Thursday, February 6, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. AMOS MAKALA AKAGUA MIRADI YA MAJI MOROGORO.

Naibu Waziri Mh.Amos Makala akiongea na wafanyakazi wa MORUWASA
Naibu Waziri wa Maji Mh.Amos Makala jana ameanza zira ya siku 4 ya kukagua miradi ya maji katika Mkoa wa Morogoro. Naibu waziri ameongelea zaidi juu ya Wakandarasi waliopewa kazi ya ujenzi wa Miradi ya maji na wakashindwa kuikamilisha kwa wakati huku wakitoa visingizio amewaagiza awakute katika vituo vyao vya kazi tofauti na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kuhusu changamoto zinazoikabili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Naibu waziri ameahidi kutoa ushirikiano ili wakazi wa Manispaa ya Morogoro waweze kupata huduma ya maji ya kutosha.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA alimueleza Naibu Waziri kuwa MORUWASA inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kuongezeka gharama za uendeshaji kutokana na kupanda gharama za umeme, gharama za madawa, pia upungufu wa maji katika vyanzo vya maji kutokana na uchafuzi wa mazingira. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo Kaimu Mkurugenzi huyo alimuambia Naibu Waziri kuwa MORUWASA inajitahidi kutoa huduma kwa wakazi wa Morogoro.
Mh.Makala akiwa anaingia katika Ofisi za MORUWASA

Mh.Makala akiwa anasaini kitabu cha wageni 

Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA Mhandisi Halima Mbiru akiwa anatoa taarifa kwa Mh.Naibu Waziri wa Maji.

Wafanyakazi wa MORUWASA wakiwa wanamsikiliza Naibu Waziri wa Maji Mh.Amos Makala.

Mtaalamu Mshauri wa mradi wa MCC mjini Morogoro akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA wakati Naibu Waziri alipotembelea kituo cha kutibia maji cha Mafiga.

Naibu Waziri akizunguka na kukagua mitambo ya kutibia maji Mafiga.

Naibu Waziri akimsikiliza Mtaalam Mshauri wa Mradi wa Maji chini ya MCC katika mitambo ya kutibu maji ya Mafiga.

Naibu Waziri akisaini kitabu cha wageni katika eneo la mitambo ya Mafiga.

Hii ndiyo mitambo ya Kuchuja, kusafisha na kutibu maji ya Mafiga.

Naibu Waziri akikagua mitambo ya kusukuma maji Mafiga.



Naibu Waziri akikagua birika la maji lililojengwa katika chanzo cha maji cha Mambogo

Naibu Waziri akikagua ujenzi wa Mitambo ya kutibu maji iliyojengwa upya katika chanzo cha maji cha Mambogo.

Kaimu Mkurugenzi wa MORUWASA akiwa anamuonesha Naibu Waziri uharibifu wa Mazingira katika Milima ya Uluguru

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...