Pamoja na jana kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu
wa 2012/2013, kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na
mazoezi ya viungo na kujenga misuli (GYM) katika kituo cha mazoezi
kilichopo jengo la Quality Cetntre kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal
Union siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo jana
imetangazwa rasmi kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013
baada ya timu za Coastal Union na Azam FC kutoka sare ya bao 1-1,
imeendelea kujifua kuhakikisha inamalizia mzunguko wa pili wa VPL kwa
ushindi kama ilivyofanya tangu kuanza duru la pili.
Azam FC
iliyokua na ndoto za kuweza kufikia pointi 56 za Yanga, ilikua ikiombea
yenyewe kushinda michezo yake yote mitatu huku iikiombea Yanga kupoteza
michezo yake miwili iliyosalia hali ambayo ilikwenda kinyume hapo jana
kwa wauza mikate kupata sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union na kuifanya
Yanga itangazwe mabingwa wapya wa VPL kwa kuwa na ponti 56 ponti 8 mbele
ya Azam yenye pointi 48.
Huu
unakua ni Ubingwa wa 24 kwa Yanga tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu
Tanzania bara rekodi ambayo hakuna timu yoyote inayokaribia kufuatia
watani wa jadi Simba SC kuwa wametwaa ubingwa huo mara 18 tu.
Rekodi ya Ubingwa wa Yanga :1968,
1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991,
1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007-2008, 2008-2009,
2010-2011, 2012-2013
Baada ya kufanya mazoezi katika
uwanja wa shule ya sekondari Loyola kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku
ya jumatano, jana wachezaji waliingia kambini katika hosteli za klabu
zilizopo makao makuu mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo wa
jumatano.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amekiongoza
kikosi cha wachezaji 26 kufanya mazoezi ya gym leo katika kituo cha
Quality Centre ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi
ya timu ya Coastal Union siku ya mei mosi jumatano katika uwanja wa
Taifa jijin Dar es salaam.
Yanga
imebakisha michezo miwili (Costal Union 01.05.2013) na (Simba SC
18.05.2013) kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodaom huku ikiwa tayari
imeshatwaa Ubingwa mapema kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom.
Uongozi
wa klabu ya Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya
Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya jumatano (mei mosi) katika dimba la
uwanja wa Taifa ili kuja kuwashangilia vijana wakiendeleza furaha ya
kutwaa Ubingwa wa VPL msimu huu.
DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD, BACKWARD NEVER (EFBN)
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa Timu ya Yanga.
Saturday, April 27, 2013
CHADEMA KUWASHA MOTO TABORA MJINI LEO,MNYIKA AMUANIKA NDUGAI KWA WAPIGA KURA WAKE.
Mh.Zitto Zuberi Kabwe. |
KUSHITAKIWA KWA NDUGAI.
Katika upande wa pili,Naibu Spika Mh.Jobu Ndugai ameshitakiwa kwa wapiga kura wake na Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwahoji iwapo walimtuma bungeni kufanya Ubabe wa kuwatoa nje wabunge wenzie badala ya kuwatetea.
Mnyika
alitoa Mashitaka hayo jana Aprilli 26, 2013 katika kijiji cha Iyegu,
Kata ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, ambapo alisema amemkatia
Rufaa Ndugai mara Tano bungeni bila majibu, kwa hiyo jana aliamua
kumshitaki kwao ili wafanye maamuzi magumu juu ya mbunge wao asiyefanya
kazi waliyomtuma.
Akizungumza
katika Mkutano huo Mnyika alimshitaki Ndugai akiwahoji kama walimtuma
kufanya hivyo, na waliposema Laa, aliwataka kufanya mabadiliko ya
mwakilishi wa Jimbo lao kama wanataka kumaliziwa Kero zao zikiwepo Haki
na Maendeleo ya kiuchumi na Matumizi bora ya Rasilimali zao.
Mwananchi
mmoja alimhoji Mnyika “Je, ni nani aliyetayarisha, kulinda, kusimamia na
kusafirisha Twiga wetu kwenda nje, lini watarejeshwa na waliohusika
watafanywaje?.
Mnyika
aliwajibu wananchi kwamba, wahusika wa usafirishaji wa Twiga wao
ni vigogo walioko madarakani, na Twiga hao wako nchi mmoja ya Kiarabu,
na mbali ya Twiga hao hivi karibuni Chadema itaibua suala la Tembo, na
kuwaambia suluhisho la haraka kwa yote hayo ni kufanya mabadiliko ya
viongozi mafisadi haraka.
Alipoulizwa
Mauaji na Vitisho wanavyofanyiwa na Kundi linalojiita Kanyaga
Twende, wanapoamua kujiunga na vyama Upinzani, Mnyika aliwauliza kama
wanayo simu ya Mbunge wao wamuulize ila wasimtukane, na waliposema
hawana aliwatajia namba ya Ndugai na ya Mkurugenzi wa Usalama Chadema
ambaye alidai atawawasaidia dhidi ya vitisho .
Aidha Mnyika
kabla ya kushuka Jukwani saa 11.30 jioni, aliuuliza umati uliokuwepo
uwanjani hapo, wangapi wapo tayari kwa mabadiliko ya M4C, watu wote
karibu 1,000 walinyosha mikono na Mnyika akashuka kuelekea Kongwa
kuungana na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, kuendelea na Mikutano
mingine.
Chanzo:Mtandao wa Kijamii wa CHADEMA.
Friday, April 26, 2013
8th EXHIBITIONS ON HIGHER EDUCATION , SCIENCE & TECHNOLOGY
THE TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES
8th Exhibitions on Higher Education, Science and Technology
Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam
Wednesday 22th to Friday 24th May, 2013
The Tanzania Commission for Universities (TCU) wishes to inform all stakeholders and the general public that, the 8th exhibitions on Higher Education, Science and Technology will be held from 22nd-24th May 2013. These exhibitions are jointly organized by the TCU, the Ministry of Education and Vocational Training (MoEVT), Higher Education Institutions, as well as Regulatory, Professional and Research Bodies in and outside Tanzania.
Theme: "Building a knowledgeable, accountable and progressive society through Higher Education, Science and Technology"
Exhibitions’ Vision:
To become the leading national and regional state of the art exhibitions that promotes participation, enhances collaboration, builds up partnerships between higher education institutions and the Industry as well as developing mutual understanding on the issues that govern the quality of Higher education in the Country for the benefit of all humanity.
Exhibitions’ Mission:
To promote equity and collaboration, create partnerships and networks amongst the exhibitors and create linkages between higher education institutions, industry, research and development institutions and the market for national, regional and global socioeconomic development.
The Objectives of the Exhibitions:
o Creation of awareness among the general public about the development of Higher Education and Research Institutions and Professional Bodies in the country;
o Providing an opportunity to Higher Education Institutions to publicize their core functions and activities in the areas of teaching, research, consultancy as well as their current performance, potentials and future prospects;
o Providing a platform for Higher Learning and Research Institutions as well as Local and International Educational Business Companies to exchange ideas and experiences related to their core functions thereby triggering competition that will result in provision of quality higher education and research output;
o Enable the public and prospective applicants for admission into Higher Education Institutions within and outside Tanzania for the year 2013/2014 to interact with Universities, Regulatory Bodies and Research Institutions in order for them to make an informed choice;
o Sensitize the public on the application process through the Central Admission System (CAS).
Participants:
Exhibitors are Higher Learning and Research Institutions, Quality Assurance Regulatory Bodies and Foreign Universities from within and outside the East Africa Region. Local and International Educational Business companies are also invited to participate.
Exhibitions Venue:
The 8th exhibitions on Higher Education Science and Technology will take place at the Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam.
Duration:
The exhibitions will be open at 09.00 hours and close at 18.00 hours for three days from 22nd-24th May 2013.
Expected Outcome:
The exhibitions will enable the Government, employers and the general public to realize the opportunities available in Higher Education sector and in Educational Business Companies within and outside Tanzania and appreciate the critical roles they play in achieving national development goals.
Sponsorship:
We invite companies, Organizations and individuals who wish to sponsor the exhibitions. Upon some agreements, sponsors will be given a chance to advertise their business/ goods/services as well as a space to exhibit their business/ goods/services. Interested sponsors please contact the Office of Executive Secretary, TCU through below address.
Issued by the office of:
Executive Secretary,
Tanzania Commission for Universities,
Garden Road, Mikocheni,
P. O. Box 6562,
Tel: 22 2772657
Fax: 22 2772891
Email: es@tcu.go.tz
Dar es Salaam
You are all welcome
Source:TCU
BAADA YA AZAM KUBANWA MBAVU,HUU NDO MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM
Rank | Teams | Played | Wins | Draw | Lost | GD | Points |
---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Young Africans | 24 | 17 | 5 | 2 | 31 | 56 |
2 | Azam FC | 24 | 14 | 6 | 4 | 22 | 48 |
3 | Kagera Sugar | 23 | 11 | 7 | 5 | 8 | 40 |
4 | Simba SC | 22 | 9 | 9 | 4 | 11 | 36 |
5 | Mtibwa Sugar | 24 | 9 | 9 | 6 | 3 | 36 |
6 | Coastal Union | 24 | 8 | 10 | 6 | 3 | 34 |
7 | Ruvu Shooting | 22 | 8 | 6 | 8 | 0 | 30 |
8 | JKT Oljoro | 24 | 7 | 7 | 10 | -5 | 28 |
9 | Prisons FC | 24 | 6 | 8 | 10 | -7 | 26 |
10 | JKT Ruvu | 24 | 7 | 5 | 12 | -17 | 26 |
11 | Mgambo Shooting | 23 | 7 | 4 | 12 | -7 | 25 |
12 | Toto African | 25 | 4 | 10 | 11 | -12 | 22 |
13 | Police M | 23 | 3 | 10 | 10 | -10 | 19 |
14 | African Lyon | 24 | 5 | 4 | 15 | -20 | 19 |
CHADEMA WAFUNIKA NJOMBE,WANANCHI WAMKANA MAKINDA
Umati mkubwa uliohudhuria mkutano wa CHADEMA. |
Katika
hali ya kushangaza wakazi na wananchi wa Mkoa wa Njombe wamemkana Spika wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madai kuwa hawakumtuma kutumikia chama bali
kushughulikia kero na matatizo ya wananchi.
Hayo yalitokea katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani hapo katikati ya Jimbo la Njombe Kusini ambalo yeye ndiye Mbunge wake.
Mkutano huo ambao uliongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo( CHADEMA), Dr wilbrod Peter Slaa,Naibu katibu mkuu kutoka zanzibari pamoja na wabunge machachari kutoka katika chama hicho(Mh Joseph Mbilinyi-Mbeya mjini, Mhezekiel Wenje-Nyamagana pamoja na Mchungaji Peter MsigwaIringa mjini) ambao wote kwa pamoja walifukuzwa bungeni kwa madai kuwa wanaleta fujo bungeni.
Dr .Slaa aliwataka wananchi wamthibitishie kuwa Makinda hakwenda bungeni kuwatetea bali kukitumikia Chama Cha Mapinduzi hivyo wabunge wa Chadema waendelee na kasi hiyo hiyo ya kuisimamia na kuikosoa serikali, hapo ndipo umati wote uliohudhuria mkutano huo uliponyoosha mikono yote juu kwa ishara ya kuunga mkono hoja iliyotolea na kiongozi huyo.
Spika Anne Makinda anatuhumiwa kwa kuliongoza Bunge ki ubabe hivyo kuwanyima wapinzani haki yao ya msingi ya kuihoji serikali juu ya matuimizi mabaya ya mali ya umma
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa CHADEMA.
Breaking news:GODBLESS LEMA AMEKAMATWA NA POLISI NA KUWEKWA NDANI.
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka Arusha ni kuwa Mbunge wa Arusha Mjini amekamatwa na kuwekwa ndani kituo cha kati Arusha. Kukamatwa kwake ni baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwake na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku wa manane, lakini baadae Mh. Lema
alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na
kupelekwa kituo kikuu cha polisi mjini Arusha.
Habari zaidi zitawajia kadiri tutakavyokuwa tunazipata.
Kukamatwa kwake kulikuja baada ya
polisi kuvunja mlango na kuingia ndani na kuendesha msako wa
nguvu humo ndani .Vitu kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa
police.
Hata hivyo, wananchi wengi walijitokeza wakati mbunge wao anakamatwa ambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani mchana wa leo.
TAMKO LA MH. GODBLESS LEMA
Mh.Godbless Lema. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jana majira ya saa nne asubuhi nilipokea taarifa kutoka Chuo cha Uhasibu juu ya tukio la mauaji ya mwanafunzi yaliyotokea jana usiku kwa kuchomwa kisu eneo karibu na chuo , nilipita Chuoni hapo baada ya kusikia taarifa hiyo , nilikuta Wanafunzi wengi sana wakiwa wamekusanyika pamoja wakiwa na jazba huku Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya akijaribu kuwasihi watulie wakati walipokuwa wanatafuta muafaka wa kuzuia jazba ambayo ilikuwa ina lengo la kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa.
Nilipata faragha ya kuongea na Mwalimu aliyekuwa pale ( Dean of Student ) pamoja na OCD na wote walinieleza tatizo lilivyoanza na kuomba nitumie busara kuzuia jazba na maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa kuelekea kwa Mkuu wa Mkoa niliongea na wanafunzi na niliwasihi watulie na nilifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa na kwa bahati nzuri nilimpata Mkuu wa Mkoa na kumweleza juu ya kifo hicho na kile ambacho wanafunzi wanakusudia kufanya kuandamana kwenda ofisini kwake. Nilimuomba afike ili aweze kutuliza hali hile na pia atoe kauli juu ya tukio hilo baya la kuhuzunisha kwani ikizingatiwa kuwa ni zaidi ya mara moja matendo kama haya yamekuwa yakitokea na hakuna hatua zozote zimekuwa zikichukuliwa kuwahakikishia Wanafunzi Usalama wao na mali zao.
Mkuu wa Mkoa pamoja na mimi kumpa taarifa mapema aliahidi kufika mapema jambo ambalo halikufanyika na wanafunzi walianza kuwa wakali na nilifanya jitihada na hekima za hali ya juu kuvuta subira za wanafunzi hao ili Mkuu wa Mkoa afike . Baada ya Mkuu wa Mkoa kufika Makamu wa Chuo aliniomba niwaandae wanafunzi kumsikiliza Mkuu wa Mkoa na yeye alikwenda kumchukua Mkuu wa Mkoa na kumpa mukutasari wa tukio zima na hali halisi ya kilichokuwa kinaendelea na kimsingi Mkuu wa Mkoa alipofika Wanafunzi walitaka apande juu kuongea mahali ambako tulitumia kama jukwaa kwa maongezi wakati wote lakini badala yake mambo yafuatayo yalianza kutokea
1) Mkuu wa Mkoa alikataa na kunitaka nishuke chini mahali alipokuwa yeye na timu yake ya ulinzi na usalama Mkoa kwa kweli nilitii na nilipotaka kuongea nae alinidharau na kuniambia hawezi kuongea na wanafunzi wahuni wasiokuwa na nidhamu maneno ambayo yaliwatia wanafunzi hasira zaidi na nilimsihi na kumuomba Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (RSO) kumshawishi Mkuu wa Mkoa kukubali kuongea nao kwani hali ilivyokuwa ni dhahiri kwamba wanafunzi wale walikuwa na jazba ya hali ya juu na hivyo hekima na unyenyekevu ndio ilikuwa njia pekee ya kutuliza hali hile.
2) Mkuu wa Mkoa alitoa masharti kwamba asingeweza kuongea nao bila kipaza sauti na wanafunzi wote waende jengo lililokuwa karibu na Utawala na wakisha kaa atakuja kuongea nao jambo ambalo wanafunzi waligoma kwa imani kwamba jengo hilo lisengeweza kuchukua wanafunzi wengi na mimi niliaga naondoka kwenda msibani na wanafunzi waligoma nisiondoke mpaka watakapo sikilizwa na kwa kweli nilitii maombi baada ya kunizuia na kukaa mbele ya gari yangu.
3) Tulipokwenda eneo la kukutania na mara hii ilikuwa ni nje jirani ya jengo la utawala wanafunzi walikusanyika wakimsubiri Mkuu wa Mkoa na kabla hajafika nilitwa na yeye mwenyewe ili tuweke msimamo wa pamoja kama viongozi lakini badala yake alitumia Polisi kunitisha na kuhaidi kuwa nitamtambua kuwa yeye ni Serikali ,tulitofautiana tena nilipokataa hofu hiyo na ghafla tuliamua kwenda eneo la kuongea na wanafunzi na ndipo yafuatyo yalitokea “
Mkuu wa Mkoa wakati anaanza kuongea alianza kusema maneno yafuatayo “ Mnaona hiki Kifua na huu mwili wangu , na hapo ndipo hali ilipochafuka na kuamsha vurugu kubwa kutoka kwa Wanafunzi waliokerwa na kauli yake na Polisi wa walimchukua na tafrani kati ya Polisi na Wanafunzi ikapamba moto hali iliyosababisha mabomu ya machozi kulipuliwa kwa wingi kila kona ya chuo na kila mtu kuanza kukimbia kuangalia usalama wake nikiwemo mimi .
Nimesikiliza Mkutano wake na Waandishi wa Habari na leo nimesoma nakusikiliza vyombo mbali mbali vya habari kwamba ninatafutwa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa , nimeshangaa sana japo sio kumshangaa Mkuu huyu wa Mkoa kwani ufahamu na uwezo wake naujua ulivyo katika kufikiri na kutatua mambo ya msingi na muhimu , kwa jinsi nilivyomsikia na kumuona alivyokuwa anashughulikia tatizo lile lililotukutanisha jana pale Chuoni , kwa kweli nilishangazwa sana na kuogopa kama hekima ya Mkiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa angeweza kushughulikia tatizo lile kwa namna ile ya Kiburi , Dharau na Majivuno ambayo hakika ilikuwa ni chanzo cha wanafunzi kukataa kumsikiliza na ndipo alipoamua kuondoka huku zomea zomea ikiendelea kushamiri vizuri . Mabomu yalianza kupigwa , wanafunzi walipigwa na kunyang’anywa pesa , simu , na lap top na vitu mbali mbali ambavyo Polisi walikuwa wanaona vina thamani kwao , nilikuwa ninatazama mambo haya huku roho yangu ikiwa inauma sana kwamba wanaopaswa kulinda usalama wa raia na mali zao ghafla waligeuka kuwa vibaka wa kuumiza raia na kupora mali zao .
Ninawapa pole wanafunzi kwa msiba wa rafiki yao na siku ya jana ilikuwa ni siku ya Serikali kutumia busara kurudisha matumaini kwa wanafunzi wale pamoja na raia , lakini badala yake wafiwa walipotaka kudai haki zao za kulindwa , walipigwa , walidhalilishwa na Chuo chao kufungwa bila sababu ya msingi wala kuzingatia mambo muhimu .
Ifahamike kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha kina wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii, na amri ya mkuu wa mkoa kufunga chuo na kuamuru wanafunzi watawanyike ifikapo saa kumi na mbili jioni , huu ni ukosefu wa upendo , hekima , busara na utu ikizingatiwa kuwa sababu na mchochezi wa vurugu hizi ni Mkuu wa Mkoa kukosa maarifa na hekima.
Nimepokea ujumbe katika simu yangu kutoka kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa inayonitishia na kuweka maisha yangu kwenye hali ya hatari na ujumbe huo unasema “ UMERUKA KIHUNZI CHA KWANZA , NITAKUONYESHA KUWA MIMI NI SERIKALI ULIKOJIFICHA NITAKUPATA NA NITAKUPA KESI NINAYOTAKA MIMI “ Mwisho wa kunukuu .
Mwisho, Ninamshukuru kijana aliyerekodi tukio lote kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hivi tutanza kusambaza video cd hizo Nchi ili watanzania wajue ukweli na Mh Rais aone utendaji mbovu wa wateule wake na vile nilitake Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria , maadili ,taratibu na kanuni za kazi na sio kuendesha Jeshi kwa matakwa ya kisiasa , kufanya hivi ni kuhatarisha usalama na utulivu wa Nchi yetu .
“ Che Guavera alisema “ if you tremble indignation at every injustice then you are a comrade of mine “
Wanafunzi jipeni moyo bado kitambo kidogo Taifa hili litabadilika .
Godbless J Lema ( MP)
25/4/2013.
Chanzo: Mtandao wa kijamii wa CHADEMA.
Thursday, April 25, 2013
UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA JUU YA AZIMIO LA MALI
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa
kupigia kura azimio linalopendekeza kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani
nchini Mali.
Kikosi hicho chenye wanajeshi 12,600
kinajumuisha takriban wanajeshi 6,000 kutoka nchi za Magharibi mwa
Afrika ambazo tayari zina wanajeshi wao nchini humo.Azimio hilo limependekezwa na Ufaransa ambayo iliingilia kati mzozo wa Mali mnamo mwezi Januari ili kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Mali mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya uchaguzi mkuu.
Hata hivyo duru zinasema kuwa azimio hilo limezua mjadala mkali.
Makundi ya kiisilamu yaliweza kutumia pengo la usalama lililotokea baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka jana na kuanza kushinikiza watu kufuata sheria za kiisilamu.
Miji iliyo Kaskazini mwa nchi, imeweza kudhibitiwa na jeshi la Ufaransa lakini baadhi ya wapiganaji wangali katika maficho yao.
Ufaransa ilianza kuondoa baadhi ya wanajeshi wake 4,000 mapema mwezi huu kutoka nchini humo, lakini imekuwa ikishinikiza Umoja wa Mataifa kupeleka wanajeshi wake.
Aidha wanajeshi wa Chad, wanasemekana kuwa wenye uzoefu mkubwa zaidi katika kupambana na wapiganaji jangwani, lakini nchi hiyo pia imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali.
Sababu ya kikosi cha Umoja wa mataifa ni kulinda amani na kitakuwa na wanajeshi 11,200, pamoja na polisi 1,440.
Lengo lake kuu litakuwa kuweka uthibiti katika baadhi ya sehemu za Kaskazini mwa Mali ili kumaliza vitisho kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Hata hivyo rasimu ya azimio hilo haisemi ikiwa wanajeshi hao wataweza kupigana na wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, lakini wanajeshi 1,000 wa Ufaransa,wataweza kusalia Mali.
Chanzo :BBC
Subscribe to:
Posts (Atom)