MONDULI
ARUSHA
CHAMA kimejipanga kushiriki uchaguzi huu kikamilifu sana na katika maeneo yote kanda imeteua MAMENEJA WA KAMPENI ili kuhakikisha uratibu na utekelezaji wa kampeni kwa mfumo tuliouweka.
Imetolewa leo tarehe 16 Mei 2013.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini

Thursday, May 16, 2013

CALL FOR APPLICATIONS FOR TRAINING WORKSHOP ON M&E - UDSM.

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, DEPARTMENT OF GEOGRAPHY
CALL FOR APPLICATIONS FOR TRAINING WORKSHOP ON MONITORING AND EVALUATION OF DEVELOPMENT PROJECTS
The department of Geography of the University of Dares Salaam is announcing a five days workshop training on MONITORING AND EVALUATION FOR DEVELOPMENT PROFESSIONALS to be conducted at the University of Dar es Salaam Main Campus from 27th to 31st May, 2013.


CALL FOR APPLICATIONS FOR ADMISSION (EVENING CLASSES)- SAUT.

ST. AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA P.O. BOX 307, MWANZA, TANZANIA

St. Augustine University of Tanzania invites applications from qualified candidates for admission into parallel programmes (Evening Classes) into CERTIFICATE, DIPLOMA and DEGREE PROGRAMMES at Mwanza Campus.
 

CALL FOR APPLICATION FOR DEGREE & DIPLOMA PROGRAMMES- JoKUCo


 JOSIAH KIBIRA UNIVERSITY COLLEGE OF TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA
                             P.O. BOX 1023, BUKOBA, TANZANIA
            Tel: +255 732 983 642; +255 732 983 643; Fax: +255 732 983 644
              E-mail: admission@jokuco.ac.tz; or jokuco@jokuco.ac.tz; Website: www.jokuco.ac.tz


CALL FOR APPLICATION FOR DEGREE AND DIPLOMA PROGRAMMES FOR 2013/2014 ACADEMIC YEAR
Josiah Kibira University College (JoKUCo) of Tumaini University Makumira (TUMA) invites applications for qualified candidates to apply for Degree and Diploma Programmes for Academic Year 2013/2014.

Degree Programmes:

BAADA YA SERIKALI KUKASILISHWA NA KATIKA KATIKA YA UMEME,KUIFUMUA TANESCO.

Serikali ilitangaza kuwa inakamilisha zoezi la kuifumua TANESCO na kuiunda upya kwa kuigawa katika makundi ili iweze kuwa na ufanisi.

KIPANYA NA WATUMISHI WANAOTUMIA "COMPUTER"

Ukweli ni 100%.Tafakari,Chukua hatua.

POULSEN AWAITA WAPYA 6 TAIFA STARS ITAKAYOWAVAA MOROCCO.

 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16,2013) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).
Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.
Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.
Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

WABUNGE WA UPINZANI WAIBUA UFISADI BUNGENI.

Mh.Highness Kiwia (MB).
KAMBI ya Upinzani bungeni imeibua ufisadi wa mabilioni ya fedha unaolihusisha Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Shirika hilo linadaiwa kuingia ubia na kampuni binafsi ya Power Pool East Afrika Ltd na hivyo kuwezesha kumpuni hiyo kupatiwa mkopo wa zaidi ya Sh bilioni 217 kutoka Benki ya Exim ya China kwa dhamana ya Serikali. 
Mkopo huo uliombwa kwa ajili ya kampuni hiyo kuendesha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

Taarifa hiyo ilitolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani bungeni, Highness Kiwia, wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Katika taarifa hiyo, kambi hiyo ilihoji uhalali wa NDC kuingia ubia na kampuni hiyo, huku wamiliki wa kampuni hiyo wakitajwa kuwa na uhusiano na vigogo wa CCM (majina tunayo).


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI PSPF - JUNI 01, 2013

PSPF imetoa tangazo la kuita watu walioomba nafasi za kazi kwa tangazo la mwezi wa Februari.Kusoma tangazo hilo na majina fungua link ifuatayo:-


http://www.pspf-tz.org/sites/files/filefield/new_interview_13.pdf

MLIPUKO WA BOMU BAGHDAD - 5 WAUAWA NA 19 WAJERUHIWA.

Mripuko wa bomu la kutegeshwa kwenye gari katika mji wa Baghdad umewauwa kiasi ya raia watano.Maafisa wawili wa polisi wamesema gari hilo lililokuwa limewekwa viripuko liligonga basi na  kituo cha texi leo asubuhi wakati watu wengi wakiwa katika pirika pirika mjini Sadr.

Mripuko huo pia uliwajeruhi watu 19.Afisa wa afya katika hospitali iliyo karibu na mkasa huo amethibitisha idadi ya waathiriwa.Shambulio la leo linakuja siku moja baada ya wimbi la mashambulio hapo jana ambayo yaliwauwa watu 33 katika mitaa inayokaliwa na washia.

Mashambulio hayo yanaongezeka wakati kuna hali ya wasiwasi kati ya serikali inayoongozwa na washia na wasunni walio wachache wanaohisi wanazingatiwa kama raia wa daraja la pili.

Source:DW

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...