Saturday, April 20, 2013

MBOWE - SPIKA ANAENDESHA BUNGE KIDIKTETA

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema kuwa Spika wa Bunge, Anne Makinda analiendesha Bunge kidikteta.
Alisema vurugu na ghasia zinazotokea bungeni wakati wa mijadala mbalimbali zinatokana na spika na naibu wake Job Ndugai kutaka kuliendesha Bunge kidikteta kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai alitoa kauli hiyo jana kupinga uamuzi wa spika wa kuridhia adhabu iliyotolewa na Ndugai dhidi ya wabunge sita wa CHADEMA.
Wabunge hao ambao walitolewa bungeni na kuzuiliwa kuhudhuria Bunge kwa siku tano ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Awali akisoma uamuzi wake jana bungeni kufuatia mwongozo alioombwa na Mbowe, Spika Makinda alisema uamuzi uliofanywa na naibu wake, Ndugai ni sahihi.
Ndugai aliamuru Lissu atolewe nje kwa kukiuka kanuni ya 60 (12) wakati aking’ang’ania kutoa mwongozo wakati naibu spika akimzuia.
Makinda alisema adhabu hiyo ilitokana na kukaidi agizo la kiti la kumtaka kukaa wakati alipompatia nafasi Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga (CHADEMA).
Alisema wabunge wengine watano walipewa adhabu hiyo kwa kosa la kuwazuia wapambe wa Bunge kutekeleza agizo la naibu spika la kutaka kumtoa nje Lissu na kusababisha fujo.
“Waheshimiwa wabunge, kanuni zetu na hasa ya 2 (2) na kanuni ya 5(1) ya kanuni za Bunge imempa mamlaka spika kufanya uamuzi pale ambapo hakuna utaratibu wa kanuni.
“Aidha uamuzi unaofanywa na spika ambao unaruhusu uendeshaji bora wa shughuli za Bunge wa kuleta amani na utulivu bungeni, unaingizwa kwenye kitabu cha maamuzi ili kuongoza mwenendo wa baadaye wa uendeshaji wa Bunge.
“Kwa kitendo kilichotokea Aprili 17 bungeni, hakiwezi kupuuzwa kwa kuwa ni kitendo dhahiri cha kudhalilisha mamlaka ya spika na kilikuwa kitendo cha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Watanzania wote waliushuhudia na wanalaani kilichokuwa kinaendelea ukumbini,” alisema Makinda.
Alifafanua kuwa mbunge yeyote aliyekuwa anaongoza Bunge wakati huo, angeweza kutoa uamuzi huo.
“Ninatumia kanuni ya 5(1) na kanuni ya 2 (2) ya Bunge inayompa mamlaka spika kufanya maamuzi ambapo jambo ama shughuli yoyote haikuwekewa masharti katika kanuni hizi.
“Uamuzi uliofanywa na mheshimiwa Job Ndugai, naibu spika wa kuwatoa nje Mheshimiwa Tundu Lissu…na kubaki nje kwa kutohudhuria vikao vya Bunge siku tano ni halali,” alisema na kuongeza:
“Na sasa utaingizwa katika kitabu cha maamuzi ya spika, na mbunge yeyote atakayefanya vitendo hivi apewe adhabu hii.”

Kauli ya Mbowe
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa mara baada ya uamuzi wa Spika Makinda, Mbowe alisema kama kiti cha spika hakitakuwa tayari kusimamia haki, wabunge wa CHADEMA hawataacha kusimama kuomba utaratibu wa kuzungumza kupinga hoja za upotoshaji za mawaziri na wabunge wa CCM na uendeshaji mbovu wa Bunge.
Alisema kanuni ya 2(2) na kanuni ya 5(1) ya kanuni za Bunge kweli inampa mamlaka spika kufanya uamuzi pale ambapo hakuna utaratibu wa kanuni.
“Kosa la wabunge wetu adhabu yake iko kwenye kanuni. Kanuni aliyotumia inahusu kwa mfano, wewe mwandishi wa habari umetoka sehemu yako, ukaingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kuanza kupigana.
“Hapo hakuna kanuni ya kukuadhibu na ndiyo spika anaweza kutumia hiyo kanuni na kisha kuingiza kwenye kumbukumbu ili iweze kutumika baadaye, lakini sio katika kosa la wabunge wetu,” alisema Mbowe.
Alisema uamuzi wa spika ni wa kitoto kwani amezidi kukoroga kanuni kwa ajili ya kumlinda naibu wake.
“Hatutangazi vita na Bunge, lakini kama Bunge halitakubali kufuata haki, wategemee hali hii kuendelea kujitokeza kwani hatutaogopa kufukuzwa kwa kupigania haki,” alisema.
Alisema Lissu alipata adhabu ya kutolewa nje na kufungiwa vikao vitano kwa sababu alisimama mara nyingi kuomba mwongozo na kutoa ufafanuzi wa hoja za kupotosha.
“Lissu au mbunge mwingine yeyote atasimama hata zaidi ya mara 100 kuomba kuzungumza, na tunafanya hivyo kutokana na wingi wa hoja za hovyo za serikali na wabunge wa CCM, na hakuna kanuni inayozuia kuzungumza mara nyingi, na katika hilo tuko tayari kufukuzwa wote,” alisema.
Mbowe alirejea kauli aliyoitoa juzi wakati akiomba mwongozo kuwa kilichotokea bungeni ni sintofahamu kati ya wabunge na kiti cha spika ambapo katika mambo ya msingi, CHADEMA ilitegemea kifungu cha nne cha kanuni za Bunge, kifungu kidogo cha kwanza kingetumika.
“Kifungu hicho kinasema hivi: ‘Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge, ikiwa;
Kwa maneno au vitendo, mbunge huyo anaonesha dharau kwa spika au mbunge huyo atafanya kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo’.
“Kosa la wabunge wetu linaangukia kwenye kanuni hii kwamba wameonyesha dharau pale walipokaidi kutoka nje. Kanuni iko wazi kwamba spika atapeleka majina ya wabunge hao kwenye Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge ambako watapewa nafasi ya kusikilizwa na kutoa ushahidi kabla ya kuhukumiwa,” alisema.
Mbowe alieleza kushangazwa na hukumu hiyo kwani hakuna mbunge wala kiongozi yeyote wa CHADEMA aliyeitwa kusikilizwa, na hata uamuzi wa spika nao haukuzingatia kuwahoji wahusika.
Aliitaka jamii kujiuliza kwanini wabunge hao wanapokutana nje ya Bunge ni marafiki wa karibu, lakini wakiingia ndani ya Bunge vurugu za kurushiana maneno hujitokeza.
“Huwezi kukuta wabunge nje wanagombana kwa sababu wanaheshimiana. Ndani ya Bunge chanzo cha hao wanaopatana nje kurushiana maneno ni kiti cha spika kushindwa kusimamia haki na kanuni,” alisema.
Hatua za kuchukua
Pamoja na Spika Makinda kuridhia adhabu ya Ndugai dhidi ya wabunge wa CHADEMA, Mbowe alisema wanatarajia kukata rufaa kwenye Kamati ya Kanuni kupinga uamuzi wa spika.
Alisema anajua CHADEMA itashindwa katika kesi hiyo, lakini wanataka kuweka rekodi na kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Alisema Spika Makinda kama ilivyokuwa kwa Ndugai, amekosea kuridhia adhabu hiyo.
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa Bunge limenajisiwa kwa kuruhusu watu wasiotakiwa kikanuni kuingia bungeni kiholela kwa nia ya kutaka kumtoa Lissu.
Akifafanua, alisema kisheria wanaoruhusiwa kuingia bungeni ni wabunge, uongozi wa Bunge na watumishi wao, na kama kuna mtu mwingine anataka kuingia lazima kanuni itenguliwe.
“Ukiacha rais ambaye ni sehemu ya mbunge, mtu yeyote haruhusiwi kuingia bila kutengua kanuni. Juzi Ndugai alivunja kanuni kwa kuruhusu askari kuingia bungeni wakati siwa iko mbele na hadi sasa hakuna taarifa iliyotolewa,” alisema.
Chanzo,Mtandao wa kijamii wa CHADEMA .

Friday, April 19, 2013

TANGAZO KUTOKA KWA DIAMOND JUU YA WATU WANAOTUMIA SOCIAL NETWORK KUFANYA UTAPELI KUPITIA JINA LAKE

Katika mtandao wa kijamii wa Msanii maarufu Diamond,ametoa tangazo linalotaadhalisha wanachi wasije tapeliwa.
Tangazo lenyewe hili hapa:-
 
"Napenda kuwataharifu fans wangu kuwa...kuna tabia imekuwa
 ikijotekeza kwenye social networks.
Tabia hiyo imekuwa ya kitapeli ya kufungua account
mbalimbali kupitia social networks
na kuanza kutuma massage za ajabu.....jambo ambalo
mimi binafsi sipendezwi nalo.....
nimelivumilia lakini nikaona isiwe vibaya nikiwajuza tena
 kuwa mkipata ujumbe wowote
kupitia social network kupitia jina langu kuomba
 msaada mtambue kabisa
si kweli......Jambo lolote kuhusiana na mimi binafsi utapata
 updates zangu kupitia
Account yangu ya facebook by Diamond platnumz ambayo ipo
 connected na tweeter
&Instangram pekee......lakini vinginevyo
sintousika na tuhuma zozote.....

Binafsi nimeshangzwa na ujumbe huu wa mtu ambae anatumia account facebook kwa jina
la Diamond platnum,kwa kuwasambazia ujumbe ufuatao:

KARIBU KTK PARTY YA KIMYA KIMYA YA KUMSHUKURU MAMA YANGU MPENDWA MAMA NASEEB.
KADI YA MWALIKO INAPATIKANA ATRIUM HOTEL BAADA YA KUTOA MCHANGO WAKO
ITAFANYIKA KTK MJENGO WANGU MPYA WA KISASA ULIOPO TEGETA NEXT WEEK.
THIS PARTY IS 4 ONLY INVITED PEOPLE..COZ IS SUPRIZING CELEBRATION PARTY
KADI ZINATOLEWA KUANZIA SAA 10JIONI HADI SAA3 USIKU MARA BAADA YA KUPOKELEWA MCHANGO WAKO.
MCHANGO NI KIASI CHOCHOTE NA UTUMWE KTK NAMBA YANGU YA TIGO.
KARIBU..
078889889 hy ndo namba yake
NB: MARA UTUMAPO MCHANGO WAKO UTAPOKEA SMS YENYE NENO LA SIRI AMBALO UNATAKIWA KUFIKA NALO KWA MUHUSIKA NA KULITAJA.
NIMEWEKA MCHANGO KUPUNGUZA IDADI YA WATU...
Niliuzunika sana kwa mambo kama haya bado kuendelea kufanyika kwenye social networks......
ni hayo tu my truly fans wa Diamond i hope mmeninyaka wote....... PEACE & LOVE"

FUATILIA UKUSANYAJI WA SAHIHI ZA KUMFUKUZA KAZI NAIBU WAZIRI MULUGO.



 Katika mtandao wa kijamii wa  http://www.frankmakange.com/petitions/ kuna ukusanyaji wa sahihi ili Rais Kikwete aweze kumfukuza kazi Naibu Waziri Phillipo Mulugo

Katika ukusanyaji huo,kuna maneno yafuatayo yanayoenda kwa Mh.Rais Kikwete:-

"Dear President Kikwete,
When you were elected President, Tanzanians expected you to provide good and strong leadership. Unfortunately, so far at least, we have not had the privilege of experiencing responsible and ethical leadership in action.
Mr. President, in the wake of what is unarguably the worst Form Four National Examination Results, I share the urgency that Tanzanians cannot accept an incompetent and information illiterate Philipo Augustino Mulugo as a Deputy Minister of an office expected to adhere to the highest standards of academic integrity.
Sir, holding onto a man who has turned out to be a public embarrassment and a national disgrace, confirms that your administration just wants to soothe public opinion and continue with business as usual.
Will you surprise us this time around? Mr. President, somewhere I read, “Hope is what makes us look foward to each and every day; without hope there is no tomorrow.” It is with this hope that I believe you are going to show leadership and sack Mulugo. Sack him! Mr. President, please do the right thing and sack Philipo Augustino Mulugo! It is not hard to see why unless you too think that, “…Tanzania was formed in one nineteen sixty four (11964) by unifying the Indian Ocean Islands of Zimbabwe and Pemba and the mainland country formerly known as Tanganyika.”
Sincerely,
[signature]"

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 12,2013

 Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.

Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.

Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata.

Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.

NANI KUWA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA ENGLAND KATI YA VAN PERSIE, BALE, SUAREZ, CARRICK, HAZARD NA MATA ???

Leo imetangazwa rasmi orodha ya wachezaji ambao wanagombania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya Uingereza - Man United imetoa wachezaji wawili, kiungo Micheal Carrick  na Robin Van Persie, Luis Suarez anaiwakilisha Liverpool, Gareth Bale, Juan Mata na Eden Hazard wakiliwakilisha jiji la london. Mabingwa watetezi Manchester City hawajatoa mchezaji hata mmoja katika listi hiyo iliyotangazwa leo.

Orodha yenyewe ni:-
Michael Carrick (Manchester United)
Gareth Bale (Tottenham Hotspur)
Robin van Persie (Manchester United)
Luis Suarez (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Juan Mata (Chelsea)


Washindi wa miaka iliyopita

2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Tottenham)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: C Ronaldo (Man Utd)

SPIKA AWATOSA CHADEMA,ABARIKI ADHABU WALIYOPEWA.

Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. 
 
Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.
 
Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bungeni kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.


Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu na wengine  watano na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge umebarikiwa na Mheshimiwa Spika..
 Hivyo Basi, maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua kanuni rasmi kwa tukio kama hilo na adhabu iliyotolewa.

KIPANYA NA BUNGE LA TANZANIA

Umeonaehhhhhhh!!!!!!

MWAKYEMBE-SERIKALI HAITAWAVUMILIA WAKANDARASI WABABAISHAJI

 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali haitawavumilia makandarasi wababaishaji  na wanaokiuka mikataba yao pindi wanapopata zabuni za kutekeleza miradi mbalimbali  nchini.
Pia, alitoa onyo kwa makandarasi wababaishaji ambapo amesema hatavumilia kuona Tanzania inafanywa kichaka cha watu wanaokuja kuchota fedha za bure na kuondoka pasipo kutimiza majukumu yao, ambayo yanakuwa yameainishwa kwenye mikataba wanayoingia na Serikali.
Waziri Mwakyembe alisema hayo  Dar es Salaam jana wakati akishuhudia   Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ikisaini mkataba wa ujenzi wa jengo  la tatu la abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza katika halfa  hiyo, Mwakyembe alisema ujenzi wa jengo hilo ni faraja kubwa kwa Serikali ya Tanzania, kwani litasaidia kuongeza ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira kwa Watanzania.
Alisema licha ya Serikali kupongeza jitihada hizo za TAA asingependa kuona ujenzi wa jengo hilo ukifanywa chini ya kiwango kwani huu ni wakati wa kuhakikisha kila kitu kinachofanyika nchini kinafanywa kwa viwango vya hali ya juu. Mwakyembe aliiagiza TAA kusimamia mradi huo uweze kumalizika kwa muda uliopangwa na kwamba idhibiti ubadhirifu wowote wa mali zitakazotumika katika mradi huo.
Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Suleiman Suleiman alisema ujenzi huo utafanyika kwa awamu mbili na kwamba hadi kukamilika kwa jengo  hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria milioni sita. “Jengo la abiria lina uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya milioni moja lakini tunapata faraja kwamba pindi ujenzi huu utakapo kamilika uwanja wa JNIA utakuwa na uwezo mkubwa wa kuchukua abiria wengi na kwamba ni faida kwa uchumi wa nchi yetu,”alisema Suleiman.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bam International Martin Bellamy alisema wamepata faraja kushinda zabuni hiyo na kwamba wao kama wenyeji hapa nchini watahakikisha wanafanikisha mradi huo. Jengo hilo linajengwa na Kampuni ya Bam Inenationali ya Uholanzi kwa gharama ya Sh275 bilioni ambapo hadi kukamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria milioni sita.

Chanzo, Mwananchi.

HATIMA YA TUNDU LISSU BUNGENI LEO.

Spika wa Bunge,Mh.Anne Makinda.
 Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema leo atatoa mwongozo kuhusu tukio la Naibu Spika, Job Ndugai kuwasimamisha wabunge sita wa Chadema.
Juzi, Ndugai aliwasimamisha wabunge hao Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje (Nyamagana) na Godbless Lema wa Arusha Mjini kutohudhuria Bunge kwa siku tano kutokana na alichokiita kufanya vurugu ndani ya bunge.
Hatua hiyo ya Spika Makinda imekuja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kumtaka aeleze Ndugai alitumia kanuni gani kuwasimamisha wabunge hao.
Jana, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbowe alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya 68(7) inayosema; “Hali kadhalika, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote ambapo hakuna mbunge mwingine anayasema na kuomba “Mwongozo wa Spika” kuhusu jambo ambalo limetokea bungeni mapema, ili Spika atoe ufafanuzi kama jambo hilo linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na majibu ya Spika yatatolewa papohapo au baadaye, kadri anavyoona inafaa.”
Mbowe alisema Kanuni ya 73(3) ndiyo inayompa ruhusa Naibu Spika na Spika kuwasimamisha wabunge na aliisoma: “Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda alipopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.
“Kwa mujibu wa yaliyotokea jana (juzi) ilitokea sintofahamu katika matumizi ya kifungu hiki wakati tulitegemea Kifungu cha 74(1) ndicho kingetumika kwani kama mbunge amedharau mamlaka ya Spika jina lake linaweza kupelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,” alisema Mbowe na kuongeza: “Mheshimiwa Spika nataka mwongozo wako kujua Naibu Spika alitumia kanuni gani?”
Awali, Spika Makinda aliahidi kutoa mwongozo wake baadaye jioni kabla ya kuahidi kufanya hivyo leo wakati akiahirisha shughuli za Bunge jana.
Awali, baada ya mwongozo wa Mbowe, Spika Makinda alimruhusu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuomba mwongozo wake na aliposimama alisema: “Mwongozo wangu uko palepale katika kanuni ileile iliyoombwa na kiongozi wa kambi ya upinzani.”
Kabla hajamaliza, Spika alimkatisha na kumweleza kuwa hawezi kutoa nafasi ya mwongozo wa kitu hichohicho.
Alimruhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema ambaye alisema: “Waandishi walioandika kanuni hizi kwamba jambo lilitokea mapema hawakumaanisha jana.”
Kabla Jaji Werema hajamaliza, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisimama lakini Spika alimzuia na kuwakatisha wote akisema: “Waheshimiwa wabunge, hakuna kitu kinachowaharibia wananchi kama kilichotokea jana (juzi), jana (juzi) hakuna kitu kilichojadiliwa zaidi ya kuleta zahama.”
Nchemba tena
Alimruhusu Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba kuendelea kutoa mchango wake ambao ulikatishwa kutokana na vurugu za juzi na jana nusura tena tafrani izuke kati yake na Mnyika hasa baada ya Nchemba kueleza suala la mabaraza ya Katiba kuwa utaratibu ulipitishwa bungeni na wabunge wote.
Alisema kinachotaka kujengwa na wapinzani hakipo kwa kuwa katika Jimbo la Karatu lililoko chini ya upinzani, wenyeviti wa mabaraza ya Katiba walichaguliwa wa CCM.
 
Mnyika alisimama akitaka kumpa taarifa Nchemba kwa kutumia Kanuni ya 63(1) akisema Mwigulu kueleza kuwa utaratibu wa kutumia mikutano ya maendeleo ya kata kuchuja wajumbe wa mabaraza WDC ulipitishwa na Bunge ni uongo kwa kuwa utaratibu huo ulipitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Spika alimruhusu Nchemba kuendelea kuchangia, ndipo aliposema: “Tunapoongea watoto wa kiume watulie.”
Kauli hiyo ilikataliwa na Spika Makinda ambapo alimtaka Nchemba kuifuta... “Naifuta mheshimiwa Spika,” alisema Nchemba.

Chanzo, Mwananchi.

MBOWE AHOJI UHALALI WA NEC KUANDAA MFUMO MPYA WA KUHESABU KURA.

 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amehoji hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuandaa mfumo mpya wa kisasa wa uhesabuji kura bila kuwashirikisha wadau.
Kutokana na hali hiyo, Mbowe aliitaka serikali kusitisha mchakato huo wa NEC hadi sheria itakapotungwa na kushirikisha vyama vya siasa.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mbunge wa Hai, alitoa kauli hiyo jana wakati akiuliza swali katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Akifafanua zaidi, Mbowe alisema kuna taarifa kwamba NEC imeanza kufanya maandalizi ya uhesabuji kura kutumia mfumo wa kisasa kama ule wa Kenya na Ghana.
Alisema mfumo huo wa kisasa wa uhesabuji kura umeshindwa kufanya kazi nchini Kenya na Ghana na kusababisha msumbufu mkubwa.
“Mheshimiwa Spika, mfumo huo ulifanyika nchini Kenya, lakini ulivurugika na kuamua kutumia mfumo wa zamani wa kuhesabu kura. Wadau wasiposhirikishwa katika hatua za awali, hautaweza kuaminika,” alisema.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Pinda, alisema ipo mifumo mingi ya uhesabuji kura, lakini hapa nchini kwa muda mrefu mfumo uliokuwa ukitumika ni ule wa kuhesabu kwa mkono.
“Hivi sasa baadhi ya nchi kama Kenya wanatumia mfumo wa kisasa. Nia ya NEC ni nzuri na bila shaka watakuwa na njia mbadala kama huu wa kisasa utashindwa kama walivyofanya wenzetu Kenya,” alisema Pinda.
Akiuliza swali la nyongeza, Mbowe alisema kwa kuwa mfumo huo ulishindwa Kenya na Ghana na kwa kuwa wadau hawakushirikishwa, waziri mkuu atakuwa tayari kutangaza kusitisha mchakato huo hadi sheria itakapopitishwa na kushirikisha wadau?
Akijibu swali hilo, Pinda alisema kuwa swali la Mbowe linatokana na hofu ambayo alisema haipo kwani hata kura zikihesabiwa kwa vidole hofu hiyo ilikuwa kubwa zaidi.
“Mimi nadhani tuamini kabisa kama NEC ina nia njema kwani imesheheni wataalamu wa aina mbalimbali. Ila hili la wadau kushirikishwa nitawasilisha wazo hilo tuone namna ya kuendelea vizuri na jambo hili,” alisema.
Katika hatua nyingine, Pinda alisema kuwa serikali itaruhusu shughuli za kisiasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara hadi hapo hali kuhusu mzozo wa gesi itakapokuwa shwari.
Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Mnyaa (CUF).
Mnyaa alihoji kwanini serikali ilipiga marufuku ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, katika mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wengine wanaruhusiwa.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema ziara ya Maalim Seif ilikuwa ya kisiasa na ndiyo maana alizuiliwa na viongozi wengine wote wa kisiasa wamezuiliwa.
“Hali itakapokuwa shwari, shughuli za kisiasa zitarejeshwa hivi karibuni na Maalim Seif na wengine wataruhusiwa kwenda kufanya kazi za kisiasa. Kwa sasa hapana,” alisema.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...