Friday, February 7, 2014

KUMBE MH. ZITTO KABWE NI MWALIMU, LEO AFUNDISHA SHULE YA MSINGI MUUNGANO - UJIJI KIGOMA.

Mh.Zitto akifundisha Hisabati
Katika juhudi za Ufuatiliaji wa vitabu vya 'change ya radar' shule ya msingi Muungano, Manispaa ya Kigoma-Ujiji. Baadhi ya vitabu watoto wamepata Leo asubuhi (Jiografia darasa la saba). 

BUNGE LA KATIBA KUANZA VIKAO FEBRUARI, 18.

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto), akizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa baada ya kuhutubia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa CUF,  Maalim Seif Sharrif Hamad na kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter Mziray. 



Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.
Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.
Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.
Bunge la Katiba linafanyika baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake ya miezi 20 kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya pili Katiba ambayo ilitolewa Desemba 30, mwaka jana.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo jana katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Rais Kikwete alisema kama wanasiasa wakikubaliana, hakuna mwananchi yeyote atakayepinga uamuzi utakaopitishwa na Bunge hilo.
“Nimeshauriana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein kuwa Bunge Maalumu la Katiba lianze vikao Februari 18, mwaka huu. Bunge hili litafanyika kwa siku 70 na kama mambo yatakuwa hayajamalizika zinaweza kuongezwa siku 20,” alisema Rais Kikwete.

Thursday, February 6, 2014

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA BAADA YA MICHEZO YA JANA.

Vodacom Premier League VPL 2013/2014
Rank
Teams
PlayedWinsDrawLostGDGoal scorePoints
1Azam FC161060192936
2Yanga SC161051223435
3Simba SC16871183231
4Mbeya City1687192131
5Mtibwa Sugar1657412022
6Kagera Sugar1656501521
7Coastal Union16310331119
8Ruvu Shooting1547401619
9JKT Ruvu15609-61318
10Ashanti UTD16349-141413
11Rhino Rangers16268-91112
12JKT Oljoro16268-141212
13Prisons FC14176-10610
14Mgambo Shooting162410-19710

NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. AMOS MAKALA AKAGUA MIRADI YA MAJI MOROGORO.

Naibu Waziri Mh.Amos Makala akiongea na wafanyakazi wa MORUWASA
Naibu Waziri wa Maji Mh.Amos Makala jana ameanza zira ya siku 4 ya kukagua miradi ya maji katika Mkoa wa Morogoro. Naibu waziri ameongelea zaidi juu ya Wakandarasi waliopewa kazi ya ujenzi wa Miradi ya maji na wakashindwa kuikamilisha kwa wakati huku wakitoa visingizio amewaagiza awakute katika vituo vyao vya kazi tofauti na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kuhusu changamoto zinazoikabili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Naibu waziri ameahidi kutoa ushirikiano ili wakazi wa Manispaa ya Morogoro waweze kupata huduma ya maji ya kutosha.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA alimueleza Naibu Waziri kuwa MORUWASA inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kuongezeka gharama za uendeshaji kutokana na kupanda gharama za umeme, gharama za madawa, pia upungufu wa maji katika vyanzo vya maji kutokana na uchafuzi wa mazingira. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Kaimu Mkurugenzi huyo alimuambia Naibu Waziri kuwa MORUWASA inajitahidi kutoa huduma kwa wakazi wa Morogoro.

Wednesday, February 5, 2014

Azam FC kucheza mechi za kimataifa Azam Complex Chamazi.


Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki  kuruhusiwa kuandaa (ku-hostmashindano makubwa ya vilabu

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...